Inasikitisha Naibu Waziri Marekani kukutana na Vyama vya Siasa Tanzania

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
696
1,000
Nimesikitishwa sana na kitendo cha Naibu Waziri mmoja wa Marekani kupewa muda wa kukutana na vyama vya siasa Tanzania.

Nimejiuliza mara nyingi sana kichwani kuwa je, Katambi anaweza kwenda USA akapewa muda wa kukutana na Biden na akaomba kukutana na chama cha REPUBLICAN wakampa mawazo yao jinsi wanavyoendesha siasa zao kule?

Je, USA wanaweza wakaenda CUBA pale Havana wakaomba kuongea na umma hasa hasa wenye mrengo tofauti wa kisiasa na wakapewa huo muda?

Kwanini tunashindwa kujiongoza kama taifa mpaka mataifa mengine yatufundishe cha kufanya wakati gani, namna gani, dhidi ya nani.
Kweli tumesoma vizuri na kuelemika kwa kiwango cha kujielewa na kijitawala wenyewe?

Serikali inaweza kuwa inafanya vibaya kwa baadhi ya mambo lakini je lazima USA ije na kuturekebisha na kutuonyesha cha kufanya?

Je, huu ndio UKOLONI MAMBOLEO?
 
Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
995
1,000
Ukijua jinsi dunia inavyoenda hutashangaa hilo suala la mkubwa kumuonya mdogo ,

Hata nyumbani kwetu mchungaji anakuja kukushauri wew na familia yako kuhusu maisha na wote mnakaa kumsikiliza ila wew ukienda kwa mchungaji unaweza ishia onana na houseboy au mkata majani tu

Ni kawaida tu kaka wala usipanic
 
edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
6,536
2,000
Waafrika sisi tumeamua kujigeuza malaya wa kisaisa chama tawala na wapinzani aote ni washamba wa watu wageni
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
7,237
2,000
Kwa taarifa yako, hamna kiongozi anayezuiwa kuongea na kikundi chochote akitembelea Marekani. Netanyau aliwahutubia Republicans wakati wa Obama. Sharti moja la kurudisha uhusiano na Cuba ilikuwa ni lazima waweze kukutana na wapinzani na wafungwa wa kisiasa na walikubaliwa.

Katika jamii ya dunia uhuru wa kuongelea masuala yanayoendelea katika nchi nyingine ni sacrosant ili kuweza kuepusha yaliyotokea Rwanda na mengine. Ukiona unaonewa unajibu kwa kuwaeleza wamekukosea wapi na sio kujificha nyuma ya pazia la sovereignty.

Amandla...
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,901
2,000
Mkuu 'MKEHA',

Nadhani naelewa mada yako inakoegemea, na kama dhana yangu ni sahihi huenda nikapingana nawe juu ya hili.

Ila ninakubaliana nawe kiujumla.

Na maana ya kukubaliana na wewe ni kuhusu nchi yetu ilivyoporomoka kihadhi; kwamba hakuna tena ule msimamo thabiti tuliokuwa tunajuwa unatupeleka wapi kama nchi iliyo huru.

Hawa viongozi wetu waliopo sasa, lengo lao pekee linalowasukuma ni kuendelea kuwa na madaraka ya kuendesha nchi, kwa hiyo watafanya chochote kitakachowapa nafuu ya kuwa na uhakika huo.
Wanaporuhusu kama walivyofanya hapo, ni kwa wao wajionyeshe kwa hao wanaotafuta fadhira kwao kwamba wao ni viongozi wanaotimiza matakwa ya wananchi, ikiwemo na uhuru wa kukutana na viongozi wa kisiasa kukutana na wageni hao, hata kama huko ni kuhadaa tu dunia.

Nigusie tu nisipokubaliana na wewe, kama dhana yangu ipo sahihi. Nakuona kama ni mmoja wa hao walioko ndani ya hicho chama kandamizi, kwa hiyo unalalamikia kitendo cha chama chako kuruhusu jambo kama hilo, hata kama kwa kutojua kwako kwamba viongozi wako wanafanya hivyo kwa maslahi yenu watawala mlioamua kwa maksudi mazima kutuweka sisi wengine wote kuwa mateka wenu kwa kutumia vyombo vyetu vya kutudindia usalama wetu.
Kama nimekosea, kuniradhi.
 
