Inakuwaje vilaza wengi ndiyo waajiri wakubwa wa vipanga wengi?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,018
16,802
Nimekuja kugundua kuwa wale wanafunzi ambao walikuwa na ufaulu mbovu au mdogo hasa kuanzia kidato cha nne ( 4 ), cha sita ( 6 ) na vyuo vikuu huku maishani ndiyo wamekuwa kimbilio ( waajiri ) wakubwa wa wale wanafunzi ambao walikuwa na akili / uwezo mkubwa sana darasani.

Je kimantiki hii inatafsiri gani wakuu? Na je ina athari yoyote kwa kilaza mwajiri na kipanga mwajiriwa?
 
Ukitoa thread kama hii bila evidence za kusupport inakuwa sio valid...lete mifano hai...
 
vilaza wanakuwaga hawaajiriki..

so wanaamua kujiajiri... na baada ya msoto mrefu wanatoboa na kuwa matajiri.. na vipanga sababu wana vyeti vizuri na wanaajirika wanaenda kuomba kazi kwenye kampuni za vilaza...

vipanga wanajua sana ku calculate risk za investment ndio maana wanaogopa sana kujiajiri.

kilaza haogopi yeye anawekeza tu anaamini ujasiri ndio utamtoa maana hana vyeti vya kuajirika
 
Mfumo wa Elimu ndo hufanya mtu aonekane kilaza au kipanga... Mfumo wetu hapa Bongo ni ule wa kukariri (yaani watu wanasoma ili wafaulu tu) So kama una kumbukumbu nzuri utaonekana kipanga... Mifumo ya nchi zingine kama France na UK zinamfanya mwanafunzi anaye-reason na kufikiria independently kuwa ndiye kipanga...na actually mtu mwenye critical mind with rational reasoning na ndiye ana nafasi kubwa ya kufanya outstanding things..
So wasomi wa Bongo wengi ni vilaza wa sehemu zingine zilizoendelea duniani.. Hawana creativity (imeuawa), Hakuna critiques, hakuna mawazo mbadala.. (Hata kama yapo watu hawana confidence) So 90% + ya wasomi Bongo lazima waajiriwe.
Hawana quality za kuajiri.
 
Endelea kuelimisha watanzania wenzako wawe vilaza, ili waje kutuajiri...........advance.OTE]
Waje kuwaajiri?inamaana wewe ni kipanga?komaa mimi ntakuajiri mana nina makarai mengi kila UE utafikiri natafuta credit niende advance.
 
Nimekuja kugundua kuwa wale wanafunzi ambao walikuwa na ufaulu mbovu au mdogo hasa kuanzia kidato cha nne ( 4 ), cha sita ( 6 ) na vyuo vikuu huku maishani ndiyo wamekuwa kimbilio ( waajiri ) wakubwa wa wale wanafunzi ambao walikuwa na akili / uwezo mkubwa sana darasani.

Je kimantiki hii inatafsiri gani wakuu? Na je ina athari yoyote kwa kilaza mwajiri na kipanga mwajiriwa?

Huo utafiti umefanyaje?

Kutengeneza hela inabidi ujue binadamu wana mahitaji gani.

Tigo wanatoa huduma za mawasiliano kwa watu zaidi ya milinoni 11.

Kila mtu anahitaji kuongea na simu.

Mvumbuzi wa simu aligundua hilo. Akaitengeneza simu na kuiwekea bei.

Alitatua tatizo la kutuma barua kwa watu wanoishi masafa ya mbali.

Huhitaji elimu ya chuo, au sekondari.

Unahitaji kujua binadamu wanataka nini.

Na utengeneze bidhaa kwa ajili ya mahitaji yao.

Matajiri wote unaowajua wewe. Sio wajinga kama unavyofikiri.

Wana elimu muhimu ambayo haifundishwi chuo.

Elimu yao inatoka duniani.

Wanajua mtu kama wewe unataka nini. Wanatimiza mahitaji yako kwa bei.

Ukinywa soda, jua ya kwamba kuna mwanaume nyuma ya pazia.

Kachunguza tabia yako, kagundua kwamba ulimi wako unapenda vitu vitamu.

Na bidhaa ni kitu chochote. Kuna watu ''wajinga'' wanmiliki kampuni za kuzoa takataka.

Wanafanya hivyo kwa bei. Wanahitaji elimu. Lakini sio elimu ya kuandikiwa ubaoni. Au kupewa notsi.

Wana elimu ya uzoefu ya kusaidia binadamu.

Wanafanya kazi masaa mengi sana ambayo wewe huwezi kuona. Na kila lisaa wanalotumia, wanawaza jinsi ya kukutoa hela mfukoni mwako.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya ''wasomi'' na wajisiriamali.
 
Back
Top Bottom