Viongozi wetu na ngonjera za umeme

Viongozi wetu na ngonjera za umeme

Bigmaaan

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2023
Posts
469
Reaction score
1,084
Mwaka 2013 ama na 14, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Maselle, alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya chakula cha usiku na Vijana wa vyuoni pale Mwanza, nilipata nafasi ya kuwepo kama 'Mzamiaji'.

Maselle alipata wasaa wa kuzungumza, moja ya jambo alilizungumzia ni kero ya umeme. Nakumbuka na kunukuu maneno yake;

"TANESCO iliwekwa kwenye orodha ya mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa enzi za Mkapa ndio maana hakuna uwekezaji uliofanyika wa kutosha kwenye uzalishaji umeme" akaendelea na kuuliza, "ingekua ndio wewe unataka kuiuza nyumba yako, utawekeza kuijenga zaidi?"Makofi hayakua haba.

Leo, miaka 10 imepita. Zaidi ya Miaka 25 ya masuala ya ubinafsishaji, bado umeme ni changamoto.

Hakika viongozi wetu hawajawahi pungukiwa maneno juu ya uhaba wa umeme.
 
Hatuna viongozi tuna majangili tupu
 
Back
Top Bottom