Inasikitisha

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,232
754
Jana nikiangalia habari saa 2 usiku kituo cha ITV, kuna habari ilinisikitisha sana,Imekuwa ni kawaida ya kuona wagonjwa wa akili wakila majalalani.

Lakini huko Dodoma watu wenye utimamu wa akili wakila jalalani na familia zao, mama mmoja akionekana akila na mtoto wake umri kama mwaka mmoja na nusu hivi vyakula vilivyotupwa jalalani.

Hivi hii serikali yetu ipo wapi? Watu wanahali mbaya kiasi hichi wananyang'anyana vyakula na mbwa jalalani. Huu ni wakati wakuchukua maamuzi magumu na si usanii kila kukicha.
 
Lahaullah!
Ndio baa la njaa limeanza, bado halijashika kasi. Sijui likishika kasi ITAKUWAJE, kilimo kwanza...
 
nami niliona hiyo habari mkuu na nilikuwa nawaza kuileta hapa jamvini kupata mawazo. Cha kusikitisha zaidi ni kuona wale watu wamechukulia hiyo hali tayari kama sehemu ya utamaduni.
Lakini pia mita si nyingi kutoka pale ndipo mstakabali wa taifa hili unajadiliwa na kuamuliwa na picha iliyo wazi ni jinsi gani pengo kati ya 'wenyenacho' na 'wasionacho' limepanuka, uhitaji ushahidi zaidi.
...Tumeimba "Mungu ibariki Tanzania" kwa miaka 50 sasa!!!!
 
Hiyo ndiyo kauli ya chama cha magamba "ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA" na Kilimo kwanza. 2tashanga.
 
Hizo ndio Athari za ccm baada ya 50yrs tunaziona na bado tutaendelea kuziona nchi haina Umeme wa uhakia, Maji safi hakuna, Hospital hazina dawa, Viongozi waadilifu hatuna ila tuna Majambazi kama Kikwete na genge lake, Sheria zipo hazifuatwi, Ardhi wanauziwa Wageni, Ajira ndio usiseme wageni kwanza mwenyeji Baadaye na Njaa inanyemelea isjui tutatokea waoi.

Mungu tunusuru na haya Mabalaa tunayosukumiwa na Genge la Majambazi na iangamize CCM kama ulivyoliangamiza Jeshi la Firauni
 
Wakati wewe ukinungunika - sisi tunasakata rumba - Matayarisho ya miaka 50 ya uhuru wako - hujui nchi hii imetoka wapi - ni vyema kukaa kimya - teh teh teh

kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake - Serikali haiwezi kukufanyia kila jambo pamoja na kumnunulia mwanao maziwa.

CCM oyeeeee.......... TANU oyeeeeee ........ Makamba oyeeeeee........... oops sorry Nape oyeeeee.......

2.JPG
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom