Imeniuma nakunisikitisha sana

Imeniuma nakunisikitisha sana

Latifaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Posts
501
Reaction score
258
Nimekuja mkoa kusalimia nyumba ni kidogo nikakuta kuna msichana wa kazi chapakazi hadi raha nikampenda sana kwa Tabia yake ya kuchapa kazi nakujielewa yupo kazini hadi nikawa natamani nipate msichana kama huyu siku moja maana niko busy sana mimi.

Sasa tuje kwenye kilichonisikitisha hapa nyumba kuna kijana ndugu anaishi hapa kwa maza kama mtoto wanyumbani tuu kwa hiyo tumemzoea kama kaka yetu kabisaaa kuna kipindi Fulani aliuguua sana hadi akalazwa TB minongono ikasikika ameathirika maana yeye mwenyewe aliwaambia baadhi ya watu wake wakaribu majibu ya dokta tukamsikitikia sana hapo.

Kwakupenda totoz anatisha, kilichonihuzunisha nakunikitisha sana ni huyu binti wa kazi kaniambia mwenyewe kubwa huyu kaka ameshatembea nae alivyokuja tuu alimtongoza japo alimkatalia lakini baadae akamkubalia niliishiwa nguvu mbaya zaidi nahisi wametembea bila kondomu kwakua kuna kipindi alikua anamrusha roho huyu kaka kwakumwambia amepata ujauzito.

Sasa sijajua anaujauzito kweli au ni geresha kwa kweli nikimfikiria namuonea huruma hadi natamani kulia hili likaka nikiliangalia ndio sina hamu kwanini kumuangamiza binti wa watu makusudi jamani? Nilikuwa nahitaji sana mdada wa kazi, ila nimeingia hofu kubwa sana kumchukua maana mama alishaniambia kama nataka nimchukue sasa tatizo ni kwamba nikimtafakari namuonea huruma sana yaani binti wa miaka 20 tuu jamani imeniuma sana kwa kweli.
 
Ukiolewa na Pdidy mtaendana sana..
Cant imagine mmefundishwa na nani kuandika!
 
Last edited by a moderator:
Mambo ya watu hayo, hata ukimsikitikia itakusaidia nini? haibadilishi chochote! kujipa stress bureee! its too late!
 
Inasikitisha sasa go and prove it to doctor, after all unaweza kulala na bundi na ukaamka mwenye bahati sio kwamba hatoweza kufanya kazi balii itamchukua muda kidogo kurudi kuwa normal just tell her, na mwambie kakaenu kama kweli anajua status yake achunge hilo fagio lake la chuma sio kila sehemu anafagia tu sio poa
 
Kwanza pole sana, pili huna haja ya kukaa kimya huyo binti akapime kama ana ujauzito na kama ameathirika. Kama hajaathirika au kaathirika mchukue hatua muafaka za kumsaidia asiathirike au kuishi na hali yake hiyo ya kuwa muathirika.
 
Nenda kampime,ukijua majibu,u can tryna help her na ukamchukua ukamfanya kama mdogo wako kabisa na maisha yakaendelea Inshaallah
 
Kwanza nasikitika kwamba kwa mujibu wa maelezo yako unapenda lu-act kwa kubase kwenye monong'ono

Pili nasikitika unapoonyesha wazi kumlaumu huyo kaka kwamba kama minong'ono ni kweli basi atakuwa amemuambukiza huyo mdada...Questions!!
1. Huyo dada alitolewa bikira huyo mkaka?..kama sio ina maama kuwa alishafanya na wengine
2. Huyo kaka ndo mtu wa kwanza au wa mwisho kuumwa hiyo kitu?..jibu ni hapana walioathirika wapo wengine ambao wanaweza kumwambukiza mdada kabla na baada ya kuanzana na huyo mkaka
3. kuna mtu yeyote aliyempima huyo dada wakati anaanza kazi hapo home kwenu na kuthibitisha kwamba hajaambukizwa? no!!
4. Kuna ushahidi kuwa anatembea na huyo kaka peke yake? kwamba kama ni maambukizi hawezi kuyatoa kwingine?

tuombe hiyo minong'ono isiwe na ukweli rafiki













 
Huo ni unyanyapaa hata wewe SI ajabu muathirika. Kwani unamchukua ukalale nae ?
 
wanawake/wanaume wenye unyanyapaa na Mungu huwa anawajibu haraka sana.

kuna dada mmoja aliwahi nifuata nimpime binti yake wa kazi eti kisa anahofu atakuwa muathirika hivyo atawaambukiza na wao.

bahati mbaya mumewe ndio tulikuwa kwenye process za ushauri nasaha ili akubaliane na hali halisi amlete na mkewe wapime.
nilimuonea huruma sana yule dada lakini nilimchukia kwa kuwa ni mnyanyapaa!!

mwathirika wa vvu mkimjali na kumpenda hawezi kuchukua hatua yoyote ya kuwadhuru.
anahitaji elimu tu ya kujilinda na kulinda wengine
 
Mie nimebaki kuwashangaa tu hasa hao kina "mpeleke hospitali ukampime" akhaa..!

Mbona umemkuta hapo kwenu anapiga mzigo, nani alimpeleka kupima? Wangapi umekaa nao hawajapima?
Mkapime kwanza wewe na mumeo maana ukute tayari mnao wenu halafu akija dada mtasingizia ndio kawaambukiza.
 
Hata Wewe Siri Za Bwanako Ulienae Huzijui Zote.Unaweza Kukuta Kuna Watu Wanakuonea Na Wewe Huruma Mara2 Hata Ya Huyu Dada.
Kwahiyo Endelea Na Maisha Yako.Kila Mtu Atabeba Furushi Lake Mwenyewe.

N.B:siku nyingine katika uandishi wako husisahau tena kutuwekea nukta ili angalau tumeze mate.
 
Hata mimi nimeumia sana mchukue mkspime ili umuokoe.
 
Jf bwana Mimi sijamnyanyapaa mtu alichoniuzi nikumuambukiza makusudi inamaana hakutumia kondom ndio maana huyu bidada anapresha ya mimba, waathirika wa vvu sasa hivi wanaambukiza watu makusudi wakielezwA ukweli wanajidai wansnyanyapaliwa inauma kwa kweli kuuwa makusudi kwa vigezo uchwara eti kunyanyapaliwa
 
Back
Top Bottom