Heri yenu wenye memories za kuogeshwa na mama zenu, mnaokumbuka mlivyotaniana na mama zenu wakati wa utoto wenu.
Binafsi nilitengwa na mama yangu nikiwa na miaka miwili. Sikumwona tena hadi nilipofika kidato cha tano na baadae kidato cha Sita. Nilijengewa mazingira ambayo kumuona ilikuwa ni kufanya wizi wa kiwango cha grade "A".
Baada ya hapo, sikumwona tena, mpaka nilipopata taarifa kwamba alifiriki miezi miwili iliyopita nikiwa najiandaa kwenda kwenye mahafali ya first degree.
Hongereni sana mliopata nafasi kuita mama,,,naye akaitika, mliokesea kisha mama akawafinya kidogo kuwakanya kwa upendo, mliosema mama njaa, akawaletea uji au mlio na kumbukumbu za matukio mbalimbali mkiwa na mama zenu. HERI YENU
Sent using
Jamii Forums mobile app