Kwani Mkuu wewe wapinzani unawachukuliaje?Nimesikitishwa sana na kitendo cha Naibu Waziri mmoja wa Marekani kupewa muda wa kukutana na vyama vya siasa Tanzania.
Nimejiuliza mara nyingi sana kichwani kuwa je, Katambi anaweza kwenda USA akapewa muda wa kukutana na Biden na akaomba kukutana na chama cha REPUBLICAN wakampa mawazo yao jinsi wanavyoendesha siasa zao kule?
Je, USA wanaweza wakaenda CUBA pale Havana wakaomba kuongea na umma hasa hasa wenye mrengo tofauti wa kisiasa na wakapewa huo muda?
Kwanini tunashindwa kujiongoza kama taifa mpaka mataifa mengine yatufundishe cha kufanya wakati gani, namna gani, dhidi ya nani.
Kweli tumesoma vizuri na kuelemika kwa kiwango cha kujielewa na kijitawala wenyewe?
Serikali inaweza kuwa inafanya vibaya kwa baadhi ya mambo lakini je lazima USA ije na kuturekebisha na kutuonyesha cha kufanya?
Je, huu ndio UKOLONI MAMBOLEO?
Bora hata huyo mchungaji unaweza kumchukulia kwamba ana neno la kiroho la kuweza kuonya na kushauri. Sasa Naibu Waziri anapewa mpaka nafasi ya kuonana na Mkuu wa Nchi.??Ukijua jinsi dunia inavyoenda hutashangaa hilo suala la mkubwa kumuonya mdogo ,
Hata nyumbani kwetu mchungaji anakuja kukushauri wew na familia yako kuhusu maisha na wote mnakaa kumsikiliza ila wew ukienda kwa mchungaji unaweza ishia onana na houseboy au mkata majani tu
Ni kawaida tu kaka wala usipanic
Ni jibu zuri uliloweka hapa mkuu 'Fundi', ukiliangalia katika kona uliyoamua kuitumia, lakini bado kutakuwepo na kona kadhaa zinazoweza kuwa tofauti na mtizamo huu.Kwa taarifa yako, hamna kiongozi anayezuiwa kuongea na kikundi chochote akitembelea Marekani. Netanyau aliwahutubia Republicans wakati wa Obama. Sharti moja la kurudisha uhusiano na Cuba ilikuwa ni lazima waweze kukutana na wapinzani na wafungwa wa kisiasa na walikubaliwa.
Katika jamii ya dunia uhuru wa kuongelea masuala yanayoendelea katika nchi nyingine ni sacrosant ili kuweza kuepusha yaliyotokea Rwanda na mengine. Ukiona unaonewa unajibu kwa kuwaeleza wamekukosea wapi na sio kujinyima nyuma ya pazia la sovereignty.
Amandla...
Kisichowezekana kwako kwa wengine kinawezekana. Nilikuwa nasoma UK na kukatokea uchaguzi wa meya wa sehemu tuliyokuwa tukiishi (Totteridge Common, London Borough of Barnet) na sisi tuliokuwa tunatoka nchi za Jumuiya ya Madola tuliambiwa tuko eligible kupiga kura na tulienda kupiga kura. Ukiacha Tanzania na UK, sijawahi kupiga kura sehemu zingine zozote ingawa nimekaa pia Zambia (mwaka mmoja) na Malawi (miaka 7). So, somethings are possible.Nimesikitishwa sana na kitendo cha Naibu Waziri mmoja wa Marekani kupewa muda wa kukutana na vyama vya siasa Tanzania.
Nimejiuliza mara nyingi sana kichwani kuwa je, Katambi anaweza kwenda USA akapewa muda wa kukutana na Biden na akaomba kukutana na chama cha REPUBLICAN wakampa mawazo yao jinsi wanavyoendesha siasa zao kule?
Je, USA wanaweza wakaenda CUBA pale Havana wakaomba kuongea na umma hasa hasa wenye mrengo tofauti wa kisiasa na wakapewa huo muda?
Kwanini tunashindwa kujiongoza kama taifa mpaka mataifa mengine yatufundishe cha kufanya wakati gani, namna gani, dhidi ya nani.
Kweli tumesoma vizuri na kuelemika kwa kiwango cha kujielewa na kijitawala wenyewe?
Serikali inaweza kuwa inafanya vibaya kwa baadhi ya mambo lakini je lazima USA ije na kuturekebisha na kutuonyesha cha kufanya?
Je, huu ndio UKOLONI MAMBOLEO?
Ni jibu zuri uliloweka hapa mkuu 'Fundi', ukiliangalia katika kona uliyoamua kuitumia, lakini bado kutakuwepo na kona kadhaa zinazoweza kuwa tofauti na mtizamo huu.
Umetoa mfano wa Netanyahu wa Israel, bila shaka bila ya kuchukulia maanani hadhi ya taifa hilo katika nchi aliyokuwa akiitembelea na kufanya alivyofanya.
Kwa kutumia mfano huo huo ulioutumia hapo na kuugeuza umwelekee mmoja wa akina Castro wawili wakitembelea Marekani ili na wao wawe na fursa kama aliyokuwa nayo Netanyahu, bila shaka utafikia hitimisho tofauti na hilo ulilofikia hapo kwenye bandiko lako.