Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Imran Khan ameapishwa kuwa Waziri Mkuu wa Pakistan leo. Chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insat kimeshinda uchaguzi.
Kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa ameahidi kukomesha rushwa nchini humo.
Imran Khan alizaliwa 05 October 1952 kwenye familia yenye utajiri wa kati nchini Pakistan. Elimu yake ya msingi aliipata mjini Lahore na shule ya upili alipata Worcester Grammar School nchini Uingereza. Baada ya hapo alijiunga na Oxford University.
Imran Khan ni mcheza cricket mzuri sana. Akiwa Captain wa team ya Pakistan, walishinda Cricket World Cup 1992.
Mke wa kwanza wa Imran, Gemima Khan ambae walioana 1995 na kuachana 2004 anatoka kwenye familia yenye ushawishi mkubwa kwa chama cha Conservative nchini Uingereza. Gemina ametoka kwenye familia ya Goldsmith na mdogo wake wa kiume ni mmoja wa wabunge vijana wanaoaminiwa sana na chama.
Baada ya kuachana na Imran Gemima alikuwa mpenzi wa mcheza sinema maarufu Hugh Grant. Kwa sasa Gemima amerudia jina lake la kuzaliwa Gemima Goldsmith.
Safari ya Imran kwenye siasa ilianzia mbali. Vyama vya upinzani Tanzania msikate tamaa. Kuna siku ya kuapishwa na kuingia Ikulu.