Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,443
- 40,537
Hili jambo huwa silielewi kabisa. Kweli Mbowe kama binadamu ana madhaifu yake, lakini inakuwaje ni CCM ndiyo wanataka kuweka ukomo wa uenyekiti wa Mbowe CHADEMA?
Yaani ni kama Wamarekani waseme ni kwa nini wajerumani wanaendelea kumchagua Angela Merkel kuwa Kansela wao. CCM kuhusu Mwenyekiti wa Taifa hakuna mahali kwenye katiba yao pamewekwa ukomo wa muda, bali wanabadilishana kwa kutegemea "Tamaduni" ya chama hicho na wala si kwa uchaguzi kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho hakuna kugombea nafasi ya mwenyekiti Taifa.
Sasa chama ambacho huwa hakifanyi kabisa uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa, kinakuwaje na nguvu ya kimaadili kuwaambia CHADEMA wabadilishe Mwenyekiti wao Taifa? Kwani kwenye Katiba ya CHADEMA kuna kipengele kinakataza mtu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa zaidi ya mara moja?