Inawezakana CDF na IGP wakapiga salute kwa mkuu wa Wilaya?

Na CDF Mabeyo kumpigia saluti Jokate unasemaje hapo?
Screenshot_20220608-161500.jpg
 

Mleta Thread Tulia Hapa Hapa Ila Kwa Taratibu Za Jeshi Hakuna Tatizo Lolote

Walilolifanya Hao Makamanda Wote Kwa Kutoa Salutation Kwa DC

 
Usi sahau dc ni mwakilishii wa Raisi ngazi ya wilaya .nacho taka kusema ni 1×1=1
 
mtoa mada mimi nafikiri kitu kama hukijui ni heri ukae kimya kuliko kujionesha hadharani jinsi ulivyo na akili fupi
 
Hakuna alichokosea hapo IGP ndivyo inavyotakiwa.

Jokate ni Mkuu wa Wilaya hivyo basi ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya husika na IGP yupo ndani ya kamati ya Usalama kwa hiyo kiprotokali IGP anatakiwa ampigie salute Mkuu wake
Blah blah blah blah, kweli kuna mtu alitugeuza watanzania wengi kuwa mazuzu, binafsi sio zuzu kabisa, ndio tatizo la kuvifanya vyombo hivi vya ulinzi na usalama ambavyo vilitakiwa kuwa neutral vimemezwa na politicians!
 
DC anateuliwa na Rais aongoze wilaya.. CDF anateuliwa na Rais anaongoza majeshi yote ya Tanzania lakini mtu bado anakwambia sababu DC kateuliwa na rais haiingi akilini kiprotocol labda kama msmee Mabeyo hana namna nyingine ya kutoa salamu zaidi ya SALUTE ukizingatia kavaa full combat.
 
DC anateuliwa na Rais aongoze wilaya.. CDF anateuliwa na Rais anaongoza majeshi yote ya Tanzania lakini mtu bado anakwambia sababu DC kateuliwa na rais haiingi akilini kiprotocol labda kama msmee Mabeyo hana namna nyingine ya kutoa salamu zaidi ya SALUTE ukizingatia kavaa full combat.
Pata picha mkuu wa wilaya ana cheo cha kapteni au meja wa jeshi hilo
 
Wananzengo wanadai 'PGO' haimruhusu IGP kumpigia saluti DC. Askari anayetakiwa kumpigia saluti DC ni yule mwenye cheo cha Mkaguzi (Inspector) – mwenye nyota mbili, na askari wote wa vyeo vya chini yake.

Kwa lugha rahisi hapa ni sawa na mtoto kusalimiwa na Baba yakeView attachment 2254370

Mambo ya kijeshi huyajui agiza mbege uendelee kumwagilia moyo.
 
Saluti ni salamu kama zingine.
Ni salamu kwa watu walioenda jando.

Husalimiwa kwa askari mdogo kusalute kwa aliyemzidi cheo au aliye senior.

Yaani NCO husalimia kwa salute mbele ya mkubwa waoa au mtu aliyeteuliwa na raisi.

Commissioned officer/ gazetted officers au askari mwenye Cheo kuanzia nyota moja husalimia kwa salute mtu aliyemzidi Cheo au most senior.

Kiprotokali Mimi naona haikukaa sawa kwa nafasi kama CDF, IGP, CGI,CGP,CGF Kutoa salute kwa mkuu wa wilaya iwe Kijeshi au kiraia.

Kwa nini?

Mkuu wa wilaya anawakilisha Mamlaka ndogo katika utawala wa nchi kisiasa.

Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ngazi ya wilaya au hata ingekuwa mkoa Bado.

Ila CDF anawakilisha Mamlaka makubwa ya kiulinzi katika Taifa yaani ni mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kitaifa kwa ujumla.

Ni mkubwa kimamlaka kuliko DC, halafu wote mteuzi ni mmoja.

IGP na Mamlaka yake ni mtu mkubwa kiusalama kwa Taifa Zima kuliko DC.

CGI ni mtu mkubwa kimamlaka kuliko DC

Hivyo protokali haikufuatwa kwa mtu anayeangalia maslahi mapana ya ulinzi na usalama kitaifa kuwa mdogo kuliko mtu anayedili na wilaya tu.

Ila kilikuwa kipindi Cha jiwe
 
Back
Top Bottom