Babra ... kwanza pole sana na yaliyokusibu toka jana ... nampa pole rafiki yako na naahidi kumjumuisha katika maombezi yangu ya leo.
Niseme tu kuwa nilikuwa nafutailia kisa hiki hatua kwa hatua tangu jana na nilisita kuchangia nikisubiri hatma ya janga lenyewe na kujizuia kuchangia kwa kufuata 'emotions' zangu zaidi ya uhalisia. Kiukweli jamaa amefanya makosa makubwa sana na ni tendo la haibu sana kwa wanaume hasa ukizingatia wanaume wenyewe wengi wameelimika kuhusu huo mfumo dume. Maoni yangu nahisi yatakuwa tofauti kidogo na wengine lkn naomba yaheshimiwe:
1. Ningekushauri umshauri rafiki yako achukue na afikie hatma ya maamuzi yake bila kuwa influenced na ndugu zake .... i mean mwacheni afikirie yeye mwenyewe kwa kina kwamba anachoamua ndicho na sio awe obliged kufuata emotions za ndugu zake; ninasema hivi nikiwa na kumbukumbu ya matukio kama haya ambapo ndugu huwa wanashawishi maamuzi magumu yachukuliwe lkn ndio wanakuja kuwa wa kwanza kuwasimanga na kuwacheka kwa maamuzi yao.
2. Nikichukulia pia kuwa huyo mumewe hilo ndio kosa kubwa na la kwanza kwa mkewe (kama nimekusoma vizuri) nadhani isingali kuwa busara kama atafikia uamuzi huu kwa ghafla namna hiyo ... we know devorce procedures takes time lkn binafsi nisingalishauri wafikie huko ... nashauri familia zao zikutane kwanza na kujadili hilo tatizo kama linaweza kutatulika then ni vyema na heri kuliko kufunga kabisa any room for reconciliation ... hatutakuwa tumetenda vyema kwa kweli!
3. Ningeshauri pia kama ni waumini wazuri then wawashirikishe viongozi wao wa dini .... ni vyema nafasi ya Muumba wetu ikaheshimiwa na sio tusukumwe na hisia zetu za kibinadamu!
@ Pearl ... dada najua inauma sana lkn kumshauri tu atafute mtu mwingine kwa sasa sidhani kama ni vizuri ... naamini kila mtu ameumizwa na tatizo hili lkn ni vyema busara ikatumika!
siku hizi kuna kautamaduni fulani ambapo watu huwa wanafurahia sana wanapoona ndoa zinavunjika ili ku-justify kwamba hakuna umuhimu wa ndoa ... i dont think this is true! kuna ambazo kweli haziwezekani hasa kama hazikustahili kuwa ndoa (haukuwa mpango wa Mungu) hivyo hizo zastahili kubatilishwa lkn kwa zile ambazo zaweza rekebishika then ningeshauri tujitahidi wanajamvi kushauri vizuri na kupunguza hasira na hisia. I'm sure this is gona be a very long debate .....
And He answered and said to them, Have you not read that He who made them at the beginning made them male and female, and said, For this reason a man shall leave his father and mother and be joined to his wife, and the two shall become one flesh? So then, they are no longer two but one flesh. Therefore what God has joined together, let not man separate.
Kudos Babra!
MDBD