Inakuwaje Mtu anakuwa mkatili kwa mama watoto wake hivi.

Hapana aisee. Na hapo wanapozungumza ni kana kwamba huyo jamaa bado yuko uraiani na anaendelea na kazi kama hakijatokea kitu. Stori haijakamilika hii, watu au majirani waliamua kulia tu na kumuacha huyo jamaa aendee?

Anayeiba huwa anaadhibiwa na wananchi wenye hasira kali, hapo hakukuwa na wananchi wenye uchungu uliopitiliza, wakaondoa mkono wake kwa panga hilo hilo?

Na wanawake, hii tabia ya kupigwa, kunyanyasika, kisha unaendelea tu kung'ang'ania huko, ni UJINGA uliotukuka.

Wazazi, mtoto wa kike akipata ujasiri wa kushtaki au kukimbilia nyumbani kwa violence yoyote atakayofanyiwa na mwenzi wake, ni UZAMANI usio na tija kuanza kuangalia PRIDE yako itakuaje mbele ya jamii ikiwa mtoto wake ameiacha ndoa na kurudi nyumbani, na kuanza kumlazimisha arudi kwa mume, eti akavumilie tu ndio ndoa hiyo.

Shambulio la kimwili ni kosa kisheria, mara moja mara mbili, msweke ndani na usirudi kwake. Achaneni na mambo ya kusuluhisha kifamilia, aaaargh.

Huo ulemavu utafutwa na samahani? Ama awekwe mirembe maisha yake yote AU segerea, hamna mjadala.
 
Katika kitu huwa kinanipa hasira ni tabia ya wanawake wanaokuwa abused wengi wao huwa wanapenda kulazimishia kubakia kwa muhusika hadi makubwa yawafike.

Halafu utadhani wanakuwa wameandikiwa kudhuriwa na hawa wajaalaaana. Unakuta mtu anapigwa yeye anakalia kusema kama unaniuwa uniuwe tu me nitaendelea kuwa hapa kwaajiri ya watoto.

Au unakuta mnasaidia kumtoa jamaa linabembeleza arudi kwa simu hadi anakubali anarudi anakaa miezi au mwaka matukio yanaanza tena.....

Its like wanaenjoy kuwa abused. Sasa kama huyu jamaa alishaanza kumfanyia ukatili kitambo, matusi, kipigo, na kumtishia ila amesubiria hadi yamemkuta haya....
 
Back
Top Bottom