India kukaa nje ya jukwaa la biashara ya Indo-Pacific

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
319
345
LOS ANGELES:

INDIA imechagua kujiondoa kujiunga na Jukwaa la biashara ya Mfumo wa Uchumi wa Indo-Pacific (IPEF) kwa hoja zake halali kuhusu uwezekano wa masharti yaliyowekwa sambamba na masuala kama vile mazingira na kazi.

Waziri wa Biashara wa Muungano Piyush Goyal aliorodhesha sababu za kufikia uamuzi huo kuwa ni kuundwa kwa sheria za data katika biashara ya kidijitali kulinganisha na manufaa ambayo India itayapata kama nchi inayoendelea kiuchumi

Hata hivyo India itaendelea kujihusisha na kongamano la wanachama 14 kuhusu suala hili, uamuzi wa mwisho utachukuliwa kwa kuzingatia "maslahi ya kitaifa ya watu wake na biashara." IPEF ina jukwaa katika ngazi nne ambayo ni biashara,njia za usambazaji, nishati safi-decarbonisation-miundombinu na ushuru na kupambana na rushwa.

Jukwaa hilo inazipa nchi hizo 14 ambazo ni wanachama uhuru wa kuchagua ni jukwaa lipi watashiriki

Piyush Goyal alisema baada ya mkutano wa mawaziri wa IPEF kilichofanyika hapa Ijumaa: "Tulifurahishwa sana na ujumbe wa matokeo ya mwisho, na nimejiunga na matamko ya mawaziri juu ya mihimili mitatu inayohusiana na ugavi, kodi na kupambana na rushwa na nishati safi.

Kuhusu biashara, makubaliano mapana bado hayajajitokeza miongoni mwa mataifa kuhusu masuala kama vile makubaliano kuhusu mazingira, kazi na ununuzi wa umma.”

"Bado hatujaona ikiwa kuna masharti yoyote. Kwa mfano, kwa upande wa mazingira hii inaweza kubagua mataifa yanayoendelea ambayo yanapaswa kutoa gharama ya chini na nishati ya bei nafuu ili kukidhi mahitaji ya uchumi unaokua.

Huku ikiendelea kushirikiana na IPEF kuhusu biashara, India itasubiri mpaka wa mwisho kabla ya kuamua (kujiunga na jukwaa hili). Uamuzi utachukuliwa kwa kuzingatia maslahi ya watu na biashara zetu."

Wasiwasi wa India ni kuhusu maswala kama vile kuunganisha mazingira na wafanyakazi na biashara na kuwa na masharti ya lazima sawa.

“Kuna baadhi ya majukumu ambayo nchi zilizoendelea inazo. Wakati huo huo huu ulikuwa mkutano wa kwanza wa mawaziri wa kibinafsi wa IPEF ambao uliundwa miezi michache nyuma.

“Ninapongeza kasi ambayo imechora mstari wa siku zijazo. Hii ni rekodi ya aina yake na hatujawahi kuona kasi kama hii.”

Katibu wa biashara wa Marekani Gina Raimondo na Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Balozi Katherine Tai wameungaa mkono hoja hiyo ya India.

Kwa pamoja kundi hili la nchi 14 litaamua hatima ya nchi wanachama 14 katika siku zijazo,” Goyal alisema India pia iko katika harakati za kuimarisha mfumo na sheria zake za kidijitali, hasa kuhusu faragha na data.

Alisema kuwa matokeo ya IPEF yatasababisha kuundwa kwa ajira katika nchi zote wanachama na kusaidia biashara za ndani kupitia minyororo ya ugavi inayostahimilika.

"India imejihusisha kikamilifu katika mikondo yote mbalimbali ya majadiliano…. Tunaamini kwamba (kuna) majukumu fulani ya ulimwengu ulioendelea. Hilo ni suala ambalo litahitaji ushiriki wa kina na mashauriano zaidi,”
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom