Nani ayafanyie kazi? hao hao wanaoshindwa kukusanya kodi, kushauri uwepo wa vipaumbele vya miradi na matokeo yake kwenye uchumi, hata kutunza takwimu hawawezi,.."imeanza kuyafanyia kazi" sentesi za kitoto kama hizi wakati mwingine zinaashiria akili ya anayeandika imedumaa!Wewe naona umeisoma report, siyo hawa wengine wanakurupuka hata kusoma hawajasoma. Nimeisoma taarifa nukta kwa nukta, mambo siyo mabaya kama ambavyo baadhi ya watu wanaamini. Kuna mapungufu ambayo kwenye taarifa kama hizi huwa yanaonyeshwa na pia kuna mapendekezo ambayo yakifanyiwa kazi kuna hatua kubwa itapigwa. Nimeona kwenye taarifa serikali imekubali kuyafanyia kazi na mengine imeanza kuyafanyia kazi.
Wizara ya fedha na hasa waziri wake hajaanza leo kuambiwa kuwa mwelekeo wa uchumi si mzuri, kila mwaka wabunge wanamwambia habari hii..mambo ya kujifunza kama kweli sisi sote tunataka uchumi wa nchi uimarike, turekebishe kasoro kwa kudeal na source, waziri Mpango hastahili kuendelea kuwa hapo, lakini nadhani ni muda sasa tuanze kujiuliza wanaowapata kina Mpango wanauwezo na hiyo kazi??? vetting za kutafuta wataalam kusaidia nchi yetu zina kasoro kubwa, hata kabla ya kum-replace Mpango, wao kwanza wawe replaced..vetting za mazoea hazitatupeleka popote kama nchi..toka awe waziri wa fedha kitu gani cha tofauti kizuri kwa nchi amefanya?? hao waliomtatfuta walijiridhisha na nini kumpa hiyo nafasi. Turekebishe kwanza mfumo na wanaofanya vetting kupata wataalamu kabla ya kupeleka majina kwa mteuzi, tutakuwa tumetatua 70% ya tatizo. Kwa hiyo tatizo si IMF pengine wala Mpango au Kichele, TATIZO ni WASAIDIZI WA MTEUZI KUPATA WATU WASIOFAA!!!