Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,620
- 6,510
Moja ya alama ya mtu yoyote aliyesoma na kuelimika ni uongeaji wake. Hata mtu ambaye hajasoma shule sana ila ni msomaji wa vitabu, ni rahisi kumtambua. Kuanzia upangaji wake wa maneno, akiwa anatoa mawazo yake, nk.
Mwigulu sijawahi kumkubali kwa sababu toka nimeanza kumsikiliza day 1, naona ni mtu anayejaribu kuficha madhaifu yake ya kifikra kwa kuweka sura ya kujiamini na kuchekacheka ila ukimsikiliza vizuri utagundua kabisa si mtu aliyeelimika wala kuwa na ufahamu wa mambo anayopewa majukumu ya kuyasimamia. Ni wale watu wajanja wajanja tu.
Makonda amesemwa kwa mengi. Kuanzia kumkwida Warioba kipindi kile kwenye Bunge la Katiba kama sikosei, utajiri wa ghafla kipindi akiwa Mkuu wa Mkoa, kuhusishwa na tukio la Lissu na mengine ya utekaji kipindi cha Magu, nk. ila jamaa ana kitu mabeberu wanaita yuko "articulate". Yaani anaongea kwa ufasaha. Sijajua ni kipaji au ni mtu ambaye anapenda kujisomea maana wote tunajua hana elimu kuuubwa.
Ukiwasikiliza wote wawili, ungeweza kudhani Makonda ndiyo ana PhD halafu Mwigulu ndiye "Bashite".
Hapa simaanishi Makonda ni mtu msafi, muadilifu au mawazo yake yote ni mazuri au ya kisomi (mfano wazo la juzi kuwanunulia vifaa waandishi binafsi ni wazo la hovyo sana ingawa tunajua nia ni nini) ila ninachotaka kusema hata akiwa anatoa mawazo mabaya bado ana uwezo wa kujielezea kwa ufasaha hata ukajua msingi wa hayo mawazo yake.
Mwigulu anajiumauma tu akidhani tai ya bendera itambeba.