Imetosha sasa

Inauma sana! inahuzunisha sana! Utu uko wapi!? Nafikiri atakayethibitika kutenda hivyo adhabu ya kwanza naye atendewe vivyo hivyo kisha zifuate adhabu nyingine! Lo!
 
Moyo unauma sana mpaka nakosa la kusema, Mungu tusamehe.
 
Pole mtoto kwa mitihani ya dunia unaadhibika bila ya kosa maskini....
 
Inahuzunusha sana mie naona wanaokutwa na hatia bora wawe wanauliwa tu
 
Lawama zote ni kwa serekali haiko makini. Hivi hawa polisi wanaoishi kwa kodi zetu wanachoweza wao kwenye intelejisia yao ni maandamano na mikutano ya wapinzani lakini linapokuja swala la usalama wa raia hawawezi kitu. Shime wandugu umefika wakati wa kufanya mabadiliko ya kutoa hawa watawala vinginevyo hakuna nafuu yoyote kwa ndugu zetu hawa.
 
Kwanini binadamu tunatendeana unyama huu?. Roho imeniuma sana yaani amefanyiwa hivyo kisa yeye amezaliwa ni albino.HAPANA INATOSHA SASA.
 
Kama hii issue ipo kisiasa basi mungu atalipa mwaka huu huu...wabaya wote nawalaani katika yeye aumbaye mbingu na nchi na walaaniwe wote wanaoamini ushirikina kwa kutegemea damu na viungo vya wenzao...hakika mungu atajibu tu...damu ya mtu haiendi bure hata siku moja...
 
Kwa Serikali kukubali ujinga huu uendelee inaiweka nchi hii kwenye laana kubwa. Haiwezekani jamii ya Watanzania wenzetu wenye mapungufu kimaumbile wauwawe au kuongezewa ulemavu alafu tuendelee kujiita kisiwa cha amani. Amani gani?
 
Kikwete aseme ukweli, yeye in sehemu ya haya mauaji! Haiwezekani akawa na intelijensia ambayo huwa inaweza kugundua kuwa wapinzani wakiandamana kutatokea uvunjifu wa amani lakini hawawezi kugundua wauaji wa watanzania ambao yeye kama Rais amepewa dhamana ya kuwalindana Bado akakaa kimya Kimsingi, kwa kitendo tu cha watu kuendelea kufa yeye akiwa madarakani kilitosha kumlazimisha ajiuzuru kwa kushindwa kuilinda katiba inayosema wazi kuwa kila mtanzania ana Haki ya kuishi. Ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba hakuna mtanzania anayekosa Haki yake ya kuishi eti kwakuwa tu kuna mwanasiasa anataka kiungo chake ili ashinde uchaguzi. Kama hawezi kabisa kuzuia hali hii ajiuzuru. Hatakuwa wa kwanza kuachia ngazi Sikh chache kbla ya muda wake kuisha. Hata Mbeki alifanya hivyo. Ajenge heshima japo kwa njia hiyo. Hii ni aibu kubwa!
 
Watu sijui tuna roho za namna gani mtoto kama huyu unamkata mkono au unamuua bila huruma jamani.yana mwisho lakini pole sana kijana.mwenyezi Mungu atawaangamiza kwa uwezo wake inshaallah.
 
Kwanini nchi nzima siku moja tusiamue kuwaombea laana kwa Mwenyezi Mungu hawa wauaji!
 
Machozi yamenitoka kwa kweli lazima tufanye kitu sisi wananchi wenyewe serikali tuiachie maandamano!
 
Mi ushauri wangu ni hawa watu wapewa hifadhi ya ukimbizi Canada us Australia au UK lakini haya matangzo ya yatosha Mara haikubaliki haisaidii wahamishwe wawe salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…