In my view, Prof. Lipumba hana cha kupoteza

Mtu mwenye uelewa mdogo hawezi kumuelewa Lipumba,ila kwa sisi wengine tunamuelewa sana Lipumba,huwezi kukaa na kumsafisha mwizi hata siku moja..sema tatizo kubwa ni pale watanzani wengi wanaendeshwa na wanasiasa,hawatumii akili kuwaza bali wanakalilishwa
 
CUF bara ina Mhitaji sana Prof Lipumba kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile

Mtu yeyote alie tazama Mahojiano ya Seif na Clouds Leo atajua kabisa Hilo

Kwake akizungumzia CUF anazungumzia Zanzibar!

Kaulizwa Idadi ya Wanachama wa CUF kwake yeye kaishia kutaja laki mbili na nusu (Idadi ya Znz )

Kaulizwa Ikitokea Hayupo Tena Siasani anadhani kina Nani ni warithi wake kawataja Kina Jussa, Duni, Mazrui, Mansour, haamini Kama kuna Mtanganyika anaweza kuw Kiongozi wa CUF

Sasa wewe unategemea mtanganyika ataenda kugombea urais Zanzibar?
 
CUF bara ina Mhitaji sana Prof Lipumba kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile

Mtu yeyote alie tazama Mahojiano ya Seif na Clouds Leo atajua kabisa Hilo

Kwake akizungumzia CUF anazungumzia Zanzibar!

Kaulizwa Idadi ya Wanachama wa CUF kwake yeye kaishia kutaja laki mbili na nusu (Idadi ya Znz )

Kaulizwa Ikitokea Hayupo Tena Siasani anadhani kina Nani ni warithi wake kawataja Kina Jussa, Duni, Mazrui, Mansour, haamini Kama kuna Mtanganyika anaweza kuw Kiongozi wa CUF
Kwa kupotosha watu ni Magwiji yeye kaulizwa ataje watu ambao wanaweza kumrithi baadae akataja wachache na kusema na wengine wengi tu.....,
 
Maalim seif leo ameeleweka sana. Na kweli ni mwanasiasa maana anajua kuuleza kwa staha yale wanayotakiwa kujua umma. Yaisyotakiwa kujulikana ameyafunika kwa heshima kubwa hii ndio siasa sio dharau,matusi ,kejeli.

Maalima anastahili kabisa kuwa kiongozi anaelewa watu wanataka nini
 
Mtu mwenye uelewa mdogo hawezi kumuelewa Lipumba,ila kwa sisi wengine tunamuelewa sana Lipumba,huwezi kukaa na kumsafisha mwizi hata siku moja..sema tatizo kubwa ni pale watanzani wengi wanaendeshwa na wanasiasa,hawatumii akili kuwaza bali wanakalilishwa
mwenyewe siungi mkono Lowasa kuja UKAWA, ila Lipumba hana nia njema hata chembe, mwanzoni nilidhani ni mtu mwenye msimamo wake kama Slaa pengine, ila nilikuja ku comfirm jamaa anatumika na analindwa na serikali kuvuruga upinzani
 
Profesa Lipumba yuko kazini.
Anapigania kiinua mgongo
Na sharifu hamadi naye ni kivuruge toka agombee urais wa Zanzibar mpaka sasa hakushinda in vyema yeye na Lipumba kukaa pembeni kuliko kutumika na chadema kuua cut bars.
 
Hapo ndio tafsiri ya msomi inapoingia. Sasa anapoamua kuharibu mambo kisa anahisi hana chakupoteza,nini faida ya elimu yake.

Yawezekana asiwe na chakupoteza kisiasa,ila nje na hapo anavingi sana vya kupoteza.
 
mwenyewe siungi mkono Lowasa kuja UKAWA, ila Lipumba hana nia njema hata chembe, mwanzoni nilidhani ni mtu mwenye msimamo wake kama Slaa pengine, ila nilikuja ku comfirm jamaa anatumika na analindwa na serikali kuvuruga upinzani
Lipumba hatumiki broo.sema watu hawaelewi.na Lowasa kuja ukawa sio kosa,ila kosa ni kuwa mgombea.anyway hayo yalishapita
 
Mkuu Lipumba hatumiki? teh....mwanzoni nami nilikuwa na mawazo kama wewe, kwa hiyo ana nia njema na CUF?
 
CUF bara ina Mhitaji sana Prof Lipumba kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile

Mtu yeyote alie tazama Mahojiano ya Seif na Clouds Leo atajua kabisa Hilo

Kwake akizungumzia CUF anazungumzia Zanzibar!

Kaulizwa Idadi ya Wanachama wa CUF kwake yeye kaishia kutaja laki mbili na nusu (Idadi ya Znz )

Kaulizwa Ikitokea Hayupo Tena Siasani anadhani kina Nani ni warithi wake kawataja Kina Jussa, Duni, Mazrui, Mansour, haamini Kama kuna Mtanganyika anaweza kuw Kiongozi wa CUF
Hili swali aliulizwa kwa Zanzibar, rudia clip usikikize upya,
 
Kwa sisi wazaliwa wa Pwani, mtu anayetumika au anayeamua kuvuruga mipango ya wengine humuita Kivuruge. Kivuruge huaribu utaratibu,utulivu na hata mipango. Hata kwenye vyama vya siasa nchini na kwingineko,kuna akina Kivuruge.

Prof. I. H. Lipumba ni msomi,mwanasiasa mbobevu na mchumi nguli. Kama mwanasiasa mwingine awaye,Prof. Lipumba alikuwa kwenye kilele cha kisiasa kwa wakati wake na sasa ameporomoka. Pamoja na kutenda na kusema yote,kwasasa Prof. Lipumba hana cha kupoteza

Katika kilele chake cha kisiasa,Prof. Lipumba amegombea Urais wa Tanzania mara nne: 1995,2000,2005 na 2010. Mara zote hakushinda. Kisiasa,Prof. Lipumba hana uwezo wa kuwa Rais wa Tanzania tena. Naye analijua hilo. Kwa ukongwe na hadhi aliyokuwa nayo,Urais tu ndio ulikuwa wa size yake. Huo umeshindikana na sasa hana cha kupoteza

Kwa matendo yake ya sasa ya ndani ya CUF,namfananisha na mzazi anayeuza mali zake zote na kubugia pesa zake akitaka atakapofariki asiache chochote kwa wanawe na hata mkewe. In my own view,mzazi wa aina hiyo inamuwia vigumu kukwepa kuitwa Kivuruge. Prof. Lipumba anapaswa kuiacha CUF kama alama yake ya kujivunia badala ya kuivuruga kila kukicha.

Tumbo lake ndilo limempumbaza na linaendelea kumpumbaza.Hawezi kukuelewa na hata wafuasi wake hawawezi kukuelewa.

Wanasema wenzetu wa pwani......''Mtoto Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Iddi"
 
Na sharifu hamadi naye ni kivuruge toka agombee urais wa Zanzibar mpaka sasa hakushinda in vyema yeye na Lipumba kukaa pembeni kuliko kutumika na chadema kuua cut bars.
hiyo ndio wish yenu CCM mmechelewa
 
Jina linasadifu kilichomo kichwani mwake, ovyo kweli
 
Back
Top Bottom