Inachanganya sana, kupata mimba sababu ya kuzini, anaogopa kutoa eti ni dhambi

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
Kuna mjadala mgumu sana kuhusu uhalali wa kutoa mimba au Kuto itoa.
Hoja za wengi wanaosema isitolewe ni za kidini wengi husema kuua ni dhambi. Sawa lakini swali la msingi ni hili hapa. Uzinzi ni dhambi kubwa kuliko zote. Mtu amezini na kupata mimba, anaogopaje kutoa kwa kuogopa dhambi hiyo hiyo?

Lakini pia lipo swali la msingi sana hapa. Je ni wakati gani kiumbe kinakuwa na haki.
Mtoto wa shule napata mimba, na shule itaisha na hapo haruhusiwi kurudi tena na inamaanisha maisha yake Dah! Hayatakuwa na matarajio ya elimu. Je ni sahihi huyu mtu kuleta mtoto atayekuwa kwenye mazingira ya kifukara kutokana na mama kushindwa shule?.
Je ni sahihi kutoa mimba katika mazingira fulani?
Kumzuia mtu kutoa mimba wakati anataka sio kuingilia uhuru wake? Maana yeye ndiye anayetoa malezi kwa mtoto ndani. Je kumlazimisha kukaa naye wakati hamtaki ni sahihi kwa afya ya mama na mtoto.

Naamini dhambi ni dhambi. Kuzini na kuua sehemu ni moja siku ya kiama
 
Ni sawa tu na kuogopa hangover wakati hauogopi pombe

Unaogopa ukimwi wakati unagongwa/gongwa peku
 
Mjadala wa utoaji mimba usijirudie....maana shetani anatumia mwanya huo huo kuualalisha. Kutoa mimba Ni kuua.
Heri nusu Shari kuliko Shari kamili
 
ukitenda dhambi moja hamna ulazima wa kuenda nyngne, acha aishie kwenye kuzini asiue
 
MKUU inakushangaza kidini ama kimtazamo wa kibinadamu ambaye haongozwi na dini?

Kwa sababu tukianzia kimtizamo wa kibinadamu ambaye anaongozwa na mawazo yake mwenyewe kwa maana dini kaiweka kando yeye hujiamulia kila jambo basi tunasema hata kuua mtu mzima aue tu kwa kuwa nafsi yake haiongozwi na imani yeyote ile na hata hilo analotaka kulifanya halina tabu na ana uhuru nao kwa kuwa hana imani inayomuongoza.

Ama kidini mkuu hilo sulala ni dhambi kubwa kwa sababu.

1.kuzini ni dhambi kubwa sawa na imeleta matokeo ya mtoto (mimba) sasa kutaka kutoa ataka azini tena ama?

Kwa sababu ameshafanya dhambi kubwa ya kuzini na kama kajutia tayari kwamba kafanya dhambi kwa mungu vipi ajiongezee dhambi ya pili ya kuua ?

Huoni kama anaongeza dhambi hapo mkuu?..kwa sababu hapo kawaida ya dhambi ni ukifanya huwa inazalisha dhambi ingine mfano..

Kama huyo kazini(dhambi)kapata mimba sasa anataka kuua kiumbe cha tumboni(nayo dhambi ilotokana na zinaa)sasa akikataa kutoa mkuu itakuwa ni sababu kubwa ya kutozalisha dhambi ingine kutokana na dhambi moja.

Hata mtu akifanya dhambi ya kulewa basi atataka afanye na dhambi ya kutukana ama kuzini,kwa hvyo dhambi huzalisha dhambi ila mtu ukishafanya ukajua hili ni kosa basi hamna haja ya kuendelea kuzalisha dhambi..

Hvyo huyo alee mimba yake na asitoe kwani kuilea ni katika alama za kuonyesha hataki kurudia kosa tena....

Haya maisha tunapita...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom