kande kavu
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 234
- 89
Tena Sana! (Endelea kusoma na tafadhali toa ushauri kama unao).
Aisee binadamu tuna mitihani.Ni hivi, baada ya kuona utendaji wa dada mmoja hivi hapa kibaruani unashuka (ikiwemo ukali wa ghafla, kuropoka na kupendelea kukaa kipekee),nikataka kujua kulikoni kabla ya kukurupuka na kutoa kadi ya njano.Baada ya mazungumzo marefu, dada alifunguka kama ifuatavyo:
"Nina watoto wawili, mkubwa wa kiume ana miaka sita. Ninawalea peke yangu sina mme. Huyu wa kiume alienda kuishi kwa mama yake mdogo mpaka alipofikisha umri wa miaka minne mkoa fulani.Miaka miwili iliyopita nilienda kumchukua ili niishi nae.Kipindi kifupi baada ya kuanza kuishi nae,nikaanza kupata ndoto mbaya kwamba mwanangu anaingiliwa kinyume na maumbile.Ndoto ziliendelea kwa muda mpaka nikashawishika kumkagua mtoto sehemu zake za siri.Nilichoona,ni uharibifu mkubwa wa sehemu zake(vidonda,fangasi) nilizimia.Kwa hasira na vipigo nilimhoji mtoto na akanambia huwa anafanya na wavulana na wanaume.Ama wanamtongoza yeye au wakati mwingine anawatongoza yeye na kwamba alianza huo mchezo akiwa mkoani akiwa bado mdogo kama miaka mitatu hivi".
Huyu dada amekwisha kuchukua hatua zifuatazo:
Maendeleo ya mtoto:
Asanteni.

- Amehamia nje kabisa ya jiji kwenda kule alikozani mwanaye hatapata watu wa kumwingilia kwani mtaa aliokuwa akiishi awali mwanaye alikuwa asusa hasa dada anapokuwa kazini.
- Ametumia nguvu sana kupambana na tabia ya mwanae.(mtoto ana makovu mwili mzima kwa vipigo) NILIMWAMBIA HILI SIO SAHIHI.
- Amempeleka mtoto kufanyiwa maombi.
- Sasa anampeleka hospitali kwa matibabu ya kisaikolojia na mtoto kwa bahati hajaambukizwa magonjwa.
Maendeleo ya mtoto:
- Bado alipohamia nje ya mji mtoto aliendelea kwa muda kuingiliwa/ama bado anaingiliwa.
- Mama yake kila akitoka kazini anamkagua lakini bado kunaashiria kuna kitu kinaendelea na dogo anajitetea kuwa ameacha kuingiliwa ila anajikwangua na vidole.NIMEMWAMBIA KWAMBA MTOTO HAWEZI KUACHA GHAFLA TABIA HIYO NA KAMA NI KWELI MICHUBUKO NI YA VIDOLE VYAKE, BASI HUENDA MTOTO AMEANZA MUITIKIO WA MATIBABU HIVYO AANZE AU AENDELEE KUMWONYESHA UPENDO NA KUENDELEA NA MATIBABU.
- Alitakiwa ampeleke mtoto hospitali kama mara tatu kwa mwezi lakini akaomba ampeleke mara moja kwa mwezi kwa kile alichodai kubanwa kazini.NIMEMSHAURI ACHUKUE LIKIZO YAKE YA KAWAIDA NA YA MIEZI MIWILI BILA MALIPO ILI AKAZANIE MATIBABU YA MWANAE.
Asanteni.