Inaniuma saana

ERIK

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
623
314
Ni kama nina mkosi au ni kwamba wanawake wote ni waongo au ni hawa ninaokutana nao tu? haya ndo maswali nayojiuliza saana:

GF wangu wa kwanza:- nilikaa naye kwa muda wa miaka 3 nikajua ndo mke wangu na maisha tulishaanza yapanga,
sijui kama alikuwa anaigiza au alibadilika but alianza kuwa jeuri na kupotosha ahad, mwisho wa siku nilimpatia hela kama 2M akalipie kitu akaondoka nazo na kuniruka kuwa sijampa na kuniambia amenichoka na umasikini wangu namsingizia!!

baada ya maumivu na majonzi nikapata mwingine ambaye alifuta machozi kwa mapenzi ya kweli na kunihakikishia ni wangu milele!! sitaki kuamini kuwa baada ya mwaka na nusu, alianza kuingia kazini usiku gafla, mara kesho yake harudi et ameunganisha shift kufatilia officen kwao hakukuwa na shift ya usiku bt alikuwa analala gest au kwa wanaume!! pia alianza kuwa mlevi na dharau ki future sikumuhitaj tena ikabidi nimpotezee japo iliniuma saaana

ilinichukua muda nikawa sina girlfrnd pamanet nikawa nachukua wa hamu kwa hasira but ikatokea kupendana na girl
1 ambaye alikuwa anafanya kazi airpot na tulikuwa tuna kutana sana week end katika swiming pool,

nilikaa naye kama miaka 2, tulianza jenga maisha na mipango kunyooka, nilishamtambulisha kwa ndugu na jamaa pia!!
miezi mi 4 iliyopita alianza ku change kidogo, tulikuwa tupo huru kila mtu kupiga au kupokea simu ya mwenzi but mwenzangu akaanza kukataa, friends zangu wa karbu na watu waliokuwa wamemzunguka pia walianza kuniambie kuwa ana wanaume mara anakaa bar ovyo na kukutwa akitoka gest mara kwa mara!! nilikuwa namwamini sikuwasikia wala kuwaamini binadamu

siku ya Ijumaa ya Tarehe 30 mwezi huu sitaweza isahau kamwe, ilikuwa jioni nikiwa njian natoka officen alinipigia simu kuniambia kuwa anakuja kwangu nikamwabia is fine baada ya dk kama 35 nitakuwa nimefika!!

saa 1 mbele akanipigia kuwa atakuja mida ya saa 5 usiku coz anapitia kwa dada yake nikamwambi fine!!

saa 2 nilipigiwa simu na namba ngeni, ilikuwa sauti ya kiume iliyoniambia 'si unamwamini sana demu wako? njoo hapa (jina ba bar & gest) haraka

nikiwa kama sijaelewa hivi nikaamua kwenda, nikapga ile number jamaa akapokea akaniambia sitaki ujue mm nani naomba tu chat na fata maelekezo yangu, tuka chat mpaka akaniambie niende room ya jina la Morogoro theni nigonge au nishubiri hapo mpaka walio ndani watoke!!

nikampigia simu rafiki yangu akaja pale akashauri nigonge! kugonga sikuamini Mpenzi wangu alitota kunifungulia, nilihisi damu kusimama nikaondoka kwa hasira nikarudi home!!

mpaka muda huu na post hapa nashukuru mungu ni mzima nipo officen na bado napumua!! tangu ile juzi sijawasiliana naye naye pia yupo kimia!!

sitaki mnishauri nimsamehe but naomba mniambie kuna haja wa kumwamini tena msichana au nianje kuwachapa tu? au nikae kivyangu nipige hata nyeto maisha yaendeleee.....?
 
Pole sana ndugu yangu,sikushauri uwahukumu wanawake wote kwa makosa ya wachache..Wapo walio wa kweli na wenye mapenzi ya dhati..Naelewa unaumia,nakusihi upumzike kwa sasa kama mwaka hivi usiwe na mahusiano na mwanamke yoyote ikisha ujipange taratibu na kwa umakini ....Vumilia tu utampata poozeo la moyo wako inshallah....
 
Tatizo mnatafuta mademu wa swiming pool arafu mnataka wawe wake zenu we unaelekea una matatizo ya kuchagua.
Ni hivi broo hawa wasichana kuna brandy ya kuoa na brand ya kuchezea sasa wewe unataka kuoa wale wa kuchezea
 
kuna sehem ya kupreview post,ungefanya hivyo ingekua bora zaidi.........

I find it so hard to believe this story hasa the last part ya ufumanizi,kupigiwa sim

ila kama ni kweli pole yako,
 
thanks but kumbuka ni mara 3 na wana wake 3 tofauti!! sasa nikikaa tena hata miaka 2 na huyu wa 4 si ndo atakuwa zaidi jamani?
 