Choo Cha Kulipia

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
959
1,000
Nimesikitishwa sana na kitendo cha Naibu Waziri mmoja wa Marekani kupewa muda wa kukutana na vyama vya siasa Tanzania.

Nimejiuliza mara nyingi sana kichwani kuwa je, Katambi anaweza kwenda USA akapewa muda wa kukutana na Biden na akaomba kukutana na chama cha REPUBLICAN wakampa mawazo yao jinsi wanavyoendesha siasa zao kule?

Je, USA wanaweza wakaenda CUBA pale Havana wakaomba kuongea na umma hasa hasa wenye mrengo tofauti wa kisiasa na wakapewa huo muda?

Kwanini tunashindwa kujiongoza kama taifa mpaka mataifa mengine yatufundishe cha kufanya wakati gani, namna gani, dhidi ya nani.
Kweli tumesoma vizuri na kuelemika kwa kiwango cha kujielewa na kijitawala wenyewe?

Serikali inaweza kuwa inafanya vibaya kwa baadhi ya mambo lakini je lazima USA ije na kuturekebisha na kutuonyesha cha kufanya?

Je, huu ndio UKOLONI MAMBOLEO?
Kwani Mkuu wewe wapinzani unawachukuliaje?
Ajenda je za kikao kati ya Waziri husika na Vyama zilikuwa ni zipi?
Dah..kwa mawazo hayo yako Mkuu basi kazi ipo..
 
kipande

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
2,080
2,000
Ukijua jinsi dunia inavyoenda hutashangaa hilo suala la mkubwa kumuonya mdogo ,

Hata nyumbani kwetu mchungaji anakuja kukushauri wew na familia yako kuhusu maisha na wote mnakaa kumsikiliza ila wew ukienda kwa mchungaji unaweza ishia onana na houseboy au mkata majani tu

Ni kawaida tu kaka wala usipanic
Bora hata huyo mchungaji unaweza kumchukulia kwamba ana neno la kiroho la kuweza kuonya na kushauri. Sasa Naibu Waziri anapewa mpaka nafasi ya kuonana na Mkuu wa Nchi.??

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,901
2,000
Kwa taarifa yako, hamna kiongozi anayezuiwa kuongea na kikundi chochote akitembelea Marekani. Netanyau aliwahutubia Republicans wakati wa Obama. Sharti moja la kurudisha uhusiano na Cuba ilikuwa ni lazima waweze kukutana na wapinzani na wafungwa wa kisiasa na walikubaliwa.

Katika jamii ya dunia uhuru wa kuongelea masuala yanayoendelea katika nchi nyingine ni sacrosant ili kuweza kuepusha yaliyotokea Rwanda na mengine. Ukiona unaonewa unajibu kwa kuwaeleza wamekukosea wapi na sio kujinyima nyuma ya pazia la sovereignty.

Amandla...
Ni jibu zuri uliloweka hapa mkuu 'Fundi', ukiliangalia katika kona uliyoamua kuitumia, lakini bado kutakuwepo na kona kadhaa zinazoweza kuwa tofauti na mtizamo huu.
Umetoa mfano wa Netanyahu wa Israel, bila shaka bila ya kuchukulia maanani hadhi ya taifa hilo katika nchi aliyokuwa akiitembelea na kufanya alivyofanya.
Kwa kutumia mfano huo huo ulioutumia hapo na kuugeuza umwelekee mmoja wa akina Castro wawili wakitembelea Marekani ili na wao wawe na fursa kama aliyokuwa nayo Netanyahu, bila shaka utafikia hitimisho tofauti na hilo ulilofikia hapo kwenye bandiko lako.
 
Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,132
2,000
Nimesikitishwa sana na kitendo cha Naibu Waziri mmoja wa Marekani kupewa muda wa kukutana na vyama vya siasa Tanzania.

