Ina maana wachumi hakuna Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ina maana wachumi hakuna Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shark, Jul 23, 2011.

 1. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,121
  Likes Received: 7,372
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Tanzania tumeishiwa kabisa watu wenye akili au ni masihara ya kuwaachia viongozi wawe ndio waamuzi wetu, maana nchi ni kama haina wataalam na wachumi kabisa wa kuweza kutuongoza au kututengenezea system ya maendeleo, eti leo hatuna umeme kisa maji yamekwisha kule mtera na maeneo kwan hakuna vyanzo vingine vya umeme mpaka tujikite kwenye maji tu mbona kuna nchi hazina mabwawa wala mito lakini hazijawai kukatikiwa na umeme maisha yao yote? ok tuna uranium mbona hakuna mwenye akili ambae kajaribu kutuambia tuichanganye na nini ili tupate umeme wa uhakika? sio lazma kitu hicho aseme mnyika hata sisi tunaweza bana. sio kwenye umeme karibu kila sekta inahitaji marekebisho ili tuendelee na wachumi wetu mnatakiwa mjitume sio kukaa na kujiita wachumi wakati huna hata moja ulilolifanya
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wapo wachumi wa vyuo vikuu vya kata
   
 3. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  unaposikia system imeoza huwa unafikiri ipi??..kifupi hapa kwetu hakuna anayefanya kazi kwa taaluma yake...yaan ni madudu tu...kuanzia karani mpaka huko juu...hawa wachumi..wanasheria..wanasiasa wote..uozo..hapa tupate dictatorship style..may be..tunaweza kubadilika
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tatizo sio hilo la kuwa na wachumi swala ni kwamba bongo kila kitu tunasubiri wanasiasa waamue na utakuta wao wako kimasilahi zaidi ndo maana wanafanya vitu vya kufikirika zaidi..
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kudos mzee pumbatupu
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Uwekezaji wa umeme unahitaji muda, fedha na mipango ya muda mrefu. Hata kama tuna uranium, usidhani kuwa kila kitu kinaweza kufanyika kwa siku moja tu. Isitoshe, matatizo ya umeme yamnakumba karibu eneo lote la nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na si Tanzania tu. Hata Lusaka juzi wamekatiwa umeme. Tuwe wavumilivu na siyo walalamivu
   
 7. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,121
  Likes Received: 7,372
  Trophy Points: 280
  ni kweli kabisa utakuta eti hata mwaanasheria kamaliza chuo anataka akajishikize kwenye kampuni fulani ya uwakili ndo atoke lakn anashindwa kuwa mbunifu wa kwenda kule kwenye magereza kuna ksei nyingi tu watu wameonewa na kuwasaidia utajulikana, unakuta mchumi anashindwa kutuambia kwa nini shilingi yetu inadondoka na tufanyaje tuweze kujiokoa hii ni ajabu kabisa.
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Sir, mbona hata rais wa hii nchi ni mchumi, mambo yake si unayaona mwenyewe?
   
 9. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu wachumi wapo tena waliobobea, na sio wachumi tu hata wataalamu wengine nao wapo. Tatizo la nchi hii ni kuwa watu hawa hawasikilizwi, na serikali yetu haijali professionalism.

  Vilevile maslahi yao ni duni na ndio maana wanaikimbia nchi hii (brain drain) au wanaingia kwenye siasa (kwa sababu wanaona kunalipa). Sasa ukichanganya politics na utaalam ndio balaa zaidi
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Huwezi kufikiri umeme wa Nuclear wakati umeshindwa kumanage thermal na hydro. Hakuna excuse kuwa management ya supply ya umeme inahitaji fedha na mipango ya muda mrefu. Kuchange mentality kutoka uswahili na kuingia kwenye professioanlism kunahitaji siku moja tu, tukiacha blaa blaa umeme utakuwepo 24/7. Tanzania ina raslimali za kuto9sha kuweza kusupply umeme 24/7, ukiangalia matumizi ya umeme per population utaona kuwa ni kidogo sana, na ni managable.


