Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,300
- 25,920
Kwa sisi wazaliwa wa Pwani, mtu anayetumika au anayeamua kuvuruga mipango ya wengine humuita Kivuruge. Kivuruge huaribu utaratibu,utulivu na hata mipango. Hata kwenye vyama vya siasa nchini na kwingineko,kuna akina Kivuruge.
Prof. I. H. Lipumba ni msomi,mwanasiasa mbobevu na mchumi nguli. Kama mwanasiasa mwingine awaye,Prof. Lipumba alikuwa kwenye kilele cha kisiasa kwa wakati wake na sasa ameporomoka. Pamoja na kutenda na kusema yote,kwasasa Prof. Lipumba hana cha kupoteza
Katika kilele chake cha kisiasa,Prof. Lipumba amegombea Urais wa Tanzania mara nne: 1995,2000,2005 na 2010. Mara zote hakushinda. Kisiasa,Prof. Lipumba hana uwezo wa kuwa Rais wa Tanzania tena. Naye analijua hilo. Kwa ukongwe na hadhi aliyokuwa nayo,Urais tu ndio ulikuwa wa size yake. Huo umeshindikana na sasa hana cha kupoteza
Kwa matendo yake ya sasa ya ndani ya CUF,namfananisha na mzazi anayeuza mali zake zote na kubugia pesa zake akitaka atakapofariki asiache chochote kwa wanawe na hata mkewe. In my own view,mzazi wa aina hiyo inamuwia vigumu kukwepa kuitwa Kivuruge. Prof. Lipumba anapaswa kuiacha CUF kama alama yake ya kujivunia badala ya kuivuruga kila kukicha.