Inakera, inaudhi, inachefua na.....

Inakera, inaudhi, inachefua na.....

nginda

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
744
Reaction score
82
Mimi ni Mtanzania na ninaishi Tanzania.
Ninao wjibu wangu kisisasa kumchagua kiongozi anayenifaa ili aniletee maendeleo.
Nina wjibu wa kufuatilia ahadi za kiongozi ninayemchagua.
Nina wajibu wa kutathmini anayoniambia na alichonifanyia.
Nina wajibu wa kuona nyendo zake zinalenga kunifanikishia kupata maendeleo.
Zaidi nina wajibu wa kuhoji endapo kiongozi huyo haeleweki.

SASA BASI NINA MAMBO 10 YANAYNIKERA KAMA IFUATAVYO:
1. Kiongozi anapokwepa kushindwa kwake kazi na badala yake anasingizia walioko chini yake kuwa hawamsaidii ilhali yeye ndiye aliyewaweka.
2. Kiongozi anapokuwa akinihutubia kwa njia ya mipasho bila kujibu hoja za msingi ambazo ninahitaji azifanyie kazi na kuleta mabadiliko.
3. Kiongozi anapokuwa anajishughulisha na mambo binafsi yeye na familia yake na kufanya kuwa uongozi alioniomba nao kura ni kwa manufaa yake na familia yake (BMW)
4. Kiongozi anapoahidi ahadi ambazo kiukweli hana uwezo nazo na zaidi anapoteza muda mwingi kujisifia kuwa anafanya kazi kumbe ni ubabaishaji.
5. Kiongozi anapoteza muda mwingi kusafiri safari kwa safari ambazo kimsingi hazina manufaa kwa wananchi wake.
6. Kiongozi anapoacha kufuatilia mambo muhimu ya msingi kulingana na hadhi yake na badala yake kukimbilia kazi za itifaki ambazo kimsingi walioko chini yake wangeweza kuzifanya.
7. Kiongozi anaponyamazia mambo mazito na yanayohatarisha amani kama uchochezi wa kidini na badala yake anasema kuwa, ‘nimechoka' bila kuchukua hatua, sijui nani afanye kazi kwa niaba yake.
8. Kiongozi anapoacha kutimiza ahadi zake na wananchi wanpohoji anawaita wenye "kijiba cha roho" na wametumwa na wapinzania wake.
9. Kiongozi anapofikia pahala anaona kila kitu kinaporomoka, badala ya kutafuta ufumbuzi yeye anasimama kwenye majukwaa na kujitapa kuwa mambo yako saaaafi.
10. Kiongozi anaposafiri angali nyumbani kwake au kwa wapiga kura wake kuna msiba tena mziito, lakini yeye hajali na badala yake anaendelea na mipango yake anayoijua kichwani.

Swali kwa watznania wenzangu, tunahitaji miujiza gani ili kupata viongozi watakaotuoa hap tulipo na kutufikisha pahala penye matumaini?

Yawezekana kuwa nawe yapo yanayokukera, siyo vibaya tukakumbushana.
 
Na kerwa na uongo wa viongozi
Kikwete muongo
Bilali muongo
Pinda muongo
Anne Makinda muongo
Kinana muongo
wasira muongo
Muhongo -Muongo
Viongozi wote Mkuu wa jeshi la polisi muongo,duh
 
Nakerwa na Haya maigizo ya kisiasa hapa nchini!!!!
 
Na kerwa na uongo wa viongozi
Kikwete muongo
Bilali muongo
Pinda muongo
Anne Makinda muongo
Kinana muongo
wasira muongo
Muhongo -Muongo
Viongozi wote Mkuu wa jeshi la polisi muongo,duh

Mbaya kuliko zote ni kutumia advantage ya watanznaia wengi kutokuujua ukweli ili waendelee kutufanyia dhihaka. Hili linahitaji Mungu au watanznia kuamka? Polisi ndo usiseme, ni waongo kwa niaba ya bwana wao.
 
watu8 kuna mtu anatumia avatar yako RIGHT prohibited?
 
Last edited by a moderator:
11. Kiongozi anayehalalisha mateso na mauaji ya raia wake kwa sababu tu ya kupingwa
12. Kiongozi anayehalalisha kutengeneza mazingira ya lawama kwa watu wasio na hatia kwa kuwa tu wanampinga
13. Kiongozi anayehalalisha Bunge kuwa la kikandamizaji ya hoja kwa sababu tu ni za wapinzani.
Huyu ni kilaza anayetafuta kumwaga damu ili aendelee kutawala. NI LAZIMA ATOKOMEZWE!!
 