  Let us be honest first. Ni uzembe tu (corruption, mismanagament na kupoliticize professions za watu) ndio unafanya Tanzania iwe na mgao wa mara kw amara na isiwe na umeme wa uhakika, si ukame, si kupanda kwa bei ya petroli. Kama unaweza kukumbuka vizuri tatizo hili limeanza hasa baada ya serikali hii kuingia 2005. Do not tell kuwa tangu JK ameingia ndio ukame umekuwa mkubwa sana.
   
 11. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Ukitaka kujua bongo masuala ya uchumi sio ishu yetu tupia thread katika jukwaa la uchumi uone jinsi itakavyopitiwa na watu wachache, lakini ukitupia thread jukwaa la siasa ni balaa. Hata iwe na kichwa cha habari kinachomtaja mjinga Nape watu wataishindia wakati za uchumi zinadorora. Kiukweli tatizo la umeme wa nchi hii sio mvua wala ukame, ni uwekezaji kidogo pamoja na uwekezaji wenye mitazamo ya kifisadi. Mtera ilijengwa kukidhi mahitaji ya miaka ya 70, tunahitaji kujenga chanzo cha umeme wa maji kukidhi mahitaji ya sasa na ni uwekezaji wa 2 billion dollars, ambazo nchi yetu inamudu. Lakini Kikwete na wenzie wanazuia uwekezaji huo ili waendelee kufanya biashara kupitia mgao wa umeme. Tatizo la umeme sio wachumi wala fedha, bali linatokana na Jakaya Mrisho Kikwete.
   
 12. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  We jamaa ni mkurya mjinga sana... Uwekezaji unahitaji muda gani zaidi ya huu wa miaka 50 uhuru, unataka hadi miaka 100 ya uhuru ndio useme muda unatosha? Fedha nchi hii inazo mnaishia kugawana posho kila siku mnashindwa kutenga fedha za kutosha. Mipango ipo ya muda mfupi na mrefu. Tanesco wanayo Master Plan ya kuzalisha umeme tokea miaka ya sabini hadi leo haifuatwi, we unataka mipango gani zaidi ya hiyo. Kama wewe ni kilaza unakubali kila unachodanganywa na magamba wenzie tulia mdanganyane na mkeo nyumbani sio kutuletea huo uongo hapa. Watu tunajua kuwa uwekezaji mkubwa wa umeme unahitaji serikali kushirikiana na sekta binafsi na wawekezaji wa uhakika wa umeme wameishakuja hapa nchini lakini wananyimwa ushirikiano kwa kuwa kuna watu wanajua mgao wa umeme kwao ni dili, hasa JK. Bila kuingia mtaani kama Malawi hili tatizo halitaisha.
   
 13. Researcher

  Researcher Senior Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Akina Prof. Ndulu walikuwa wanafundisha Oxford, Wakina Mpango wamekuwa senior economists benki ya dunia kwa miaka mingi tu. Mungu atupe nini zaidi?
   
 14. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania amna wachumi, mfano mdogo angalia bajeti za nchi wanakanganya tu. amna kinachoeleweka, kuhusu umeme tatizo ni
  watendaji wameweka maslahi yao binafsi mbele kuliko ya taifa. wakati hata kwa muda wa mwezi mmoja tatizo la umeme tunaweza
  kulisahau kabisa Tanzania. Lazima twende kwa wakati na wala wasisingizie maji. Kuna gas, umeme wa kutumia jua pamoja na
  wa kutumia upepo. sasa tatizo lililokuwapo vichwani mwao ni nini nashindwa kuelewa.
   
 15. P

  Peter bedson Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suluhisho tukaichukue inchi yetu pale magogoni inchi imeoza hakuna wachumi hapa mnashindwa na kinchi kidogo cha comoro, "pesa yake ina nguvu, faranga 50 sawa na uero 1
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kiongozi nimekusoma mara 3 kupata logic yako! Una uchungu kama mchungaji hapa! Tanzania ina wachumi wa nyanja zote shida serikali ina raisi kilaza ambaye kila kitu amebinafsisha na siasa. Jamaa kwa kujua ni kilaza basi humjaza ujinga kwa kumsifia kwa mambo anayopenda kusikia. Ndipo hapa tulipo.Hebu fikiria Inflation ipo kwenye region ya 17% mishahara imepanda kwa 3% wajinga wameshangilia. UK kwenye reccesion waliongeza mishahara kwa 4% na walishusha VAT kuongeza unafuu kwa raia. Tanzania raisi wenu anazungumza kama Zombie eti yeye si mawingu hawezi nyesha kwenye mabwawa! Thats very low na Mukama na Nnape wako busy kuandaa wandamanaji kupongeza hilo. Tunatatizo kubwa sana kama taifa tumepoteza patrotism aloijenga Nyerere kwa miaka mingi. Kila mtu anazungumzia kupiga dili, rushwa ni sehemu ya job description serikalini...leo hii nipatie 100 Mil nitafanya kipaimara cha mtoto wangu kwenye viwanja vya Ikulu na Jakaya atakuwepo.

