Madhara ya kubadili Baraza la Mawaziri mara kwa mara

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
365
303
Wanabodi,

Wizara yoyote ni muhimu katika suala zima la kutoa huduma kwa wananchi na kuleta mageuzi yenye ubunifu kwenye maendeleo ya jamii. Hii ndiyo ingetakiwa kuwa kauli mbinu ya wizara yoyote Ile nchini Tanzania. Ubunifu huu ambao unaweza kuleta maendeleo ya kudumu huhitaji mipango thabiti na utekelezaji mzuri wa mipango kwa muda mrefu.

Serikali imekuwa na mtindo wa kubadilisha baraza la mawaziri mara kwa mara kwa sababu ambazo haziko wazi kwa wananchi na kwasababu hiyo ni ngumu kuelewa kama maoni yangu yanaweza kuchochea mabadiliko yoyote.

Kwanza kabisa tuelewe kwamba ubunifu kwenye kitu chochote unaanza kwa kuwa na ujuzi. Ni muhimu kwa serikali kuangalia kama ujuzi wa waziri yoyote unaendana na wizara yake. Ujuzi huu na uzoefu ndio utamwezesha waziri wa madini kuwa na mchango kwenye negotiations na kampuni ya wawekezaji kutoka nchi ya nje, ujuzi huu ndio unge muwezesha waziri wa fedha kutatua changamoto ya upungufu wa Dola nchini, ujuzi huu ndio unge muwezesha waziri wa afya kufufua shirika la bima ya afya.

Kwa kubadilisha Baraza la mawaziri mara kwa mara bila kuzingatia ujuzi wa mawaziri tunao wahamisha tuna dumbukia kwenye mtego wa kuwa na mawaziri ambao kazi yao ni kusema ambacho serikali inawataka waseme kwenye vyombo vya habari bila ya wao kuwa na mchango muhimu kwenye wizara zao. Ujuzi pia wa wizara inayo hudumiwa ni mwanzo wa kuboresha wizara hiyo na kuleta maendeleo ya kudumu.

Hata kama waziri hana ujuzi wa kutosha, ni muhimu kwa wizara kuwa na range kubwa ya wataalam wa kutosha katika sekta husika. Vilevile dira ya maendeleo ya 2050 inatakiwa kuainisha vya kutekelezwa na kila wizara. Dira ya kila wizara haiwezi kutekelezwa na waziri wa muda mfupi
 
Kuna mkeka mwingine unakuja Leo au kesho kitu cha msingi ni mama anaboresha panapovuja
 
Back
Top Bottom