SASA BASI NINA MAMBO 10 YANAYNIKERA KAMA IFUATAVYO:
1. Kiongozi anapokwepa kushindwa kwake kazi na badala yake anasingizia walioko chini yake kuwa hawamsaidii ilhali yeye ndiye aliyewaweka.

Yawezekana kuwa nawe yapo yanayokukera, siyo vibaya tukakumbushana.

Hapo kwenye red panachefua zaidi
 
kama inakukera vyakutosha., usi ishie kuandika hapa tu., tafuta sera za vyama kadhaa zisome., chukua maamuzi., tafuta kadi ya chama unachokiona kina endana na mabadiliko unayo ya hitaji., halafu ingia katika mapambano., tulikomboe taifa letu!., hii inataka kazi., sio maneno tu.,

ukiniuliza ushauri nitakujibu - ingia chadema! vaa gwanda., tuko vitani.
 
1. Kiongozi asiyetii mamlaka halali za kisheria
2. Kiongozi anayetumia kutokujua kwa wananchi kufanya na kutangaza anayoyajua na anayoyataka yeye na wafuasi wake tena kwa kutumia damu, madonda, kufukuzwa vyuo kukipaisha chama chake. Hii niseme ni kucheza na hisia za watu.
3. Kiongozi anayeahidi maziwa na asali kwa wananchi wote
4. Kiongozi anayeaminisha wananchi kuwa bila baandamano na kurushia mawe, kutukana na kupigana na wafuasi wa vyama vingine haki haitapatikana
5. Kiongozi anayedanganya umma kuwa anayeonekana kwenye video si Lwakatare ilihali Lwakatare anakiri ndiye ila sauti si yake
6. Kiongozi anaye aminisha watu akiingia madarakani na chama chake wasipotimiza wajibu basi waondolewe kwa maandamano
7. Kiongozi anayewadanganya wabunge wasihojiwe ilihali yeye si mbunge wala mwanasheria na wakati huohuo mwanasheria wa chama ameshahojiwa
8. Kiongozi anayehatarisha amani ya nchi wakati wa uchaguzi kwa kusema malori ya kura yamekamatwa na wafuasi wake huko mbeya alipoulizwa ukweli wa hayo anasema alikuwa anawatest wezi wa kura
9. Kiongozi anayelalamika kila siku kuwa anafuatiliwa ili kutafuta huruma ya nguvu ya umma
10. Kiongozi asiye na mvuto wa kiongozi zaidi ya mvuto wa kibabe na kidikteta
11. Kiongozi mwenye haiba ya ujanjaujanja
12. Kiongozi asiye na sera zaidi ya ufisadi wa chama fulani kinachomsumbua asiingie madarakani
13. Kiongozi anayekurupuka na kuropoka bila kuona matokeo yaliyofichika hasa katika kukiua chama changu
14. Kiongozi asiyesikia ushauri wowote toka ukanda fulani wa nchi au dini fulani.
15. Kiongozi ayefurahia matatizo ya nchi na kuyatumia kama ndiyo sera za kukipaisha chama. Yaani nchi inapoangamia ndiyo furaha yake.
16. Kiongozi asiyetoa mafunzo au waraka wa namna nchi itasonga mbele kuhofia nchi ikifanya vizuri basi chama fulani kitaonekana kinafanya kazi nzuri.

Jamani na mimi hizi ndiyo kero zinazonisumbua kwa kiongozi wangu
 
Ndugu zangu. utaratibu wa ufanyaji kazi ni mgumu sana. Unaweza kuwa Rais lakini ni kweli kama wa chini wako hawawajibiki ipasavyo watakuangusha tu. Wengine watasema si awafukuze? Kuna taratibu za kuajiri na kufukuza. Kwa mawaziri ni sawa wanaweza kufukuzwa lakini waajiriwa wengine ni lazima taratibu zifuatwe vinginevyo serikali ikishtakiwa kwa kufukuza watu kiholela italipa fedha nyingi. Kwa waelewa wa mambo ndo maana wanalalamikia mfumo wa uongozi kwa ujumla si suala la rais. Na kubadili mfumo ni lazima wananchi ndo wafanye maamuzi magumu. Kwasababu ubovu wa uongozi unaanzia chini kabisa kwenye mashina.Wengine wanafanya mambo ya ajabu kwa kuzingizia wametumwa na rais. Nchi tulishafikia hata Mbunge anafunga shule! Jamani.
 
