Important: How to inspire manners to your children

Important: How to inspire manners to your children

Hizi ni moja kati ya zile thread ambazo zinatia shime ya akili, lets walk the talk.
 
Jambo la msingi kabisa ambalo tushaelezana na huwa tunakumbushana mara kwa mara ni kuwa hakuna mtu aliyemkamilifu. Na kwa sababu hiyo kukosea ni sehemu ya maisha na kutakuwepo tu hata iweje.

Lililo la muhimu zaidi ni kuweza kutambua, kukubali makosa, kuweza kuomba radhi, na kujifunza ili kutokurudia tena kosa/makosa.

Kwa hiyo daddy naye huwa anaomba radhi pale anapokosea kwa sababu binti anatambua kuwa nami ni binadamu. Na kwa vile Kiingereza ndo lugha kuu ndani ya himaya yetu maneno kama 'sorry sweetheart, my fault', 'oops..it's daddy's fault', 'my bad...that's on me'...na kadhalika ndo hutumika zaidi.

Pia ni kawaida kwa samahani za daddy kufuatiwa na kumbatio pamoja na busu shavuni. Ila kuna nyakati samahani za daddy lazima ziambatane na ziara za kwenda mall na kutia hasara kwenye akaunti😀.

Huwa sipendi kuwa mjeuri na mbishi inapokuja kwenye suala la mahusiano na binti. Sitaki kuwa mungu mtu nisiyekosea au hata nikikosea nikatae kukubali makosa yangu.

Kama mzazi mwajibikaji ni muhimu kuwa mfano bora kwa mtoto.
nimetamani
 
Ngoja nijaribu kuiweka kwa KISWAHILI maana kuna wengine hapa kama mimi lugha hii haipandi kivile
 
Thread nzuri nimejifunza kitu kitanisaidia kuwaongoza hawa wangu.
Hapo kwenye kugonga mlango binti yangu nlishamfundisha asiingie kwangu bila hodi, ila sasa mi nkiingia chumba chao huwa sigongi nimejifinza aisee.

Out of topic:Jamani mtoto wangu huwa anapenda kulia sana mpaka kuna wakati nashikwa hasira nampiga(japo sipendi).Kitu kidogo tu analia,mfano akishindwa kuchora mchoro flani atalia,akishindwa kuandika kitu wakati anafanya homework atalia mpaka kero.Naombeni mwelekezo hapo nimfanyaje.
 
Safi sana nice thread yani nimekuelewa aisee one day uje Kurasini tupate Lunch bills on me
 
Hiyo namba 9 sasa, ingawa watu wengi tunachukulia kumuomba mtoto msamaha ni kama uzungu zaidi au kujidhalilisha, but honestly kuomba msamaha hakuna umri. Watoto wapo very sensitive, na wana hisia kama tulizo nazo sisi wakubwa. Wanajua kuumia na hawapendi pia mtu amtendee kosa afu amuignore. Ni watu wazima, tunajua how it feels mtu akikukosea afu aonyeshe hajali, na watoto wana-feel hivyo hivyo

Above all, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mfundishe mtoto thamani ya msamaha, atajua kuwaomba msamaha na wengine once akikosea. Yani kuna muda tunalaumu kuna watu ni manunda, hata akikosea haombi msamaha, but kumbe hana msingi mzuri wa kitu msamaha


Kingine watoto wafundishwe ku-appreciate vitu wanavyofanyiwa, kusema "Ahsante". Hata kama tunafanya vitu vingi as part of majukumu/wajibu wetu na kuna muda wazazi wanaenda extra miles kuhakikisha kila kitu kuhusu watoto kiko sawa, but still watoto ni muhimu wajifunze kushukuru. Mzazi umetoka kazini mtoto kakupokea pochi or bag basi mshukuru, kakuvua soksi, mara akufulie leso, mshukuru kwa vyote. Kuna watu jamani hata umfanyiaje, yeye anaona tu ni wajibu wako. Utahangaika hata usiku kufanya chochote but yeye akhaaa, anaona kawaida tu. Yani hajuagi neno Ahsante hata iweje. Na hakuna kitu kibaya jamani kama mtu asiyejua ku-appreciate, utakata hadi tamaa ya kumfanyia mema

Wajengee watoto kujiamini, msifie " my baby is so cute", my baby can do this. Hata kama mtoto ni mzito kufanya kitu fulani, endelea kumtia moyo. Leo hawezi, kesho akijitahidi kwa 2,%, mwambie tu, do you see it baby, leo umepiga hatua nyingine mbele. Waambie jinsi unavyowapenda etc

La msingi zaidi, wafundishe na wakumbushe wanao kumtanguliza na kumtegemea Mungu kwa kila jambo. Nenda nao kanisani/msikitini, msome neno kwa pamoja, ombeni pamoja, waombee.
Ahsante HS
 
zamani nilpasua sahani au bakuli ya mama aliyokuwa amenunua wakati yupo shule baada ya kulipwa kwa kazi ya kufuma vitambaa vya uzi kwa mkuu wake wa shule, aisee nilfinywa kwenye paja na makofi juu, baadaye mama aliniambia NISAMEHE MWANANGU ni hasira na ugumu wa maisha. alijenga moyo wa kumpenda zaidi na nkilamba stick naelewa kweli nimemkasirisha..
Dah, hii imenigusa
 
Inawezekana sijazaa bado, but nina watoto ninaowalea na kulea ni zaidi ya kuzaa. Afu na mimi si nimelelewa na wazazi na ndugu, na ninaona wengine wanavyowalea watoto wao pia, so chochote kizuri nachokiona naki-adapt tu. Hata asiye na mtoto anaweza akashauri kitu kuhusu mtoto, kizuri kichukue, kibaya muachie. Inshallah na me ntakuwa mzazi siku moja
Kumbe ako singali[emoji6]
 
Back
Top Bottom