India: Mke ajiua baada ya kudhihakiwa na mumewe kuwa ngozi yake ni nyeusi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mwanamke mmoja nchini India mwenye miaka 21 anadaiwa kujiua kutokana na kudhalilishwa na mumewe kwa sababu ya ''rangi nyeusi'' ya ngozi yake.

Polisi wa jimbo la Rajasthan wamefungua kesi dhidi ya mume wa mwanamke huyo baada ya baba wa marehemu kumshutumu mume kuwa chanzo cha kifo cha binti yake.

Polisi wameiambia BBC India kuwa mwanaume huyo hajakamatwa. Na mume akiwa bado kutoa taarifa kuhusu shutuma dhidi yake.

Raia wengi wa India wana mtazamo kuwa rangi nyeupe ni watu wa tabaka la juu kuliko wahindi weusi.

Baba wa mwanamke huyo aliiambia polisi kuwa mume wa binti yake mara kwa mara alikuwa ''akimdhalilisha kwa sababu ya weusi wa ngozi yake'', vitendo ambavyo vilimfanya ayakatishe maisha yake.

Hii si mara ya kwanza kwa vitendo vya dhihaka dhidi ya wanawake wa India wenye rangi nyeusi kutokea na kusababisha vifo.

Mwanamke mmoja mwenye miaka 29 alijiua mwaka 2014 baada ya mumewe kudhihaki rangi ya ngozi yake, polisi wameeleza.

Na mwaka 2018, binti wa miaka 14 alijiua baada ya wanafunzi wenzake kumzomea kuwa ana ''muonekano mbaya'' kwa sababu ya rangi ''nyeusi '' ya ngozi yake.
 
Naomba tenda ya kupeleka kuni kwa Mnyazi Mungu amuoneshe kazi huyo dada marehemu
 
Mbona sisi wasukuma huwa tunachambwa sana kuwa ni washamba lakin hata hatujiui tunaendelea kudunda tu
 
Back
Top Bottom