imenisikitisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

imenisikitisha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by queenkami, Oct 20, 2010.

 1. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  MWANAMKE AGEUKA BUBU GHAFLA BAADA YA KUNG'ATWA NA KUTOLEWA ULIMI WAKE ......  [​IMG]Binti aliyeng'atwa ulimi wake na kuwa bubu kwa sasa akionyesha jinsi alivyoondolewa ulimi wake
  [​IMG]Binti aliyeng'atwa ulimi wake mkazi wa mtaa wa Izia Sumbawanga mjini
  [​IMG] Hiki ni kipande cha Ulimi kilichong'atwa
  [​IMG]

  mama mzazi wa binti huyo Bi Salome kapele akionyesha kipande cha ulimi alichokihifadhi nyumbani kwake.


  WIVU wa kimapenzi wamsababishia ulemavu wa maisha mkazi wa Izia Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa Grace Senga (29)baada ya kung’atwa ulimi wake na kipande kutolewa wakati wakigombea bwana.  Mama mzazi wa binti huyo Salome kapele ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Izia aliwaeleza waandishi wa habari hizi jana waliofika nyumbani kwake kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5 usiku wakati binti yake huyo akitoka klabu ya pombe za kienyeji kunywa pombe.  Alisema kuwa akiwa amelala aligongewa mlango wa wasamaria wema kumjulisha juu ya tukio hilo la kuvamiwa kwa binti yake huyo japo hakuweza kutoka nje kwa kuhofu usalama wake kutoka kwa wavamizi hao .  "Kweli siku ya tukio kuwa vijana walikuja kunigongea mlango wangu na kunieleza kuwa motto wangu anapigwa ila sikuweza kutoka kwani niliogopa kuchomwa kisu katika ugomvi huo iwapo ningetoka……baada ya hapo alikuja kijana mwingine na kunieleza kuwa motto wangu amng’atwa ulimi basi sikutoka hadi alipokuja mme wake ndipo nilitoka na kwenda kumkuta akiwa hoi”


  Mwenyekiti huyo alisema baada ya kufika eneo la tukio alimwona binti yake huyo akiwa amelala chini jirani na eneo hilo la klabu ya pombe za kienyeji huku damu zikiwa zinamtoka kwa kasi .


  Kapele alisema kuwa baada ya hapo walikwenda kumkamata mwanamke huyo ambaye mbali ya kumng’ata ulimi binti huyo pia usiku huo huo alikuwa amemng’ata kidole mme wake ambaye alikuwa akimuuliza sababu za kulowa damu .


  Hata hivyo alisema mbali ya kumkamata mwanamke huyo na mpenzi wake huyo ambaye walishirikiana naye kumfanyia unyana huo binti huyo bado walilazimika kwenda eneo la tukio na kufanikiwa kuokota kipande cha ulimi ambacho baada ya kumng’ata alikitema chini.  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Isunto Mantage alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kinyama na kumtaja mwanamke huyo ambaye alitenda unyama huo kuwa ni Agnes Mandi (25) mkazi wa mtaa huo wa Izia pamoja na Mpenzi wake Mashaka Lupasha (32) pia mkazi wa mtaa huo wa Izia .


  Alisema kuwa watu hao wote wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumjeruhi mwanamke huyo wakiwa katika klabu cha pombe ya kienyeji kijulikanacho kama Katamakondo na kuwa kwa pamoja walisaidiana kumshambulia mwanamke huyo na kung’ata ulimi wake.


  Kwa mujibu wa kamanda Mantage kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mwanamke huyo aliyetendewa unyama huo alipata kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume huyo Lupasha kabla ya kutengana .


  Hivyo alisema kuwa kuwa siku hiyo ya tukio mwanamme huyo akiwa na mpenzi wake wa sasa Agnes Nandi alimkuta Grace Senga akiwa katika eneo hilo la pombe akiendelea kunywa pombe na ndipo ugomvi baina yao uliponza na kupelekea wapenzi hao kumchangia kwa kipigo huku wakimkaba koo .


  “Mbinu waliyotumia kumng’ata ulimi ni ile ya kumkaba koo na baada ya kuzidiwa alitoa ulimi wake nje mithiri ya mtu anayetaka kufa na ndipo wanamke huyo alisogea na kumng’ata ulimi wake na kutoa kipande cha ulimi ….hadi sasa binti huyo hawezi kuongea kabisa “


  Kamanda huyo alisema kuwa watuhumiwa hao wote wawili wamekamatwa na watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa

  source:Francis Godwin Iringa.
   
 2. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mmmh yani kabisa unakula nyama ya binadam mwenzio?:A S-frusty:Dunia imekwisha
   
 3. carina-TI

  carina-TI Senior Member

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha naomba nimpe pole huyu dada huyo jamaa kweli hana utu
   
 5. K

  Kipenzi Chao Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ole wao wanaopenda kula na kuliwa denda....!
   
 6. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  vipi tena?
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huu ni unyama uliokamaa! Suwanga live
   
 8. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kuna watu wako tofauti sana
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Jamani huu unyama gani tena this is so bad yaani what wivu wa mapenzi? huyo aliyemg'ata anatakwia selo hata kupiga kura hatuhitaji kura yake...such as barbaric act!
   
 10. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  I real dnt think huyu ni binadam kwakweli,vivu wa mapenzi wakati mtu mwenyewe wameshaachana?lol
   
 11. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135

  haiingii akilini kabisa sijui matapu tapu aliyokunywa yalimzidishia ukatili!
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Hospitali zinao uwezo wa kuurudisha ulimi kama utakuwa umenyofolewa ndani ya masaa ishirini na manne tu. Kwa hiyo huyo atakuwa amechelewa tu
   
 13. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  haaaaaaaaaaaaaaaa duh, dada pearl shikamooo na samahani kwa kwenda nje ya topic.
   
 14. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  yaani kaizer imeniacha hoi...eti hata kura yake hamuhitaji???? Duh! N to think that hawa ni wale wa kumpigia jk eh???? Ahahaha
   
 15. father-xmas

  father-xmas JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  huo si wivu ni ushetani...............!
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  OMG unyama wa kutisha
   
 17. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  malyaba vipi tena?
   
 18. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha jamani mwanadamu amekuwa zaidi ya mnyama!pity her
   
 19. Nchi Kavu

  Nchi Kavu JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 3,520
  Likes Received: 1,041
  Trophy Points: 280
  Najiuliza aliufikia vipi huo ulimi. Mambo mengine ya ajabu sana
   
 20. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mmmmmm watu wana roho mbaya zaidi ya wanyama, mmm so sad
   
Loading...