Inakuaje mtu anakuwa na majina manne?

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,299
2,000
Naomba niwaulize wakuu,

Inakuaje mtu anakuwa anamajina manne. Mi naelewa kwa mfumo wa kawaida huwa mtu anakuwa na majina matatu. Yani jina la kwanza, la kati na la mwisho, kwa kienglish ni First name, middle name na last name.

Wengine huwa ni jina la ukoo au lakuzaliwa, la ubatizo au la dini na la mzazi yani Baba. Kwa mfano Julius Kambalage Nyerere au Jakaya Mrisho Kikwete.

Sasa huwa napata kizunguzungu unakuta mtu anamajina manne. Yote ayo anakuwa kayatolea wapi?

Au kuwa na majina manne nacho ni cheo?

Kwa mafano: John Pombe Joseph Magufuli, Nduli Iddi Amini Dada.

Sasa apo nachanganikiwa sielewi la dini au ubatizo ni lipi, la ukoo ni lipi na la baba yake ni lipi. Maana yapo dabble dabble tu.

Kisheria na ki official Ni majina matatu ndyo yanatambulika. Haya mengine ni kutaka kutuchangaya sasa.Nitegulieni hiki kitendawili wakubwa.
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,299
2,000
kumbe umemlenga mtu
Hapana nimetoa mifano ambayo kila mtu atakuwa Rahisi kuitambua. Maana hakuna asiyejua majina ya Maraisi wake. Je ningetolea mfano wa mtu ambaye humtambui si ingekuwa ngumu kukubali?
 
Nassormbaruk

Member
Apr 15, 2014
70
95
Du mimi
NIKUPE MJI
ILA KUNA
JINA LAKO
LA BABA ALIE KUZAA KWA MANTIKI ALIEOWANA NA MAMA
BABA WA BABA YAKO huitwa babu kuna NA nababa WA babu yako inaendelea hivo
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,241
2,000
Naomba niwaulize wakuu,

Inakuaje mtu anakuwa anamajina manne. Mi naelewa kwa mfumo wa kawaida huwa mtu anakuwa na majina matatu. Yani jina la kwanza, la kati na la mwisho, kwa kienglish ni First name, middle name na last name.

Wengine huwa ni jina la ukoo au lakuzaliwa, la ubatizo au la dini na la mzazi yani Baba. Kwa mfano Julius Kambalage Nyerere au Jakaya Mrisho Kikwete.

Sasa huwa napata kizunguzungu unakuta mtu anamajina manne. Yote ayo anakuwa kayatolea wapi?

Au kuwa na majina manne nacho ni cheo?

Kwa mafano: John Pombe Joseph Magufuli.

Sasa apo nachanganikiwa sielewi la dini au ubatizo ni lipi, la ukoo ni lipi na la baba yake ni lipi. Maana yapo dabble dabble tu.

Nitegulieni hiki kitendawili wakubwa.
Iko hivi,
-John ni la kwake.
-Pombe ni la baba yake.
-Joseph ni la babu yake na
-Magufuli ni la ukoo wake.

Mimi pia nina majina manne.
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,299
2,000
Iko hivi,
-John ni la kwake.
-Pombe ni la baba yake.
-Joseph ni la babu yake na
-Magufuli ni la ukoo wake.

Mimi pia nina majina manne.
Kwa mfumo huo kila mtu anamajina manne. Ila kwa mfumo wa kawaida kuita majina. Jina la babu ndilo hutumiaka kama jina la ukoo.

Kama jina la babu yako sio jina la ukoo basi uyo atakuwa babu wa kambo.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,241
2,000
Kwa mfumo huo kila mtu anamajina manne. Ila kwa mfumo wa kawaida kuita majina. Jina la babu ndilo hutumiaka kama jina la ukoo.

Kama jina la babu yako sio jina la ukoo basi uyo atakuwa babu wa kambo.
Kabila gani wewe? Yawezekana kabila lenu ndo mnafanya hivyo, mfano, babu yangu anaitwa Samson, je hilo linafiti kuwa la ukoo??
Kwa wale wenye majina ya kizungu, je wajukuu wao watatumia majina ya babu zao kama ya ukoo?? NOPE!
 
kasamba12

JF-Expert Member
Aug 18, 2016
341
250
Naomba niwaulize wakuu,

Inakuaje mtu anakuwa anamajina manne. Mi naelewa kwa mfumo wa kawaida huwa mtu anakuwa na majina matatu. Yani jina la kwanza, la kati na la mwisho, kwa kienglish ni First name, middle name na last name.

Wengine huwa ni jina la ukoo au lakuzaliwa, la ubatizo au la dini na la mzazi yani Baba. Kwa mfano Julius Kambalage Nyerere au Jakaya Mrisho Kikwete.

Sasa huwa napata kizunguzungu unakuta mtu anamajina manne. Yote ayo anakuwa kayatolea wapi?

Au kuwa na majina manne nacho ni cheo?

Kwa mafano: John Pombe Joseph Magufuli.

Sasa apo nachanganikiwa sielewi la dini au ubatizo ni lipi, la ukoo ni lipi na la baba yake ni lipi. Maana yapo dabble dabble tu.

Nitegulieni hiki kitendawili wakubwa.
Kitendawili chako hakina tija yeyote kwa maendeleo yetu na ya taifa kwa ujumla, nenda katafute pesa mkuu, hivi vitendawili vya majina havina tija yeyote Mwenye kutumia majina matatu ua mwenye kutumia majina saba ni maamuzi yake tu, hili halina umuhim mkuu
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,299
2,000
Kabila gani wewe? Yawezekana kabila lenu ndo mnafanya hivyo, mfano, babu yangu anaitwa Samson, je hilo linafiti kuwa la ukoo??
Kwa wale wenye majina ya kizungu, je wajukuu wao watatumia majina ya babu zao kama ya ukoo?? NOPE!
Uwezo wako wa kufikiri na kujenga hoja ni mdogo sana. Babu lazima anamajina watatu ambayo moja ni la ukoo. Sumson ni la dini.
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,299
2,000
Kitendawili chako hakina tija yeyote kwa maendeleo yetu na ya taifa kwa ujumla, nenda katafute pesa mkuu, hivi vitendawili vya majina havina tija yeyote Mwenye kutumia majina matatu ua mwenye kutumia majina saba ni maamuzi yake tu, hili halina umuhim mkuu
Basi sawa naona wewe umeingia kazini sasa.
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
53,126
2,000
Hakuna ukomo wa idadi ya majina mkuu...

Mtu atakavyo ndivyo aitwavyo, mzazi atakavyo ndivyo mtotowe aitwavyo n.k

Kimsingi ukomo upo katika matumizi tu, mfano sisi Watanzania na mataifa mengine tunatumia muundo wa majina matatu yaani jina la mwanzo, kati na familia...Kuna mataifa mengine wanatumia muundo wa majina mawili mfano yale mataifa ya mashariki ya mbali, na mathalani Wachina hutanguliza kwanza jina la familia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom