moyafricatz
JF-Expert Member
- Nov 27, 2015
- 2,905
- 4,944
Tafadhali mods msiunganishe na ule uzi mwingine.
Umeyasema yote yaliyokua Moyoni mwangu.Kipindi hiki vyombo vyetu vya ulinzi vimejitahidi sana tena sana!
Wakati msafara uliobeba mwili wa mpendwa wetu Jpm ukipita maeneo ya mkwajuni kuelekea magomeni mapipa,
Niliona Police wakiwasogeza wananchi walioingia barabarani na kuzuia msafara, kwanjia ya ustaarabu sana, waliwaondoa barabarani polepole bila kuwasukuma wala kuwaumiza, kiustaarabu na kiungwana sana mpaka nikashangaa!
Hapa tena naona mwanajeshi military police amembeba mlemavu wa miguu ili nae aweze kumuaga aliyekuwa Rais wake mpendwa Jpm. Kweli majeshi yetu yamepiga hatua kubwa sana! Nijambo jema la kupongeza!
Niwape kongole sana kwao!
Jpm
Apumzike kwa Amani,
Amina!
SawaIkikugusa sana unga nae juhudi
Tafadhali mods msiunganishe na ule uzi mwingine.View attachment 1730378