Sababu ya Nne: CAG kakosea kutamka Bunge ni dhaifu jumla jumla. Yaani kusema Bunge ni dhaifu bila kusema katika lipi? Hivi ni kweli kwamba mambo yooote yanayo ainishwa na CAG bunge halifanyii kazi? Kama ni hivyo ingewezekana vipi hati chafu zikapungua. Mbona mambo mengi sana yaliyoibuliwa na CAG yanajadiliwa Bungeni na kufanyiwa kazi. Sasa kutamka kauli isiyo na maelezo kama hii hakika ina tatiza. Unapolenga kumkosoa mtu inafaa kumwambia umekosea katika lipi na kama ni udhaifu wa bunge ni katika lipi? Je kutunga sheria? Kushauri serikali? Kusimamia serikali? Au katika lipi?
Kwa maoni yangu haya ndio makosa ya CAG katika hili.
Mkuu Mupirocin, kwanza asante kwa maelezo marefu ya kina, unachambua vizuri, ila nina ushauri mdogo kwako.
Next time ukisikia mtu anashutumiwa ametamka kitu fulani, usiishie kusilikiza watuhumu, bali tafuta na aliyetamka usikie hicho kilichotamkwa ujiridhishe ndipo utoe maoni.
1. Jee ulimsikiliza CAG?.
2. Ulisikia akitamka "Bunge Dhaifu"
3. Ulisikia hakusema ni Dhaifu wapi?.
Ukisikiliza upande mmoja kama upande huo ni upande wa vichwa maji na wewe utakuwa kichwa maji. Kama ni upande wa viazi, na wewe utakuwa kiazi.
Kwa kukusaidia tuu
1. CAG hajasema popote "Bunge Dhaifu"
2. Amesema "Bunge Limeinyesha Udhaifu"
3. Na Akataja maeneo yenye udhaifu.
Mtu ambae hajui tofauti ya "Dhaifu" na "Udhaifu" ni kiazi.
Haya hata mimi yakiwahi kunikuta na niliitwa huko huko Dodoma kuhojiwa.
Niliuliza humu "Jee Bunge Linajipendekeza Kwa Serikali?.
Mbunge mmoja kiazi akasimama na kusema nimelidhalilisha Bunge kwa kuliita "Linajipendekeza Kwa Serikali"
Take time kamsikilize CAG alisema nini, usiwategemee Sana watuhumu wengine ni viazi.
Wanabodi, Wakati tukiendelea kuisubiria hiyo tarehe 21/1/19 ifike, hakuna ubaya kama Watanzania tutaelimishana kidogo ni nini haswa CAG alichokisema kuhusu Bunge letu wakati akiwa nchini Marekani hadi watu kuhamaki, kukasirika, hadi kupandisha jazba na kuanza kuitana kwa kutishina kwa pingu...
P