Inakuwaje mawaziri kudai hadharani kuwa hawashirikishwi kwenye maamuzi na viongozi wa mashirika yao?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Hili jambo huwa linajirudia na likishatokea basi kiongozi wa shirika anakuwa kafara hapo hapo na mara zote rais Magufuli amekuwa akimuunga mkono waziri husika.

Alianza Dr. Mwele Malecela wa NIMRI dhidi ya waziri wake Ummy Mwalimu na waziri akatangaza hadharani kuwa hakushirikishwa kwenye utafiti thidi ya homa us Zika nchini. Hali hiyo ilipelekea kuondolewa kwenye nafasi yake kama mkurugenzi wa taasisi hiyo iliyoko chini ya wizara ya afya.

Juzi kwenye swala la umeme ndugu Sospeter Muhongo naye akatangaza kuikana hadharani EWURA na TANESCO kuwa yeye kama waziri hakushirikishwa kwa namna yoyote ile dhidi ya upandishwaji wa bei ya umeme. Waziri huyo akaenda mbali zaidi akiwatuhumu viongozi watendaji wa TANESCO kwa kufanya makusudi kulihujumu shirika. Hali hiyo ikapelekea ndugu Engineer Mramba Feleschemi kung'olewa kwenye nafasi yake hiyo kama mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo lililoko chini ya waziri Sospeter Muhongo.

Nini tatizo? Je ni kweli kuwa hawashirikishwi?

Mawaziri huwa wanapanga bajeti za kila mwaka na ndiyo hasa wanaofuatilia utekelezwaji wa bajeti hizo kwenye taasisi zilizo chini ya wizara zao. Sasa watueleze na wao kuwa bajeti zao wanazopanga ni hewa kwakuwa hawashirikiani na viongozi wa mashirika yaliyo chini ya wizara zao? Huenda bajeti ya Sospeter Muhongo aliyoitoa katikati ya mwaka jana ikawa ni bajeti hewa kwani pengine hasa angekuwa amekaa na menejimenti ya TANESCO basi hata swala la gharama za umeme lingejadiliwa kwa kina. Nasema hivyo kwakuwa bei elekezi ilitolewa baada ya bajeti kusomwa.

Kwenye wizara ya afya pengine ndiyo maana kuna hadi matatizo ya chanjo muhimu, yote haya yakiwa ni matokeo ya bajeti hewa isiyoendana na hali halisi ndani ya wizara hiyo na pengine ni matokeo ya mawaziri kutokushirikiana ipasavyo na viongozi wa taasisi zilizo chini yao.

Mwisho niseme kuwa waziri kutoka hadharani na kumkana msaidizi wake wa chini kwenye taasisi anayoingoza yeye tena baada ya kila kitu kuwekwa hadharani ni udhaifu mkubwa na inaonyesha ama kuna usaliti kwa maslahi ya kisiasa ama uzembe wa hali ya juu! Kumvumilia waziri wa aina hii ni sawa na kuhifadhi "kinyesi" kwenye nguo ya ndani kisha ukatembea nacho! Kitakuwa kinaendelea kutoa harufu kali na mbaya na mwisho ile harufu itazoeleka kwa usugu!
 
Sakata la Tanesco muhongo kaonesha udhaifu wa hali ya juu....hadi mchakato wa kupandisha bei vikao vimefanyika na wadau kushirikishwa inamaana katika ngazi zote hakujua mpaka lifikie mwisho ndio atoe tamko??? Vikao vingapi vimefanyika na wametumia pesa kiasi gani hadi mchakato unakamilika....?? Ulikuwa wapi muhongo ??????
 
Kesho Hao Hao ndio watakanusha na kusema kuwa wanashirikishwa na kuna mawasiliano mazuri Sana
 
Ufanyaji kazi Wa viongozi wetu unatia mashaka sana.Inaonekana Hakuna mawasiliano.Kila mtu ni kambale.
 
Au hii
downloadfile.jpeg
 
Ni yeye Hana akili au hoja yake haina akili!?
Tuachane Na akili zake, zungumzia kuhusu hoja yake.

Napenda kuiona akili yako ilivyokubwa ikijibu hoja za mdau!

Mtoa mada ameongelea coordination na hajapinga kuzuia umeme kutokupandishwa, tatizo lake ni lipi? Waziri alishindwaje kumpigia CEO wakaongea kiofisi? mambo mengine ni kutaka sifa za wazi. Toka October mpaka tarehe 30 Dec ndiyo kapata taarifa? rejea kwa Mafuru na mtoto wa Malecela.
 
Huwa nawashangaa sana hawa mawaziri...eti wanakuja mbele kabisa tena na munkari wa kutosha kuwa ''sikushirikishwa'' what a shame. Waziri??!! Shirika lipo chini ya Wizara yako linafanya maamuzi fulani unakuja kulialia mbele ya wananchi eti kuwa hukushirikishwa...wewe ni waziri kamili au waziri kivuli??

Cha kusikitisha sana badala ya Mkuu wa nchi kumuwajibisha waziri husika kwa kushindwa kusimamia tahasisi na idara zilizo chini ya Wizara yake...eti na yeye anakuja na ngonjera zake kuwa nampongea naniliu kwa uamuzi wake wa kinaniliu. .these shits happen only in Tanzania.

Mtu wa kwanza kuwajibika endapo uchafu fulani utafanyika kwenye idara iliyochini ya Wizara fulani nadhani ni karibu Mkuu kama Mtendaji Mkuu wa Wizara akifuatiwa na waziri.

Kwenye sakata la EPA mama naniliu alisomeshwa namba kwa sababu tu ishu ilifanyika katika tahasisi ikiyochini ya Wizara yake. Alipoulizwa alijitetea kuwa alidanganywa na wakuu fulani Kutoka tahasisi fulani. Utetezi huo haukufanya aonewe huruma....alisomeshwa namba. Sasa itakuweje kwa mawaziri wa Wizara tajwa kwenye Uzi wanasema eti hawakushirikishwa kwenye mchakato uliofanyika ndani ya Wizara wanazoziongoza??

Hivi kweli Muhongo anataka kutuambia pendekezo la kupandisha bei ya Umeme na kupelekwa ewura...ewura wamelipokea na kulifanyia Kazi kwa kushirikisha wadau mbalimbali na matangazo walikuwa yanatolewa kwenye vyombo vya habari... Ewura wamekuja na bei yao na kuiwasilisha kwa wananchi..eti muhongo ndo anajitokeza na kusema hakushirukishwa...ulikuwa Wapi MZEE husishirikishwe...Je baada ya kuona/au hata kusikia kuwa kuna mchakato wa kupandisha bei ya Umeme kwenye shirika lililochini ya Wizara yako...MZEE ulichukua hatua gani??


Ebu mawaziri wa magufuli acheni kutufanya watu wazima kama watoto wadogo bwana...Khaaaaa
 
Sakata la Tanesco muhongo kaonesha udhaifu wa hali ya juu....hadi mchakato wa kupandisha bei vikao vimefanyika na wadau kushirikishwa inamaana katika ngazi zote hakujua mpaka lifikie mwisho ndio atoe tamko??? Vikao vingapi vimefanyika na wametumia pesa kiasi gani hadi mchakato unakamilika....?? Ulikuwa wapi muhongo ??????
Hakushirikishwa...na hakutoa tamko bali katekeleza sheria ya nishati inayompa madaraka waziri kutengua mapendekezo yoyote ya ewura.
 
Back
Top Bottom