  We need to stand up with the same spirit kama taifa! Imetosha mafisadi waondoke, lakini nao wananjia zao za kudumu, kudanyanya amani na utulivu, Kuleta mgawanyo wa kidini, Islam na Christians, ili waendelee kunyonya. Lakini wewe na mimi tukisimama kwenye ukweli na kuhoji ninaamini wale vilaza waliobungeni wataamka na kusingizia kulala kwao kutaisha. Umeme ni aibu ya mwaka Jakaya anajisifia historia ya ujinga wake
   
 17. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,121
  Likes Received: 7,372
  Trophy Points: 280
  Kaka hapa hata ukiamua kufikiria matatizo ya nchi hii utaumiza kichwa chako bure tu.
  Kuna jamaa kataja sifa za ndulu hapo juu, na ndio anaotuongozea BOT na hela yetu ndo hiyo inazidi kushuka thamani.
  Ukweli kila mahali kumeambukizwa virusi vya CHUKUA CHAKO MAPEMA ambavyo ni virusi vibaya kuliko hata VVU
   
 18. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Je, unaweza kuishauri serikali ya kj ikakuelewa pamoja na utaalamu wako huo? Wana uchumi wapo wengi ila wameamua kuendelea tu na mambo yao!
   
 19. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Nchi ina wataalamu wengi tu tena top class.


  Tatizo letu kama nchi ni kubwa na ambalo limeota mizizi...mfumo na muundo mzima wa ufanyaji kazi serikalini. Kwa kifupi kwa utaratibu wetu uwezi tofautisha wanasiasa wanaishia wapi ktk kazi zao na watalaamu wanaanzia wapi..mbaya zaidi wenye sauti ni wanasiasa.

  Kiongozi mkuu wa wizara ni mwanasiasa sio mtaalamu husika na wizara, maamuzi yake ni ya mwisho na si lazima yaendane na utaalamu husika.

  Nilidokeza hapo juu kuwa mifumo yetu ya utendaji imekaa kisiasa zaidi badala ya kuwa kitaalamu. Kwa maana nyingine ni kuwa kama mtu anafanya kazi yake kitaalamu ni lazima utacross path na wanasiasa yaani utaonekana wazi kuwa hufai. Kwa kulitambua hilo nafasi zote muhimu kiutendaji kutokana na mfumo huu mufilisi zimeshikwa na wanasiasa mfano kina Jairo na wengine.

  Nimalize kwa kusema shida kubwa tuliyonayo ni mfumo na muundo wa utawala serikalini kwa ilivyo sasa hivi kwa mfano kama kuna Waziri ana jambo zuri labda kalipata wizarani toka kwa wataamu say wa uchumi wazo hilo halitaweza kufanyiwa kazi mpaka lipitie mchakato mrefu sana wa kisiasa (siyo wa kitaalamu) kabla ya kuaafikiwa...utasikia inter ministerial committee, muswaada, etc sasa chances ni kwamba kama issue yenyewe inalenga wananchi zaidi na si viongozi kama zilivyo issue za madini basi hilo jamboo litapigwa chini mapema tu.

  Kwa hiyo wataalamu wapo lakini ili wafanye kazi lazima kuwepo na mazingira sahihi (ikiwemo kipato kizuri) vinginevyo ni kama tunavyoshuhudia namna technical people (drs, wahadhiri, accountants, wanavyokimbilia siasa...ubunge, uwaziri etc (note kuna sehemu ndogo sana ya wataalamu ambao wanahisi kuwa hawana sehemu ya kusikilizwa mawazo zaidi ya Bungeni)
   
Loading...