In a dilemma: mke wangu ananishauri nimuoe rafiki yake

In a dilemma: mke wangu ananishauri nimuoe rafiki yake

Sembinga

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2014
Posts
393
Reaction score
345
Habari za wakati huu great thinkers.

Takribani miaka kumi na mbili sasa katika ndoa yetu na tumefanikiwa kupata watoto wawili wote wa kiume. Mke wangu ana rafiki yake wa muda mrefu sana (mchepuko wangu) tangu wakiishi udogoni na kusoma wote huko shinyanga ingawa wametofautiana miaka kama minne hivi (huyo rafiki ndio mkubwa kwa wife ila mdogo kwangu).

Siku ya jumatatu hii iliyopita (18-08-2014) baada ya kupata chakula cha jioni na watoto kwenda kulala ndipo akanijia na hiyo "surprise" ambayo sitasahau maishani mwangu. Aliniambia kama ninaweza nimuoe tu huyo rafiki yake maana ana miaka takriban 34 sasa, na ni "bila bila"(kakosa mume).

Kwa kuwa sisi watu wa mkoa wa Mara kimila tunaruhusiwa ata wake wanne, hivyo kumuweka ndani itakuwa nimempunguzia aibu ya kukosa mume huyo mwanamke waliyeshibana sana, sasa machale yamenicheza, naona kama wife ameshtukia "issue ya kuchepuka" sasa kanitega aniingize kingi.

Najiuliza sijui ni mpe jibu gani wife aisee, naombeni busara wakuu wenzangu maanake naona kama "nimekamatika vile"

cc:matola, miss chagga:
 
(NOTE: INAWEZA KUKOSA MTIRIRIKO MZURI) HABARI ZA WAKATI HUU GREAT THINKERS. NI TAKRIBAN MIAKA KUMI NA MBILI SASA KATIKA NDOA YETU NA TUMEFANIKIWA KUPATA WATOTO WAWILI WOTE WA KIUME. MKE WANGU ANA RAFIKI YAKE WA MUDA MREFU SANA (MCHEPUKO WANGU) TANGU WAKIISHI UDOGONI NA KUSOMA WOTE HUKO SHINYANGA INGAWA WAMETOFAUTIANA MIAKA KAMA MINNE HIVI (HUYO RAFIKI NDIO MKUBWA KWA WIFE ILA MDOGO KWANGU). SIKU YA JUMATATU HII ILIYOPITA (18-08-2014) BAADA YA KUPATA CHAKULA CHA JIONI NA WATOTO KWENDA KULALA NDIPO AKANIJIA NA HIYO "SURPRISE" AMBAYO SITASAHAU MAISHANI MWANGU. ALINIAMBIA KAMA NINAWEZA NIMUOE TU HUYO RAFIKI YAKE MAANA ANA MIAKA TAKRIBAN 34 SASA, NA NI "BILA BILA"(KAKOSA MUME). NA KWA KUWA SISI WATU WA MKOA WA MARA KIMILA TUNARUHUSIWA ATA WAKE WANNE, HIVYO KUMUWEKA NDANI ITAKUWA NIMEMPUNGUZIA AIBU YA KUKOSA MUME HUYO MWANAMKE WALIYESHIBANA SANA..SASA MACHALE YAMENICHEZA, NAONA KAMA WIFE AMESHTUKIA "ISSUE YA KUCHEPUKA" SASA KANITENGA ANIINGIZE KINGI..NAJIULIZA SIJUI NI MPE JIBU GANI WIFE AISEE. NAOMBENI BUSARA WAKUU WENZANGU MAANA'KE NAONA KAMA "NIMEKAMATIKA VILE"
cc:matola, miss chagga:


Utakamatika kama huna akili....tumia zako hapo, usichanganye na za mkeo.
 
Pole sana mkuu, naona mkeo anataka uumpandishe cheo mchepuko Wako awe mke mwenzie
Kwa kweli inashtusha , ebu endelea kukaanae vizur njia ya mwongo nifupi
Mzungushe, usikubali haraka

Swali: kwani na we uko tayar kumuoa uyo mchepuko?
 
cheki uongo unavyo tutesa yaani Amani ya moyo huna. Mawazo tele pole sana ila hiyo inafahamika bwana zama hizi kuwa na wanawake wengi sio sifa hayo mambo ya kizamani sasa kama unataka uishi karne hii kwa fikra za babu zetu mbona kasheshe
 
Huyo kashagundua tabia yako na amechoka kuumia maana ni muda mrefu anaona upo na huyo mwanamke na hauna dalili za kumuacha.

Umemtenda kosa kubwa sana mkeo na umemuumiza sana moyo wake, kua makini hata kujiua huyo anaweza.
 
We beba tu uwe na wake wawili maana mila si zinaruhusu. Ila uwe makini. Wewe mwambie poa tena kwa masikitiko makubwa.
 
Mkeo ana akili sana,amechoka kudhalilishwa na anakuomba tu isiwe siri tena bali muyaweke hadharani,zungumza na mkeo umalize hilo soo,mpeleleze ujue kwanini kakwambia hivyo,utubu na uzinzi uache.
 
You are making noise with capital letters.

BTT: Get them all, officiate your ................
 
kwanza dini yako inaruhusu kuoa mke zaid ya mmoja? swal la pili unahisi uko tayr kuoa mk wa pili?
swal la tatu mkeo ameshawah kuzungumzia kuhusu huyo rafik yake kutoolewa mpaka sasa na response yake ikawaje?
swal la mwisho kwann ulichepuka kwa bestfrend wa mkeo huon kama ndio umemtia nuks ya kutoolewa?
 
We beba tu uwe na wake wawili maana mila si zinaruhusu. Ila uwe makini. Wewe mwambie poa tena kwa masikitiko makubwa.

hahahaaa...unamaanisha sitaki nataka?!!!
 
kwanza dini yako inaruhusu kuoa mke zaid ya mmoja? swal la pili unahisi uko tayr kuoa mk wa pili?
swal la tatu mkeo ameshawah kuzungumzia kuhusu huyo rafik yake kutoolewa mpaka sasa na response yake ikawaje?
swal la mwisho kwann ulichepuka kwa bestfrend wa mkeo huon kama ndio umemtia nuks ya kutoolewa?

Dini hairuhusu ila mila zinaruhusu...nipo tayari kuongeza wa pili...nikichepuka bahati mbaya tu mkuu!!!
 
Mkeo ana akili sana,amechoka kudhalilishwa na anakuomba tu isiwe siri tena bali muyaweke hadharani,zungumza na mkeo umalize hilo soo,mpeleleze ujue kwanini kakwambia hivyo,utubu na uzinzi uache.

asante mkuu wangu!!!
 
Mbona jina lako ni gum kulisoma?
Mke wako kajua mienendo yako ana kutega tuu kwasababu hiyo habari anayokuambia ipo kwenye movie za kihindi na kinaigeria hainaga uhalisia kwasababu kila mtu ni mbinafsi by nature .Be smart
 
Back
Top Bottom