Imefikia wapi kampeni dhidi ya dawa za kulevya?

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,977
2,200
Wakuu
Kipindi kifupi cha nyuma tulishuhudia ikianzishwa kampeni ya kupambana na kutokomeza dawa za kulevya kabisa hapa nchi, kampeni hii awali ilianzishwa na kusimamiwa mkuu wa mkoa wa Dar
Lakini alipata vikwazo na vigingi vingi toka kwa wapinzani wake binafisi ndani na nje ya ccm kwa njia alizotumia

Hii ilimlazimisha rais kuundwa tume itakayojihusisha na kupambana na biashara hii haramu, lakini hali imekuwa tofauti!

Imefikia wapi ile vita ya dawa za kulevya?
Tume inayoongozwa na Sianga inafanya shughuli zipi bila ya kutupa mrejesho?

Zile kesi za awali za watuhumiwa wa mwanzo nazo vp maendeleo yake?

Ndio wengi wetu tuliunga mkono tume hii ifanye kazi pasipo kutangaza majina hadharani, je ndio kusema kwamba hatupaswi kuwajua watuhumiwa?

Kama wanakamatwa kimya kimya, wanashitakiwa mahakama zipi?

Ukweli hali ya upatikanaji na utumiaji wa dawa za kulevya huku mtaani umerudi kama ilivyokuwa awali tena kwa kasi zaidi ya mwanzo
Tume imeifikisha wapi vita ya dawa za kulevya?
 
Back
Top Bottom