Kapime kama uko ok anza kuwafagia ukiwa umevaa uso wa nyani na kondom tatutatu
 
Tafuta innocent girls wanavaa magauni,na wanasali sana sasa wewe unaenda kwa hao wavaa vipedo,na kwenda kula bata swiming pool.POLE ZAKO Unatakiwa uwe na mke ambae ukimwambia twende kula bata swimming pool anajibu "mpz zambi kwenda huko"
 
Ili ubarikiwe na maisha yaendelee lazima usamehe.
Ila nachoweza kushaur tu kwa kipindi hiki ambacho upo serious watafuta mke hebu jikabidhi kwa Mungu kwani yeye atakupa mke wa kufanana na wewe.
Tatizo letu tunatumia macho na akil zetu kutafuta mke na tunamsahau Mungu......huna haja yakuchukia wanawake kwa kosa la wanawake 2 uliokutana nao.MUNGU ANAWEZA,akil ya binadamu inapofika mwisho bas Mungu ndipo anapoanzia!!!!!
 
Tatizo mnatafuta mademu wa swiming pool arafu mnataka wawe wake zenu we unaelekea una matatizo ya kuchagua.
Ni hivi broo hawa wasichana kuna brandy ya kuoa na brand ya kuchezea sasa wewe unataka kuoa wale wa kuchezea

pa kumpatia sio sababu ila ni kama umeongea point kuwa kuna wa kuoa na kuchezea sasa utawajuaje wakati unakutana nao mara ya kwanza? na kama mtu unakaa naye zaidi ya miez 6 mpaka mwaka anakuwa anaelekea kuwa mke mwema na mbele ana change kama hivi si tutaoa baada ya kukutana na wanawake zaidi ya 10 jaman??
 
kuna sehem ya kupreview post,ungefanya hivyo ingekua bora zaidi.........

I find it so hard to believe this story hasa the last part ya ufumanizi,kupigiwa sim

ila kama ni kweli pole yako,

ni kama stor au move, na nilichogundua kuwa watu walikuwa nananionea huruma kwa madhambi yake aliyokuwa anatenda bila mm kujua!!
 
thanks but kumbuka ni mara 3 na wana wake 3 tofauti!! sasa nikikaa tena hata miaka 2 na huyu wa 4 si ndo atakuwa zaidi jamani?
Ndio maisha ndugu yako hayana mteremko yamejaa misukosuko na misukosuko hio ndio inatupa nguvu,busara na hekima za kuwa watu tulio sasa...Kumbuka kuna watu wana matatizo kuzidi yako wewe..We shukuru mungu na uombe akupe mke mwema na inshallah dua zako zitasikika...
 
Tatizo mnatafuta mademu wa swiming pool arafu mnataka wawe wake zenu we unaelekea una matatizo ya kuchagua.
Ni hivi broo hawa wasichana kuna brandy ya kuoa na brand ya kuchezea sasa wewe unataka kuoa wale wa kuchezea

Hii dhana yakuchezea mwanamke huwa sielewagi!!!!!unamchezea how wakati kama kufanya mnafanya wote..........mwanaume anayejitambua pia hachezei mwanamke.
 
Mkuu hawa watu ni kuwa nao 50/50 tu usiwaamini kivilee saa yoyote wanabadilika. Wengine tulishaga umizwa mioyo mpaka sasa tumeota sugu. Ni viumbe wa ajabu sana hawa.
 
Dunia hii si kwamba uaminifu umepungua sana bali teknolojia imeongezeka kiasi kwamba ni rahisi kugundua uovu wa mwenzako ikiwa utadhamiria.

Jambo la kufanya ni kuwa na moyo mwepesi wa kusahau, kikubwa fahamu unatakiwa ufungue mlango wa maisha ya ndoa na mkononi unazo funguo nyingi wakati inahitajika moja tu ya kufungua, hivyo usichoke kujaribu funguo zingine kwani yawezekana funguo halisi iko mwishoni.
 
hicho ndo kitu nahisi ni dhambi kwangu!! ku change na kuwa na wasichan tofauti!! sema nako elekea itabidi nijifunze
 
dah... Pole sana ndugu yangu...majarib mengine mazito kweli.
Siwezi kukushauri umsamehe. Rudi ktk sala na maombi ya kuomba mwenza wa maisha. Mungu atakujibu.
 
Mkuu hawa watu ni kuwa nao 50/50 tu usiwaamini kivilee saa yoyote wanabadilika. Wengine tulishaga umizwa mioyo mpaka sasa tumeota sugu. Ni viumbe wa ajabu sana hawa.

daaah naweza amini maneno yako 100% asante mkuu, pia pole kwa maumivu uliyopataga na mimi inaniuma saana
 
Back
Top Bottom