mhhh usifanye hivyo..... A Problem Shared is Half a Problem........ lakini inabidi tuangalie ni nani tunaongea nae na ni kweli matatizo ya wapenzi inabidi wenyewe ndio wayasolve sababu wanajua kuhusu matatizo yao kuliko mtu mwingine yoyoteninapofikiri hapo huwa naona bora matatizo yangu nife nayo.
Habari zenu wapenzi wangu wote wa MMU??
Hili jambo nimelifikiria kwa muda mrefu, na kila siku nazidi kulifikiria ila nakosa jibu. Watu wengi wanapokuwa kwenye mahusiano eg wapenzi, inapotokea wamegombana wanatafuta mtu mwingine awasuluhishe na mara nyingi huwa anafanikiwa. Swali ninalojiuliza, inakuwaje mwanamke/mwanamme haupo tayari kumsikiliza mwenzio na kumuelewa ila upo tayari kumsikiliza mtu wa pembeni? Hivi inaleta picha gani baada ya nyie kupatana baada ya kusuluhishwa na ndugu au rafiki?
Binafsi nafikiri kama mpenzi wangu hatonisikiliza mimi, sitokuwa tayari amsikilize mwingine kwa niaba yangu na kama sipo tayari kumsikiliza yeye na kutatua tatizo basi sitoweza kumsikiliza ndugu wala jamaa yake. Wewe je unaonaje?
sijajua umemaanisha kuongelea kimtindo upi. Kuna wengine huongelea matatizo baada ya kuwa washayatatua (napendelea zaidi hili), wengine huongelea matatizo kwa wakati ule ambao wapo kwenye matatizo kwa nia wasaidiwe au waonewe huruma.Kuongelea matatizo yako na mtu mwingine ni behaviour inayokubalika kama utamshirikisha friend or family member, au confidant ambaye anaweza kukupa unbiased perspective. .
Habari zenu wapenzi wangu wote wa MMU??
Hili jambo nimelifikiria kwa muda mrefu, na kila siku nazidi kulifikiria ila nakosa jibu. Watu wengi wanapokuwa kwenye mahusiano eg wapenzi, inapotokea wamegombana wanatafuta mtu mwingine awasuluhishe na mara nyingi huwa anafanikiwa. Swali ninalojiuliza, inakuwaje mwanamke/mwanamme haupo tayari kumsikiliza mwenzio na kumuelewa ila upo tayari kumsikiliza mtu wa pembeni? Hivi inaleta picha gani baada ya nyie kupatana baada ya kusuluhishwa na ndugu au rafiki?
Binafsi nafikiri kama mpenzi wangu hatonisikiliza mimi, sitokuwa tayari amsikilize mwingine kwa niaba yangu na kama sipo tayari kumsikiliza yeye na kutatua tatizo basi sitoweza kumsikiliza ndugu wala jamaa yake. Wewe je unaonaje?
sijajua umemaanisha kuongelea kimtindo upi. Kuna wengine huongelea matatizo baada ya kuwa washayatatua (napendelea zaidi hili), wengine huongelea matatizo kwa wakati ule ambao wapo kwenye matatizo kwa nia wasaidiwe au waonewe huruma.
Mie tabia hii inanikera sana kusema kweli ila namshukuru Mungu katika mahusiano niliyowahi kuwa nayo hakujawahi kutokea tatizo la kumshirikisha 3rd party ili kutafuta usuluhishi wa tatizo lilikuwepo.
Kwanza naona ni kuwapa faida watu wengine wayajue matatizo yenu na si ajabu kuyatangaza kwa watu wengine na wao kuwa wanawachora tu kila wawaonapo.
Mna matatizo yenu kaeni chini hata kwa masaa, siku hata wiki ili kutafuta suluhisho kama kweli wote mna nia ya kumaliza tatizo lilikuwepo basi ni lazima tu mtafanikiwa ila kama mmoja ana ajenda zake za siri basi itakuwa ngumu sana kupata suluhisho.
mkuu namaanisha kuongelea tatizo ili uonewe huruma na utatuliwe, mfano mmegombana mnatafuta mtu awasuluhishe, hiyo sikubali nayo na hata wadau hapo chini wamechangia vizuri tu ubaya wa kuwaambia watu matatizo yako. Binafsi nahisi ni bora kama unapenda watu wayajue matatizo yako, waambie wakati ushayatatua. Hapo itaonyesha pia ni vipi upo imara. Kama mdau mmoja alivyocomment hapo chini kuwa wengine hufurahi kuona wenzao wapo kwenye matatizo, wengine wana matatizo zaidi yako na wengine hawapendi kusikiliza matatizo ya watu. Matatizo yetu tutafte namna ya kuyatatua wenyewe.Kwa hiyo kati ya hayo mawili ni lipi unazungunzia? Kuongelea tatizo baada ya kulitatua au kuongelea tatizo kabla ya kulitatua? Kama ni kuongelea tatizo baada ya kulitatua, then I can't see the point of doing that. Sidhani kama wataweza kuongelea tatizo ambalo tayari wameshalitatua, b'se hakuna tatizo hapo tena. Kama ndipo ulipobase argument yako, then tuko pamoja. Lakini kama ni kuongelea tatizo kwa wakati ule ambao upo kwenye tatizo kwa nia ya kutaka usaidiwe au uonewe huruma, then kutokana na nilivyosema kwenye post yangu ya mwanzo that is perfectly fine.