Nimejiuliza mara nyingi sana kichwani kuwa je, Katambi anaweza kwenda USA akapewa muda wa kukutana na Biden na akaomba kukutana na chama cha REPUBLICAN wakampa mawazo yao jinsi wanavyoendesha siasa zao kule?

Je, USA wanaweza wakaenda CUBA pale Havana wakaomba kuongea na umma hasa hasa wenye mrengo tofauti wa kisiasa na wakapewa huo muda?

Kwanini tunashindwa kujiongoza kama taifa mpaka mataifa mengine yatufundishe cha kufanya wakati gani, namna gani, dhidi ya nani.
Kweli tumesoma vizuri na kuelemika kwa kiwango cha kujielewa na kijitawala wenyewe?

Serikali inaweza kuwa inafanya vibaya kwa baadhi ya mambo lakini je lazima USA ije na kuturekebisha na kutuonyesha cha kufanya?

Je, huu ndio UKOLONI MAMBOLEO?
Kisichowezekana kwako kwa wengine kinawezekana. Nilikuwa nasoma UK na kukatokea uchaguzi wa meya wa sehemu tuliyokuwa tukiishi (Totteridge Common, London Borough of Barnet) na sisi tuliokuwa tunatoka nchi za Jumuiya ya Madola tuliambiwa tuko eligible kupiga kura na tulienda kupiga kura. Ukiacha Tanzania na UK, sijawahi kupiga kura sehemu zingine zozote ingawa nimekaa pia Zambia (mwaka mmoja) na Malawi (miaka 7). So, somethings are possible.
 
Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
935
1,000
Kuna sehemu humu JF nilisoma maoni ya watu. Watu wamekuwa na Shaka sana na HII LIST YA WAPINZANI ILIYOKUTANA NA HUYU UNDERSECRETARY.

Nadhani mmenielewa
 
gimanini

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
1,561
2,000
Chanjo ya Corona akupe Marekani,misaada mwingine umlilie akupe Tena bure alaf ikifika pointi asije kukuona kwako.mtoa mada ata mawazo ya sizitaki mbichi hizi.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
7,237
2,000
Ni jibu zuri uliloweka hapa mkuu 'Fundi', ukiliangalia katika kona uliyoamua kuitumia, lakini bado kutakuwepo na kona kadhaa zinazoweza kuwa tofauti na mtizamo huu.
Umetoa mfano wa Netanyahu wa Israel, bila shaka bila ya kuchukulia maanani hadhi ya taifa hilo katika nchi aliyokuwa akiitembelea na kufanya alivyofanya.
Kwa kutumia mfano huo huo ulioutumia hapo na kuugeuza umwelekee mmoja wa akina Castro wawili wakitembelea Marekani ili na wao wawe na fursa kama aliyokuwa nayo Netanyahu, bila shaka utafikia hitimisho tofauti na hilo ulilofikia hapo kwenye bandiko lako.

Mfano wako wa Cuba kwa hapa haufai. Haufai kwa sababu chama cha upinzani Marekani ni maadui wakubwa wa Cuba na hivyo hawatakubali kuonekana nao chumba kimoja. Wakifanya hivyo watapoteza kura nyingi za wakimbizi kutoka Cuba wanaoishi Florida na hivyo wanaweza kupoteza electoral votes za jimbo hilo. Na wakati wa Trump, ndio kabisa. Suala la Marekani sio viongozi hao kuruhusiwa kukutana na wapinzani bali utayari wa wapinzani hao kukutana nao. Kwa mfano, ni vigumu sana kwa kiongozi wa wapalestina kukutana na chama chochote Marekani kwa sababu wote wanaogopa nguvu za raia zao wenye asili ya kiyahudi. Hata Netanyahu alivyofanya aliyofanya, alilaumia sana kwa kutomheshimu Obama lakini lawama kubwa zilielekezwa kwa Republicans kwa kumkaribisha kuwahutubia. Lakini hamna aliyepinga haki yake ya kukutana nao. Kilicholalamikiwa ni optics za kufanya hivyo.

Amandla...
 
  • Thanks
Reactions: Qwy

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom