Inahitaji akili kidogo, kufikiri na kuamua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inahitaji akili kidogo, kufikiri na kuamua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masauni, Sep 10, 2010.

 1. M

  Masauni JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninapenda kuongea na mashabiki wa CCM. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana hasa ni nini CCM INACHOTAFUTA? Nimefahamu na kugundua kuwa CCM inachotafuta ni ulaji tu na sio kweli kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli. Kama kweli CCM ni chama cha watu wote na kinawajali wanyonge wasingeweza kufanya yafuatayo
  • Kutumia kila aina ya mbinu kuhakikisha Dr. Slaa haonekani katika vyombo vya habari,wala kusikika, Hivyo kuwanyima haki wananchi kuwasikiliza wagombea na kuamua wampe nani kura. Kama CCM wanaamini sera zao ni nzuri kwa nini wanazuia sera za mwingine ambaye wanasema sio nzuri kujulikana kwa wananchi? Katika hilo mtanzania huitaji ushabiki inahitaji akili kidogo tu kufikiri na kujua yupi bora
  • CCM wamekataa midahalo, Kama CCM mna amini wagombea wenu ni safi na makini kuanzia raisi mpaka wabunge kwa nini muogope kuulizwa maswali na wananchi, ambao mnasema mnawapenda na kuwajali? na pia kwa nini mnaogopa kuwekwa pamoja na wapinzani wenu ambao mnawaita wadhaifu , hawana uwezo wa kuongoza !Katika hilo haitaji ushabiki, unahitaji akili ndogo tu kufikiri na kujua yupi bora.
  • CCM kwa nini mnakumbatia ushirikina(refer statement za sheikh yahya) kama kweli mnawajali wananchi, kwa nini kutafuta kura kwa ushirikina. Kama mna amini sera na mambo yenu wananchi wanayakubali. katika hilo huitaji ushabiki, inahitaji akili ndogo sana kufikiri yupi bora.
  • Ufisadi ndo hamtaki kabisa kuongelewa, kama ufisadi wa CCM si kweli kwa nini mnatumia nguvu kuhakikisha watu hawaongelei ufisadi? Mwana CCM huitaji ushabiki katika hilo, INAHITAJI AKILI NDOGO SANA NA UZALENDO WA KWELI KUAMUA NANI NI KIONGOZI ANAYETAKIWA KUONGOZA TAIFA LETU.
   
 2. D

  Dopas JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Umenena mkuu. Natamani nakala ya hii imfikie Makamba, na hata JK, hata kama watatupa kwenye trush bin. Lakini ipo siku ukweli utajiwekea huru ambapo hao na ushirikina wao wataumbuka.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  MKOMBOZI WA KARNE!
  Chagua mabadiliko!

  CCM.....
  Wanakula hawashibi!
  Wanakula wanavimbiwa!
  Wanakula wanasaza!
  Wanakula bila kunawa!
  Wanakula huku wanatukana
  Wanakula huku wanapuliza!
  Wanakula huku wanatoa hewa!...uhuuuufff!
   
 4. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,399
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Brilliant!!!!!!!
   
 5. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Na pia haihitaji akili nyingi kuelewa kuwa mleta hii thread uelewa wake ni mdogo. hivi unamaanisha nini unaposema slaa hapewi nafasi kwenye vyombo vya habari? kwani yeye ni nani mpaka awe spesho wakupewa nafasi zaidi ya wengine? Kikwete mwenyewe pamoja na kuwa bado ni rais bado anapewa nafasi sawa na wengine, au nyinyi watu wa chadema mlitakaje? Mara sheikh yahaya, kwani huyu anaingieje humu? Shame thread, na kweli INAHITAJI AKILI KIDOGO KUFIKIRIA NA KUAMUA thread zisizokuwa na mbele wala nyuma kama hii.
   
 6. M

  Masauni JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe nadhani uelewa wako bado, sijasema slaa apewe nafasi zaidi ya wengine ninachosema kwa nini CCM wanamminya katika vyombo vya habari. Wewe hujasoma au kusikia alichosema sheikh yahaya? Pole ndugu yangu uenda CCM washakuloga
   
 7. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #7
  Sep 10, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pole sana ndg yangu, moyo wangu unalia na kusikitika juu ya ujinga wa ubongo wako, shame on you man.!
   
 8. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #8
  Sep 10, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,399
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  You have to be forgiven and then forgotten, as you're not thinking properly!!
   
 9. S

  Safre JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo vijana hatujajua mabadiliko ya kwel maana tunafata wazazi na ccm yao maana tunaletewa hadi kadi za ccm nyumban
   
 10. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mashabiki wakubwa wa CCM ni vijana, wale niliowategemea wawe wanamapinduzi! Mavijana ya siku hizi ni maconservative, na hii inaleta shida, na CCM wametumia hii bahati mbaya ya historia kuwarubuni, na kama unakumbuka ule msururu wa vijana wa chuo kikuu pale uwanjani wakati wanazindua kampeni. Sintashangaa sana huyu aliyejionyesha ujinga wake hapo kuwa ni kijana. Iko kazi kweli.

  Nimeipenda sana mada hii kama ilivyowasilishwa imetulia safi sana
   
Loading...