Inawezekana vipi mtu akajiajiri ambapo hajawahi kuuza hata karanga? Serikali acheni porojo, toeni ajira kwa wahitimu

mtamba b

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
317
1,000
Kichwa cha habari kinajieleza vizuri.

Hizi story za kujiajiri ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa serikali ambao wao ni waajiriwa zinaumiza sana.

Haiwezekani nipo shuleni kuanzia Nina umri wa miaka 6 Mpaka leo Nina miaka 25/26 then uje uniambie nijiajiri.

Najiajiri Nini Sasa?

Inaudhi sana.
 

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,912
2,000
Kichwa Cha habari kinajieleza vizuri
Hizi story za kujiajiri ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa serikali ambao wao Ni waajiriwa zinaumiza Sana.
Haiwezekani nipo shuleni kuanzia Nina umri wa miaka 6 Mpaka leo Nina miaka 25/26 then uje uniambie nijiajiri
Najiajiri Nini Sasa?
Inaudhi sana.
We ni tatizo kabisa ktk nchi hii.

Kila mwaka vyuo vinatoa wahitimu,unadhani ajira za kuwatosha wote zinatoka wapi ktk nchi hizi za kiafrika masikini?

Unapaswa kujiongeza kwa akili ya kuzaliwa kwamba juhudi zako hazitegemei mawazo ya wengine wawaze cha kufanya ili wakuajiri wewe ,unapoambiwa tegemea akili yako,juhudi na maarifa ndiyo tafisiri ya neno "KUJIAJIRI "

Kaa hapo unasubiri serikali utakufa masikini
 

mtamba b

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
317
1,000
Cha kushangaza wao wanapishana na mav8 kuroga ili wabakie hapo na hawataki kuja kujiajiri ili kupisha hizo nafasi wakae wengine
Mungu anawaona
Utasikia sijui kamatia fursa yani tunawazoom tu,
So ndo hapo.
Inashangaza Kuna watu wanawasapoti humu

Hakuna mtu anaweza kujiajiri bila sapoti
Watoe basi hata mitaji
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
43,740
2,000
We ni tatizo kabisa ktk nchi hii.

Kila mwaka vyuo vinatoa wahitimu,unadhani ajira za kuwatosha wote zinatoka wapi ktk nchi hizi za kiafrika masikini?

Unapaswa kujiongeza kwa akili ya kuzaliwa kwamba juhudi zako hazitegemei mawazo ya wengine wawaze cha kufanya ili wakuajiri wewe ,unapoambiwa tegemea akili yako,juhudi na maarifa ndiyo tafisiri ya neno "KUJIAJIRI "

Kaa hapo unasubiri serikali utakuta masikini


Hawa ndo unakuta wanatembea na bahasha halafu nauli wanapewa na wadogo zao wanao uza maji au kutengeneza makochi..
Wao akili zao zote ni kuajiriwa na kulaumu serikali...
 

Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,171
2,000
natamani kutoa darasa na kwa mifano tena kwa vijana yaani tuanze nadharia kisha vitendo nauhakika nikiwa na vijana 50 baada ya miezi sita tunaweza kuwa sehemu fulani na baada ya miaka miwili 25% wanaweza kumiliki biashara zao wenyewe ikiwemo 10% walioajiri watu wawili kila mmoja.
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
43,740
2,000
Yes walitakiwa watoe hata mtaji na sio maneno tu,,

Mtaji gani mnataka wakati shule mmeenda na nguvu mnazo?

Hamuwaoni wenzenu hawajaenda shule lakini wanaosha Tu miguu wakina dada na kukunja hadi 150k kila siku??

Wewe why usijiunge huko?

Wanaouza maji mitaani huwaoni?
Unajua wanaigiza ngapi kwa siku?

Nikikwambia ajira unayoitafuta mshahara wake hautafika hata nusu
Ya wanachopata waosha miguu
Utaamini?
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,065
2,000
Natoa wito kwa vijana mjitambue andamaneni Kudai haki yenu ya kupewa ajira na serikali ya Tanzania hii ya kihuni kihuni

Mwenye nacho anaongezea na asiyekuwa nacho ananyan'ganywa hata kidogo alichonacho hii roho ipae iende mpaka kwa vijana wanaomaliza JKT na kurudishwa mitaani kuja kusota kataeni huo ujinga kuna watu wanafaidi sana hii nchi mishahara na maposhoposho Kibao nyie mnatoka JKT mje kujiajiri hamna hata mitaji wawape mitaji hata mil 3 tatu ndiyo mje mtaani vinginevyo kataeni andamaneni fanyeni Fujo zisizo na mwisho nyie mnamafunzo polisi hawatawaweza piga polisi akileta kiherehere, mwisho wa siku hii nchi watu wote tutanufaika.

Pia nawaamsha na watumishi wa chini wenye mishahara midogo unafanya kazi nying mwisho wa mwezi mshahara wako haufiki hata million wakati kuna mtu kwa mwezi anapokea zaidi ya M 2 na maposhoposho Kibao kataeni huo utumwa kufanyishwa kazi na kulipwa kidogo nasema kataeni.

Pia polisi mjitambue na nyie acheni ujinga mnalala kwenye malindo kazi nying mishahara yenu ni midogo mno mkilinganisha na kazi mnazofanya ifike kipindi mjitambue wakubwa wenu wanafaidi sana nchi nyie wa chini mnatumika kuwanufaisha wa juu polisi na magwanda yako hayo unaishi maisha magum mshahara wako kiduchu ukilimganisha na hali halisi ya maisha, polisi huna hata gari la kumtembelea hujajenga mwaka wa tatu sasa uko kazin na zaid wewe unatumika tu

Leo hii ukifa ndani ya muda mfupi watoto wako wote walio na bima zitachukuliwa watabaki kupanga folen kupata matibu kataa huo utumwa

Nawahurumia sana polisi unakuta mtu anamaisha magum kuliko hata machinga wa barabaran bosi wake anakula na kubadili madem kila siku yaan acha niishie hapo yapo meng hata huko kwenye vyombo vingine ni hovyo mnadanganywa na reshen na vinywaji mishahara kiduchu Jinga sana nyie majamaa
Id yako thou🤫😪
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom