India kupiga marufuku talaka za kiislam

India kupiga marufuku talaka za kiislam

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,050
Reaction score
12,966
Nchi ya india iko katika hatua za mwisho za kupitisha sheria itakayopiga marufuku talaka za kiislam.

Bunge la nchi hiyo liko katika hatua za mwisho kupiga marufuku utaratibu wa waislam wa kutoa talaka kienyeji kwa mwanaume kutamka tu mara tatu neno talaka kwa mke wake.

Sheria hiyo itatoa adhabu ya miaka 3 jela kwa atakaekiuka.

Mimi binafsi nawapongeza wahindi, hizi taratibu za ndoa za kidini zimekua zikinyanyasa wanawake na kuwanyima haki zao za msingi.

Kumpa talaka mke/mume ni haki ya huyo anaetaka kifanya hivyo ila utaratibu wa kisheria ufuatwe na huyo alieachwa apate haki zake za msingi.

Triple talaq: India moves to criminalize Muslim instant divorce - CNN
 
MTU akifikia kutamka talaka maana yake nafsi imemkataa mwenza..kupewa talaka si kuonewa,kung'ang'ania kugawana Mali sawasawa wakati mke alikua nyumbani tu pengine akigawa uchi kwa watu wengine ni dhulma..wanawake mnaweza,tafuteni vyenu
 
Haki ya mtu waliotalikiana ni tofauti sana na mukhtadha mzima ya talaka.

Kupiga marufuku taraka sio ufumbuzi, kwa sababu dini ya kiislam wanandoa wakishindwana huruhusiwa kuachana, kitendo tu cha kutamka si mke tena hapo habar imekwisha.

Na mtu anaonewa vipi kwa kupewa talaka! waendelee kuishi pamoja na hata wamefikia hatua ya uadui!

Labda tatizo liwepo kwenye kugawana mali, na hapa kama kidini taratibu zifuatwe, na kama sio kidini pia zifuate.

Ila kwa imani ya Kislam kutalakiana na swala linaloluhusiwa, sasa kuja na hiyo sheria nikuingilia dini husika.
 
Uislam unanyanyasa wanawake tangu uasisi wake.

Ni wanawake wengi wa kiislam huwa wanacomplain hilo pamoja na suala la kuletewa wake wenza.

Wabillah Tawfiq,
 
wananyanyaswa vipi!?..uislam unamtaka mwanaume ndiye amlishe,amvishe na ampe malazi mwanamke..wakati huohuo kipato cha mwanamke ni chake halazimiki kuhudumia familia..anapoolewa apewe mahari yake..sasa hapo nani anakandamizwa kati ya mwanaume na mwanamke!?
 
Hapo Mwanaume hajakandamizwa, ila ametimiza majukumu yake.

Halafu, wewe umeongelea kupitia references ambayo ni jinsi Qur'an inavyotaka ILA mimi nimeongelea uhalisia wa hali halisi maishani.

Mwanamke Muislam KHASA! atakupenda na kukuheshimu sana kama mumewe mkiwa wawili ndoani. LAKINI utakapomwambia habari ya kuongeza Mke / Wake mara nyingi hawafurahii hilo.

Kwanini? Kwasababu nao ni binadamu na wana WIVU.

Wivu ni inborn behaviour inayoambatana na Mapenzi.

Wivu upo kwa Watu wa Dini zote na hata kwa Wanyama.

Hili suala la Wivu mnalishughulikiaje kwa Wanawake wa kiislam?
 
Uislam unanyanyasa wanawake tangu uasisi wake.

Ni wanawake wengi wa kiislam huwa wanacomplain hilo pamoja na suala la kuletewa wake wenza.

Wabillah Tawfiq,
we mgalatia acha kuropoka utumbo kisha kuhitimisha Uharo wako na Kauli tukufu.
utalaanika.

Nionyeshe Imani moja tu kabla ya Uislamu iliotoa haki ya Mwanamke kurithi mali .
na iliompa uhuru mwanamke kuchagua wa kumuoa.

Au unataka tugeuzs uzi? mtoto huna nidhamu kweli kweli wewe.
 
Unajua maana ya Wabillah Tawfiq?

Kuna ubaya kutamka meneno hayo?
 
Hapo Mwanaume hajakandamizwa, ila ametimiza majukumu yake.

Halafu, wewe umeongelea kupitia references ambayo ni jinsi Qur'an inavyotaka ILA mimi nimeongelea uhalisia wa hali halisi maishani.

Mwanamke Muislam KHASA! atakupenda na kukuheshimu sana kama mumewe mkiwa wawili ndoani. LAKINI utakapomwambia habari ya kuongeza Mke / Wake mara nyingi hawafurahii hilo.

Kwanini? Kwasababu nao ni binadamu na wana WIVU.

Wivu ni inborn behaviour inayoambatana na Mapenzi.

Wivu upo kwa Watu wa Dini zote na hata kwa Wanyama.

Hili suala la Wivu mnalishughulikiaje kwa Wanawake wa kiislam?
wanakandamizwa vipi sasa..mbona huelezi!?..kimsingi wivu ni ubinafsi,anaeolewa ni mwanamke,anaeona wivu/mbinafsi ni mwanamke..kama muumini wa kiislam mke mwenza hawezi kuwa tatizo..
 
Sasa kama mtu kakuchoka kakwambia hakutaki utamlazimisha .
Hata wakristo wenyewe kuna mda wanatamani kuachana na wenzao kwa kuchokana ila Sheria zinawabana
 
Unajua maana ya Wabillah Tawfiq?

Kuna ubaya kutamka meneno hayo?
unaweza kutoa kashfa kwa wagalatia wenzako ukamalizia na Haleluyah?

jifunze matumizi ya.Lugha Kijana. na epuka kukashifu Imani usioijua. kesho unaweza kupata Shemeji wa Kiislamu akaoa Dadako.

Sio tabia njema hio.
 
Nchi ya india iko katika hatua za mwisho za kupitisha sheria itakayopiga marufuku talaka za kiislam.

Bunge la nchi hiyo liko katika hatua za mwisho kupiga marufuku utaratibu wa waislam wa kutoa talaka kienyeji kwa mwanaume kutamka tu mara tatu neno talaka kwa mke wake.

Sheria hiyo itatoa adhabu ya miaka 3 jela kwa atakaekiuka.

Mimi binafsi nawapongeza wahindi, hizi taratibu za ndoa za kidini zimekua zikinyanyasa wanawake na kuwanyima haki zao za msingi.

Kumpa talaka mke/mume ni haki ya huyo anaetaka kifanya hivyo ila utaratibu wa kisheria ufuatwe na huyo alieachwa apate haki zake za msingi.

Triple talaq: India moves to criminalize Muslim instant divorce - CNN
Ndg unavosema inakandamiza w.wke ur wrong!1st talaka c lazima atoe mmme thgh imezoeleka hvo ...ht mmke akiwa hamtaki mume anaweza kuandika talaka(chunguzeni mjue?
2nd hmn anaekandamizwa as km ni mali kuna sheria ya kugawana
3rd kuendelea kuishi p1 yl mna misunderstanding ni kukandamizwa zaid psychological ambalo linaweza sababisha depression na hypertension
 
Waislamu India wananyanyasika kweli, Muhindi akimuua Muislam anaonekana ni shujaa. Siku zilizopita Muhindi mmoja alimuua Muislam kisa kilikuwa ni Ng'ombe jamaa aliyetekeleza mauaji alichangiwa pesa nyingi kwenye Account yake mpaka ikafungwa
 
MTU akifikia kutamka talaka maana yake nafsi imemkataa mwenza..kupewa talaka si kuonewa,kung'ang'ania kugawana Mali sawasawa wakati mke alikua nyumbani tu pengine akigawa uchi kwa watu wengine ni dhulma..wanawake mnaweza,tafuteni vyenu
Unapoandika haya mfikirie mama yako angepewa talaka ungejisikiaje?chukulia unaumri mdogo.....na yeye ni housewife....na si ajabu alikuwa na kazi ila baba yako akamwachisha akae home!
 
Binadamu wa sasa hatufati misingi ya dini si waisilamu wala wakristo kama tukifuata misingi ya dini kutakuwa hakuna talaka. Sisi dini tuko nazo tu kwakuwa tumezaliwa waisilamu au wakristo basi tumemaliza misingi ya dini hatufati utasikia sisi waisilamu tumeruhusiwa kuoa na kuacha, sio kirahirahisi na mna hiyo ndoa ina misingi yake Uisilamu una misingi yake, tukifanya mambo yetu tusiishirikishe dini si Uisilamu wala Ukristo.
 
Unapoandika haya mfikirie mama yako angepewa talaka ungejisikiaje?chukulia unaumri mdogo.....na yeye ni housewife....na si ajabu alikuwa na kazi ila baba yako akamwachisha akae home!
hata angekua mama yangu..utamlazimishaje MTU kuishi na MTU ambaye hataki tena kuishi nae!?
 
Uislam unanyanyasa wanawake tangu uasisi wake.

Ni wanawake wengi wa kiislam huwa wanacomplain hilo pamoja na suala la kuletewa wake wenza.

Wabillah Tawfiq,
ushauri kwa anaeona uislam mgumu ahamie kwenye ukristo. very simple
 
Back
Top Bottom