1. Kiongozi asiyetii mamlaka halali za kisheria
2. Kiongozi anayetumia kutokujua kwa wananchi kufanya na kutangaza anayoyajua na anayoyataka yeye na wafuasi wake tena kwa kutumia damu, madonda, kufukuzwa vyuo kukipaisha chama chake. Hii niseme ni kucheza na hisia za watu.
3. Kiongozi anayeahidi maziwa na asali kwa wananchi wote
4. Kiongozi anayeaminisha wananchi kuwa bila baandamano na kurushia mawe, kutukana na kupigana na wafuasi wa vyama vingine haki haitapatikana
5. Kiongozi anayedanganya umma kuwa anayeonekana kwenye video si Lwakatare ilihali Lwakatare anakiri ndiye ila sauti si yake
6. Kiongozi anaye aminisha watu akiingia madarakani na chama chake wasipotimiza wajibu basi waondolewe kwa maandamano
7. Kiongozi anayewadanganya wabunge wasihojiwe ilihali yeye si mbunge wala mwanasheria na wakati huohuo mwanasheria wa chama ameshahojiwa
8. Kiongozi anayehatarisha amani ya nchi wakati wa uchaguzi kwa kusema malori ya kura yamekamatwa na wafuasi wake huko mbeya alipoulizwa ukweli wa hayo anasema alikuwa anawatest wezi wa kura
9. Kiongozi anayelalamika kila siku kuwa anafuatiliwa ili kutafuta huruma ya nguvu ya umma
10. Kiongozi asiye na mvuto wa kiongozi zaidi ya mvuto wa kibabe na kidikteta
11. Kiongozi mwenye haiba ya ujanjaujanja
12. Kiongozi asiye na sera zaidi ya ufisadi wa chama fulani kinachomsumbua asiingie madarakani
13. Kiongozi anayekurupuka na kuropoka bila kuona matokeo yaliyofichika hasa katika kukiua chama changu
14. Kiongozi asiyesikia ushauri wowote toka ukanda fulani wa nchi au dini fulani.
15. Kiongozi ayefurahia matatizo ya nchi na kuyatumia kama ndiyo sera za kukipaisha chama. Yaani nchi inapoangamia ndiyo furaha yake.
16. Kiongozi asiyetoa mafunzo au waraka wa namna nchi itasonga mbele kuhofia nchi ikifanya vizuri basi chama fulani kitaonekana kinafanya kazi nzuri.

Jamani na mimi hizi ndiyo kero zinazonisumbua kwa kiongozi wangu

wewe huna issue unatafutia watu wapigwe ban humu jamvini, wana jamvi wenzangu tumuache huyu hajui alisemalo, masaburi kabisa huyu gamba
 
Kiongozi ambaye mwanae anauza unga

Tatizo sio kiongozi bali wananchi wasiojua nini maana ya maendeleo.
Wakiadiwa maisha bora kwa kila Mtanzania na hawayaoni wao ni sawa tu, kwani hata huo msamiati wa maisha bora hawaujui.
Watu ambao wako tayari kutetea uozo wa vingozi kwa sababu tu wapo madarakani.
Watu wanao amini propaganda bila kujua kwa nini propaganda zimekuwepo.
Watu wasijua kulinganisha maendeleo ya wengine na ya kwao.
Watu wanao ona kila kitu ni sawa tu kwao kiwe kibaya ama kizuri hajui kuchuja.
Watu wasiofahamu kuwa wameletwa duniani kwa faida na si kuja kuabudu Binadamu wenzao.
Watu wasio amini juu ya uwezo wao wenyewe hata wakidanganywa vipi wanakubali tu kwa sababu hawaoni mbadala wa anayewadanganya.
Watu wanao uona ukweli lakini wanalazimisha akili zao kutokuuona.
Watu wasiojibu hoja zaidi ya matusi na kufuatilia maisha ya watu binafsi.
Watu wanao amini kila wanachodanywa na kukifanya sera ya maisha yao.
 
Back
Top Bottom