Fikiria hapo mnaenda kuanika madhaifu yenu kwa watu halafu baada ya hapo mnapatana, mnaanza kuambatana. Wale wasuluhishi wenu wanawatazama tu, na gumzo juu, wale usiwaone vile yule mwanaume yulo hivi na hivi yule mwanamke ndo usiseme...dah na ukishasema hayafutiki. Tumalizane humu ndani bana mzee!
mkuu namaanisha kuongelea tatizo ili uonewe huruma na utatuliwe, mfano mmegombana mnatafuta mtu awasuluhishe, hiyo sikubali nayo na hata wadau hapo chini wamechangia vizuri tu ubaya wa kuwaambia watu matatizo yako. Binafsi nahisi ni bora kama unapenda watu wayajue matatizo yako, waambie wakati ushayatatua. Hapo itaonyesha pia ni vipi upo imara. Kama mdau mmoja alivyocomment hapo chini kuwa wengine hufurahi kuona wenzao wapo kwenye matatizo, wengine wana matatizo zaidi yako na wengine hawapendi kusikiliza matatizo ya watu. Matatizo yetu tutafte namna ya kuyatatua wenyewe.
ok nilikutongoza mwenyewe na ww kwanini uwape wengine......mi pia jaman hii tabia siipend kwel kama uliweza kunitongoza kwa nn tukikosana uniogope
yaani wewe ndio umeelewa topic vizuri kabisaaa. Tumeishi wote miaka mingi ila usinielewe wala kusikiliza ninayokwambia aje 3rd party akwambie yale yale umsikilize na ukubali.umeshindwa kunielewa mimi ukumuelewa huyo third part! .
EMT kiukweli ndivyo watu wanavyoishi wanatafuta wasuluhishi wanarudi tena kukaa chumba kimoja! Inauma ujue yani umeshindwa kunielewa mimi ukumuelewa huyo third part! Wakati unaniambia unanipenda? Kha mioyo ya binadamu mibaya sana.
Ni vyema wanandoa/wapenzi kumaliza mambo yao wenyewe..kama watu wawili walikutana na kuwa pamoja, hata wakati wa migogoro wawe pamoja kuyamaliza.
Laa ikitokea kumshirikisha mtu basi kuwe na mipaka ya kitakachoongelewa..Naamini wengi wanashirikisha watu kwa kupanic, stress na mawazo ambapo hukuta ameshasema yanayomtatiza hata kama aliapa asingefungua mdomo..ikiwa anayeshirikishwa ana roho nzuri pia experience ya jambo kama hilo anaweza kutoa shauri nzuri kama vile kujishusha,kusamehe na kutoa moyo kuwa hizo changamoto zinatokea hata kwa watu wengine..
Mind you, ujue nini unaongea na unaongea na nani!!..mwisho wa siku ni kujitahidi kupambana na kutatua matatizo binafsi kwa wapenzi wenyewe maana ni sehemu ya maisha!!
FA hii umenipa elimu mpya....nilikuwa najua na mpaka sasa naamini wanawake ndio wenye tabia ya kutoa mambo ya ndani nje kumbe wanaume pia!!Nadhan mtoa mada umeuliza swali na kujijibu! Kutokubali kujishusha kwa mmoja wa wapenz huchaangia kuhusisha mtu wa nje! Kila Mmoja akipanda hata mkeshe hamtafikia muafaka.... Ila kuna mazingira mengine ambayo huchangia pia, mfano mmekwaruzana na shem, unamwangukia kuomba msamaha shem hataki kabisaaa kukusamehe, nawe wampenda lazima utatoka 'ukajishtaki' kwa mtu mwingine ili aje akuombee msamaha (ilaa kama kosa linatishia kuachwa)Mie naona kama unavyoona.Halafu hii tabia ya baadhi ya wanaume kusambaza taarifa za ndani ya nyumba zao au mapungufu ya wake zao kwa ndugu zao ndio inayosababisha ndugu waanze kumchukia mkeo, mpenzio. Ukiingia kwenye mahusiano ikiwamo ndoa, jua fika umekuwa mkumbwa na umeanza familia ambayo ni baba, mama (na watoto kama mtabarikiwa). Aibu yako ni aibu ya familia na aibu ya familia ni yako.