Tatizo sio kiongozi bali wananchi wasiojua nini maana ya maendeleo.
Wakiadiwa maisha bora kwa kila Mtanzania na hawayaoni wao ni sawa tu, kwani hata huo msamiati wa maisha bora hawaujui.
Watu ambao wako tayari kutetea uozo wa vingozi kwa sababu tu wapo madarakani.
Watu wanao amini propaganda bila kujua kwa nini propaganda zimekuwepo.
Watu wasijua kulinganisha maendeleo ya wengine na ya kwao.
Watu wanao ona kila kitu ni sawa tu kwao kiwe kibaya ama kizuri hajui kuchuja.
Watu wasiofahamu kuwa wameletwa duniani kwa faida na si kuja kuabudu Binadamu wenzao.
Watu wasio amini juu ya uwezo wao wenyewe hata wakidanganywa vipi wanakubali tu kwa sababu hawaoni mbadala wa anayewadanganya.
Watu wanao uona ukweli lakini wanalazimisha akili zao kutokuuona.
Watu wasiojibu hoja zaidi ya matusi na kufuatilia maisha ya watu binafsi.
Watu wanao amini kila wanachodanywa na kukifanya sera ya maisha yao.