Inawezekana 'Herd Immunity' na hali ya hewa (Mazingira) ndio vitu vinavyotuokoa Watanzania dhidi ya COVID-19

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,062
144,498
Kwanza niweke wazi kuwa mimi si Daktari na wala sina utaalamu wa magonjwa ya kuambukiz bali nimetumia tu common sense na elimu ya kusoma vyanzo mbalimbali na hatimae ku-arrive at this conclusion:

Tuanze kwa kutazama herd immunity ni mini.

Herd immunity ni kinga inayotokana na sehemu kubwa ya jamii kuugua ugonjwa husika na baadae kujenga kinga dhidi ya ugonjwa huo au ni kinga kwa jamii baada ya sehemu kubwa ya jamii kuwa imepata chanjo hivyo kupunguza uwezekano wa watu wachache ambao hawana kinga katika jamii hiyo kuambukizwa ugonjwa huo.

Mtandao wa Wikipedia umeelezea hivi kuhusu Herd Immunity;

Herd immunity is a form of indirect protection from infectious disease that can occur with some diseases when a sufficient percentage of a population has become immune to an infection, whether through vaccination or previous infections, thereby reducing the likelihood of infection for individuals who lack immunity.

Kwanini inawezekana hali kuwa n hivyo kwa Watanzania?

Jibu ni rahisi tu nalo ni kwamba hatuchukua tahadhari za kutosha mlipuko unapotokea na matokeo yake wengi tunaugua ns baadae kupona na wengine kupata maambukizi bila kuonyesha dalali kutokana na uimara wa kinga zao ila mwisho wa siku sehemu kubwa ya jamii inakuwa imetengeneza kinga( herd immunity).

Kinachotokea ni watu wengi kupata maambukizi huku baadhi wakiugua na kupona na wengine kutoonyesha kabisa dalili huku wachache(hasa wazee na wenye matatizo fulani fulani ya kiafya)wakifariki na ushahidi wa kimazingira wa hali hii ni kipindi ambao vifo huwa vingi kuliko kawaida tena vikionekana ni vifo vya ghafla kwa walio wengi.

Nini hutokea baada ya hapo (Herd Immunity kuwa Developed)?

Kwa mtazamo wangu, kwakuwa kinga hii huwa si ya Kudumu, basi kuna wakati kinga hii huisha ila virusi vinakosa mazingira ya kuviwezesha kuendelea kutushambulia mpaka kipindi fulani cha mwaka(probably January to March) kijirudie ndio hali ya hewa huwa conducive kwa virusi hawa ku-survive na kutushambila na ndio maana kwa miaka hii miwili ya 2020 na 2021, milipuko na ongezeko la vifo vilijitokeza zaidi katika kipindi hicho kwa hii miaka miwili mfululizo.

Tusubiri tena kuanzia mwezi January mpaka mwezi March mwakani(2022) ili tuweze kujiridhisha na wakati huo huo tuombe kirusi kitachokuwa kimejibadilisha na kusubiri conducive environment kisiwe hatari kulik virusi vilivyopita.

Kwahiyo ni imani yangu si maombi, nyungu, malimao, pilipili wala tangawizi ndio vinavyotusaidia, badala yake ni herd immunity na hali ya hewa (mazingira) ndio vinavyotusaidia na si vinginevyo.

Vile vile ushahidi wa kimazingira unatuonyesha mazingira ya baridi sio factor kabisa kama inavyodaiwa kwani kipindi cha January mpaka March, si kipindi cha baridi kwa maeneo mengi ya nchi yetu, ila mlipuko huwa juu kipindi hicho. Hivyo, labda hali ya hewa ya joto ndio inaweza kuchangia kwani kwa mkoa kama wa Dar-es-Salaam kipindi hicho joto huwa kali zaidi.

Ni mtazamo wangu ingawa naamini utafiti unahitajika kupata ukweli na mambo mengine kuhusu hili gonjwa hapa nchini na mwenendo wake na hasa utafiti utaolenga kujua nini hutokea katika kipindi cha January mpaka March kinachopelekea maambukizi(ugonjwa) huu kuonekana unaongezeka.
 
Wimbi la Kwanza huwa la Wastani.

Wimbi la Pili huwa ndio komesha yao.

Wimbi la Tatu (au mengineyo, yakiwapo) huwa dogodinyo...
 
Umefanya research gani au umetumia kigezo gani kugundua kuwa Tanzania Corona haipo kwa kiwango kikubwa?
 
Kwanza niweke wazi kuwa mimi si daktari na wala sina utaalamu wa magonjwa ya kuambukiz bali nimetumia tu common sense na elimu ya kusoma vyanzo mbalimbali na hatimae ku-arrive at this conclusion:

Tuanze kwa kutazama herd community ni mini.

Herd community ni kinga inayotokana na sehemu kubwa ya jamii kuugua ugonjwa husika na baadae kujenga kinga dhidi ya ugonjwa huo au ni kinga kwa jamii baada ya sehemu kubwa ya jamii kuwa imepata chanjo hivyo kupunguza uwezekano wa watu wachache ambao hawana kinga katika jamii hiyo kuambukizwa ugonjwa huo.

