Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Imegundulika kwamba maskini anayeishi miongoni mwa matajiri hufa haraka kuliko masikini anayeishi miongoni mwa masikini wenzie.Mtu jana kalala njaa,anamka asubuhi unakutana na mtoto wa jirani anamwaga maini yaliyobaki jana jalalani.Unatembea kwa miguu kutoka kwako,jirani anakupita huku akikutimulia vumbi na ukicheki unaishi mitaa ya watu wazito hakuna daladala.Ukizingatia haya na ma-gap mengine mengi mtu unapata kihoro mpaka kufa.Ila mkijipanga sehemu masikini watupu,mambo mswano,hamna mnachozidiana na kama mnazidiana basi ni viji-gap vidogo vidogo tu,kiufupi mnafarijiana na kuridhika na hali zenu,inakuwa rahisi kumtuma mwanao John akaombe kiberiti kwa akina Juma na ndo maana uswazi akiingia tajiri mmoja,masikini wanasepa wenyewe bila hata kuambiwa.