Inaniuma sana: Juma Nature Kwanini usiache kama huwezi?

Inaniuma sana: Juma Nature Kwanini usiache kama huwezi?

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,092
Naomba nitumie lugha kali kumkemea huyu Msanii mkongwe wa muziki wa B. Flava nchini, Juma Cassim Nature, maana naona wasanii wanazidi kutudharau na kutunyanyasa kwa sababu ya ubinafsi wao, shenzy kabisa!

Mwanamuziki/Msanii yeyote ni kama nabii, ni kama mteule au mpakwa mafuta kwa sababu moja kuu; Ana ufuasi mkubwa sana unaomfuatilia.

Sasa mtu wa aina hii, ni lazima ajue anabeba hisia, matarajio na mioyo ya watu wengi. Kwahiyo anapaswa kujua kwamba anabeba maumivu, furaha, hasira, na faraja za watu wengi sana. Hana budi kuheshimu hilo na kuwa makini kwa kila akifanyacho; hususani kwenye kile kilichompa wafuasi wengi..

Kufanya kazi nzuri, sio hiari, ni lazima. Kwa sababu hufanyi kwa ajili yako tu, bali kwa ajili ya wanaonunua kazi yako. Ni dharau ya hali ya juu kufanya kile unachojisikia kwa vile tu unapendwa!

To cut the story short, Juma Nature ame-release RMX ya wimbo wake wa kihistoria, wimbo uliobeba kumbukumbu za maisha ya miaka ya nyuma ya watanzania wengi, wimbo unaowakumbusha watu mambo flani flani kwenye maisha kila wausikiapo. Wimbo wenye heshima na unaokumbukwa zaidi kwa muda mrefu sasa. INANIUMA SANA!

INANIUMA SANA ni wimbo wenye 'emotional value', ambayo pengine Nature ameamua kuichezea na kuipuuza. Ameifanyia Remix kwa mtindo wa 'kigodoro' kwa kumshirikisha Msaga Sumu, mtindo wa kisasa, mtindo ambao unaendana na nyakati zilizopo, Old wine in a new bottle..

Si dhambi, lakini je kuna haja ya kufanya hivyo?

Alichokifanya ni 'Value Assassination' ya huu wimbo bila kujua. Ni nani aliyemshauri hata kuthubutu kufanya hivi? Ni nini kimemsukuma kufanya huu ujinga? Watu wengine sijui wakoje!!!

Anatafuta namna ya kurudi? Kwani kwenye muziki hakuna kustaafu? Hivi hakuna namna ya kumfanya msanii akapumzika kutumikia kufanya alichokifanya kwa muda mrefu ili asiharibu reputation yake? Ninachoamini, Utendaji huenda na umri, zama na shauku ya mtendaji. Vikipita hivyo, ni kuboronga tu ndio kunakofuatia..

Kwa hili, Nachelea kusema Nature umedharau sana watu wengi, zaidi umedharau 'thamani' ya kazi yako! Ni bora ukatangaza kustaafu, ili tukuenzi kwa heshima.

Nimechukia kweli kweli!

attachment.php

OLD: View attachment Juma_Nature-Inaniuma_Sana.mp3
NEW: View attachment Juma_Nature-Inaniuma_Sana_RMX_Ft_Msaga_Sumu.mp3
 
Kila zama na mfalme wake,zama za akina Nature,Chenge,Temba,Prof J ,Jide, Blue,Nako 2 Nako, T.ID. zimeshapita,,Sasa hivi Diamond ndio habari ya mujini
 
Si amrudishe mganga wake aliyeibwa na Dayamondi maana zaidi ya hapo hakuna jinsi ya yeye kurudi top hata are-remix chachandu ya dhahabu
 
Jombaa njoo Dar Live tar 30,Kiroboto anatimiza miaka 16 kwenye game,njoo tufanye tasmini kwa pamoja!hapo ndo utapojua kiwango kipo au aanzie bench.
 
Unananikumbusha Jay Z alipoitwa nae ajumuike kwenye wimbo wa We are the World part two or unaweza ukasema remix pia. Aliwajibu that a classic song u cnt touch it.
Kuna nyimbo ambazo zinaheshima yake kubwa sana kwenye jamii si sawa kuzirudia. Na pia Joh Makini aliulizwa Xxl kama anaweza akarudia au remix ya wimbo wake wa Chochote popote poa alisema hivo hivo Kuna nyimbo nyingine inabidi zibaki kama zilivyokua.
 
Juma Nature ni kijana wa uswahilini kweli kweli, sishangai kuimba kigodoro
 
Unananikumbusha Jay Z alipoitwa nae ajumuike kwenye wimbo wa We are the World part two or unaweza ukasema remix pia. Aliwajibu that a classic song u cnt touch it.
Kuna nyimbo ambazo zinaheshima yake kubwa sana kwenye jamii si sawa kuzirudia. Na pia Joh Makini aliulizwa Xxl kama anaweza akarudia au remix ya wimbo wake wa Chochote popote poa alisema hivo hivo Kuna nyimbo nyingine inabidi zibaki kama zilivyokua.

Nakubaliana nawe Juma Nature amechemsha sana kufanya hiyo remix,ameshindwa kufikia hata nusu ya wimbo original.Nyimbo kama Hao,Tunasonga,Alikufa kwa ngoma,Bongo Darisalaam,Hili Game,Mtazamo,Zeze hazifai kurudiwa kabisa
 
Duh kama vipi vunga tu mpwa wewe jisogeze kwa Jux na wenzie uku uswazi tukimtoa mwali ndio vitu vyetu hivi kama haujui uku uswazi msaga Sumu ni zaidi ya Diamond na kifupi Kiroboto ni uswazi oriented kwake izi balaa ni za kawaida,karibu Dar Live uone huu mgoma ukipigwa nani atakaa chini na kuhusu kustaafu sahau labda akatike ulimi.
 
wee msaga sumu ndo kila kitu tena ukiweka mziki bila kupiga nyimbo zake hawakuelewi
 
Back
Top Bottom