Inawezekana?

Elizabeth Dominic

Platinum Member
Dec 7, 2007
4,555
3,649
Salamu, hivi ukishazaa na kuachika unaweza kupata mwanaume mzuri akakupenda wewe na watoto wako maana watu wanasema eti ukishazaa thamani inapungua. Nisaidieni jamani i'm a single mother and i believe i'm attractive but nimekata tamaa ya kupendwa.
 
Aiseeee!

Kwanini umekataa tamaa ya kupendwa bibie?!Labda kama una sababu nyingine zaidi ya kuzaa maana watu wanaolewa wakiwa na timu zao na wanapendwa na kuheshimiwa kama wengine tu.Yani kama ni hiyo tu inayokupa presha SAHAU.Fungua akili yako kwamba utapendwa utakapokutana na wako wa kukufaa na utakaemfaa....swala la kupoteza thamani ni la kufikirika zaidi!!!Kama mvuto wako wa sura/umbo na wa tabia unaendana ondoa hofu....
 
Mara nyingi wanaume wanachukulia " Mfupa uliomshinda fisi mimi nitauweza?" lakini nadhani hii ni mtazamo tu. Wewe jaribu kujitambua kuwa una nafasi gani kama mwanamke kitu ambacho wengi kinawashinda, kuwa na watoto sidhani kama ni kipingamizi labda uwe nao wengi kiasi cha kuathiri uchumi wako na huyo atakayekupenda kukuoa. Ushauri, unatakiwa ujipende, ujielimishe sio lazima darasani ujue ulimwengu unaendeleaje na usiwe mvivu wa kufikiri kiasi kwamba mtu akiongea na wewe u-synchronise naye.
 
Kwa nini unafikiri ili mtu akupende inabidi uwe attractive? Love is myth..huwezi kujua ni kwa sababu gani mtu anakupenda.. Kuna vitu vingi sana na kuna uwezekano hivyo unavyovihisi havipo!

Jitulize kwa imani yako..kama imeandikwa..basi itakuwa hivyo!
 
Wako wanaume wengi tu wanaweza kukupenda wewe pamoja na wanao. Usikate tamaa mapema mapema.
 
Salamu, hivi ukishazaa na kuachika unaweza kupata mwanaume mzuri akakupenda wewe na watoto wako maana watu wanasema eti ukishazaa thamani inapungua. Nisaidieni jamani i'm a single mother and i believe i'm attractive but nimekata tamaa ya kupendwa.
una umri gan? Na watoto wangap? Na unaish wapi?
 
Sasa m2 umeisha zeeka nani akutake tena!?
wewe kwanini unmwambia ivi mwenzio?
amezeeka umemwona?
kuzaa mtoto ndo kuzeeka ..ata km amezaa na miaka 26 ndo kazeeka?
usimvunje moyo mwenzioo..tabia mbaya tu mwone vile
 
Back
Top Bottom