Inakuwaje unamuacha mpenzi wako wewe mwenyewe, kisha unakuwa king’ang’anizi?

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Kuna wanaume na wanawake wana maisha magumu, anafanya uamuzi wa kuvunja mahusiano yake tena wengine kwa mbwembwe na matusi juu, ila baadae anarudi tena na kulilia penzi alilolivunja.

Wapo tayari kuharibu mpaka maisha ya aliyemuacha ili mradi amrudie, kumtisha, kumnyanyasa kama ana cheo ofisini na kumfatilia kama tamthilia.

Kushindwa kuishi katika maneno uliyoyatoa.
Hasira inapotawala ni rahisi mtu maneno kumtoka na kujipa uhakika anachokikusudia atakimudu. Lakini baada ya kuachana, anapokuwa pekeake na kuona wengine waliokosana wanaishi vyema, uanza kuuchukia upweke na kujiona hakustahili kuchukua uamuzi aliofanya.

Kugundua ukweli.
Unapoacha mpenzi ama mwenza wako alafu baadae unapata kuujua ukweli, mfano ulimtusi na kumdhalilisha kisa maneno ya watu au hisia zako mbaya, alafu unagundua sio kweli bali ulimhukumu bure. Huja ugumu kwa mtu kukubali kumkosa aliyemuacha kwani majuto umtawala.

Kuiona thamani ya uliyenaye.
Ni rahisi kutoiona thamani ya mapenzi unapoacha kwa kuwa unapata ngono kwa mpenzi mwingine au kupata uhusiano mpya unaokupetipeti wakati huo, ila pale unapopata changamoto kwa huyu mpya, tayari mawazo ujaa na kuona ni bora uliyemuacha na hapa ndio tunaposema ya kheri shetani unayemjua na sio malaika usiyemjua.

Kuzama kihisia kwa uliyemuacha. Unaweza toa uamuzi ila ukawa ni wa kwenye akili yako ila kihisia ni tofauti. hapa ndio kupatwa kwa akili hutokea, umeacha kwa ujasiri lakini muda kwenda unateseka kihisia mpaka unapata msongo, unakondeana, mambo hayaendi na mwisho unaanza kummisi na kumhitaji.

Kufanya uamuzi kwa kuogopa watu na kutizama jinsia yako.
Kuna wapenzi na wenza wanapokosewa na wenza wao, wao uwaza tu watu watanionaje ama mimi mwanaume haiwezekani ama mimi ni mwanamke ni pesa natafutwa na kila mtu au kuna mtu unachepuka nae anakupa jeuri kwahiyo unaamini ili uonekane unamsimamo au unapenda mchepuko wako, unaamua kumwaga penzi lako la zamani kutokana na changamoto,lakini baada ya yote hawa watu hawakusaidii na unabaki pekeako, ni ngumu sana kiisemea akili ya mtu au watu. Ukisikia mtu kafumania na kasamehe sio bure.

Wivu kwa uliyemuacha. Ni wachache wanaoweza kuacha na kuvumilia ama kuwapuuza waliowaacha, wengi uishia wivu kila amuonapo ama kasimama na mtu. Akili yake uona kuendelea kuwa nae ni bora kuliko fedheha. Ndio maana wengine waliokusudia kuacha uamua kuhama eneo analoishi ili kuepuka kumuona mara kwa mara.

Kutoteteleka kwa aliyemuacha. Raha ya anayeacha huwa ni kumuona aliyemuacha anateseka na anadhoofika. Lakini wengine uwa imara na kupambana na maumivu yao na maisha yao

Hili umpa homa aliyeacha kuona yeye ni wa kawaida sana alikuwa ndio maana aliyemuacha hajateteleka bali anasonga mbele na maisha yake.Hivyo ili kuikwepa aibu utaka amrudie.

Kutojiamini.
Wapenzi huweza kukaa muda mrefu lakini wakawa hawaaminiani, hivyo uanza kutingishiana viberiti kama kipimo aone kama anapendwa kweli, lakini mwisho uachwa kweli. Kutokujiamini umaanisha mtu hayupo tayari kupoteza aliyenaye ila anatishia tu kuona muitikii wa mwenzie kimapenzi. Ameshaharibu ila kubakia upendo anautaka ila ndio kashaharibu.

Hivyo ni lazima unapofanya maamuzi, usikurupuke na usitizame watu wanaokuzunguka bali jitazame wewe mwenyewe kiakili, kihisia na kimaisha, unapokosa kutulia ndio kutafuta kujitesa kwako.

Na unapoamua kuacha, kubali kupambana na hali uliyokubali kuianza, tambua maamuzi yoyote uenda kuwa sahihi kama yanakutoa katika baya kiakili, kihisia na kimaisha. Jifunze sio kila mahusiano uanayo imara, kuwa hayana changamoto au hayaja wahi kuwa na changamoto, bali ni maamuzi yalio wafanya washibane na kuendelea kuwa pamoja.
20221020_125603.jpg
 
Back
Top Bottom