Mtandao wa Wikipedia umeelezea hivi kuhusu herd community:

Herd immunity is a form of indirect protection from infectious disease that can occur with some diseases when a sufficient percentage of a population has become immune to an infection, whether through vaccination or previous infections, thereby reducing the likelihood of infection for individuals who lack immunity.

Kwanini inawezekana hali kuwa n hivyo kwa watanzania?

Jibu ni rahisi tu nalo ni kwamba hatuchukua tahadhari za kutosha mlipuko unapotokea na matokeo yake wengi tunaugua na baadae kupona na wakati huo huo tunakuwa teyari tumejenga kinga katika mbili yetu.

Kinachotokea ni watu wengi kupata maambukizi huku baadhi wakiugua na kupona na wengine kutoonyesha kabisa dalili huku wachache(hasa wenye matatizo fulani fulani ya kiafya)wakifariki na ushahidi wa kimazingira wa hali hii ni kipindi ambao vifo huwa vingi kuliko kawaida tena vikionekana ni vifo vya ghafla kwa walio wengi.

Nini hutokea baada ya hapo(herd community kuwa developed)?

Kwakuwa kinga hii huwa si ya Kudumu, basi kuna wakati kinga hii huisha ila virusi vinakosa mazingira ya kuviwezesha kuendelea kutushambulia mpaka kipindi fulani cha mwaka(probably January to March) kijirudie ndio hali ya hewa huwa conducive kwa virusi hawa kutushambila na ndio maana kwa miaka hii miwili ya 2020 na 2021 milipuko na ongezeko la vifo vilijitokeza katika kipindi hicho kwa hii miaka miwili mfululizo.

Tusubiri tena kuanzia mwezi January mpaka mwezi March mwakani(2022) ili tuweze kujiridhisha na wakati huo huo tuombe kirusi kitachokuwa kimejibadilisha na kusubiri conducive environment kisiwe hatari kulik virusi vilivyopita.

Kwahiyo ni imani yangu si maombi,nyungu, malimao wala tangawizi vinavyotusaidia, badala yake ni herd community na hali ya hewa(mazingira) ndio vinavyotusaidia.

Ni mtazamo wangu ingawa naamini utafiti unahitajika kupata ukweli na mambo mengine kuhusu hili gonjwa hapa nchini na mwenendo wake.

mm pia sio daktari ila nna rafiki ambae ni daktari india, ivi ndivo alivoniambia!
- kwanza kabisa covid hua ni code ya information kuhusu huyo virus, so wenyewe hua wanamchukua huyo virus na kusoma code zake then wanatengeneza dawa kupitia same same code, lakini ata the same time binadam tuna kitu kinaitwa (WBC) hizi pia kulingana na mwili wako hua znachukua code ya huyo virus na kusambaza kwenye wbc cells mwili mzima next time akija tena corona(SARS-V) hua tayar information yake inakua saved so it becomes harmless
 
Kwamba unadhani mwanadamu anayeitwa Mtanzania aliyepo Tanzania ana utofauti gani na mwanadamu mwingine aliyepo nchini kwake?

Watu wameumwa na wapo wengine wanaumwa, utofauti ni kwamba upashaji wa habari za hao wauguao au waendao katika wafu haufanywi kama kwenye mataifa mengine...

Ingalikuwa takwimu zinawekwa wazi, kila mtu pengine angelikuwa kwenye 'panic mode', na mitaani ungelikuwa wapishana na watu wenye kuchukua tahadhari zaidi...

Hata hivyo hili uliloliweka bayana nalo huenda lipo, by the way it's herd immunity and not 'community'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli Herd Immunity inasaidia sana kwa watu walio wengi hasa maskini, kwa kuwa ndio walio wengi wanaotumia nguvu nyingi kujitafutia kipato.
Herd Immunity ya namna hiyo ni ile ya asilia inayoongezewa na nguvu kazi mahala pa kazi.
Ugumu wa maisha na hali ya kumuomba Mwenyezi Mungu atupatie ridhiki zetu ndimo palipo na kinga kuimalisha zaidi Herd Immunity.
 
mm pia sio daktari ila nna rafiki ambae ni daktari india, ivi ndivo alivoniambia!
- kwanza kabisa covid hua ni code ya information kuhusu huyo virus, so wenyewe hua wanamchukua huyo virus na kusoma code zake then wanatengeneza dawa kupitia same same code, lakini ata the same time binadam tuna kitu kinaitwa (WBC) hizi pia kulingana na mwili wako hua znachukua code ya huyo virus na kusambaza kwenye wbc cells mwili mzima next time akija tena corona(SARS-V) hua tayar information yake inakua saved so it becomes harmless
Sio dawa..ni chanjo ndo inatengezwa hivyo.
 
Umefanya research gani au umetumia kigezo gani kugundua kuwa Tanzania Corona haipo kwa kiwango kikubwa?
Naposema herd immunity,maana yake ni asilimia 80 ya watu wawe wameugua au wamepata maambukizi pasipo kuonyesha dalili lakini waka-develop kinga. Kwahiyo, kitendo cha kuongelea tu herd immunity, maana yake ugonjwa umefikia aailimia 80 ya watu katika jamii yetu.
 
Back
Top Bottom