Inakanganya. . . . . . !!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inakanganya. . . . . . !!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Apr 25, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Sio kila jambo ni la kushea,binadamu tuna marafiki,wazazi na ndugu,wote hawa kila kukicha tunasema tunawapenda lakini linapokuja suala la mapenzi hapo tunataka tuwe wenyewe tu. Japokua zipo imani na mila zinaruhusu mahusiano ya kindoa kuwa na mke zaidi ya mmoja maumbile bado yanakua kinyume na ruksa hii, yanasimama peke yake, mwanadamu hataki kuwa na penzi la kushea na mwanadamu mwenzake.Lakini pia katika mahali ambapo mwanadamu anaonekana mnafki na mwenye choyo ni eneo hili.

  Ni mnafiki kwa sababu mwenzi wake anataka awe wake yeye tu lakini yeye akitaka awe na mahusiano mengi.Jambo hili ni kwa jinsia zote.Lakini pamoja na kuwa na mahusiano na wapenzi wengi bado mwanadamu hatosheki, ruhusa ya kuwa na wake wa 4 imeshindwa kumsaidia mwanaume, "maendeleo" ya kuanza ngono kwa idadi ya wapenzi unaotaka ukitosheka ufunge ndoa nayo imeshindikana,sasa zimekuja ndoa za mikataba unaweza kuoa/kuolewa leo na ndoa ya mkataba wa wiki moja baada ya hapo unakua huru.

  Mwanadamu hana tofauti na mbuzi ambae anampanda mama yake!Mi napata wasiwasi kama huyu mwanadamu ndo yule alieumbwa mwenye mfano wa Mungu.Mi nadhani ni wakati muafaka wa kujiuliza,hivi wanawake wote au wanaume wote niliofanya nao ngono nimefaidika na nini?Je huu ni ubinadamu kweli?

  ..Kama kweli tunataka furaha ya kweli tuache unafiki na tujitazame bila kujipendelea kisha tubadilike.Kuna watu wameshafanya ngono na wanaume au wanawake ukiwakusanya wanajaa basi nne.Ukimuangalia alichopata cha maana hakuna zaidi ya umaskini mkubwa!
   
 2. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mkuu lipi limekukuta leo,maana......
   
 3. HOPECOMFORT

  HOPECOMFORT JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 2,784
  Likes Received: 3,519
  Trophy Points: 280
  Sio bure kuna lililomkuta kweli!! Na chanzo sio kingine bali yule alombwagia moyo.
   
 4. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  yamekukuta nn? komaa acha kulalama
   
 5. J

  JOJEETA Senior Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli umenena la maana sana,tho hujabase upande mmja bt hili tatizo lipo kwa wanaume zaidi.nina anko wangu ana wake w4 wa ndoa,wa nje hawahesabiki till nw ana umri wa kama miaka 60 bt bado ana vitoto vidogo ambavyo vipo sawa na vi2kuu vyake.ifike wakati wa2 watambue kua,kua na mke au mume mmoja ni ujanja na cio ushamba.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  mapenzi yanaumiza kichwa.....
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo . . .
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe Chief, tunatakiwa kuishi kama binadamu wa kweli wenye utu, na siyo kama wanyama ambao wakiona chochote mbele yao wanadandia.
  Asante kwa hoja nzuri.
   
 9. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Nimependa hoja yako ubarikiwe sana lakini kuna wengine ni kama unampigia mbuzi gitaa,anasoma anayaacha hapo hapo na akitoka anaenda kurudia kosa,ndo binadamu tulivyo..
   
 10. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena! So sad kuwa ktk generation hii mambo ya kishamba yanaitwa ya kijanja na ya kijanja yanaitwa ya kishamba!
  Kisimu changu hapa hakina option ya 'Like'...!!
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Sio lazima linikute lolote ndugu yangu!
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Akili hizi za aina gani?Hivi mtu akisema jambo mpaka liwe limemfika?Hebu jaribuni kujadili mada na msingi wake msijadili kitu kisichokuwepo!
   
Loading...