Leo vyombo vya habari vimeripoti kwamba imegundulika mitungi ya gesi hutumika kusafirishia madawa ya kulevya. Habari hii imeonekana kushangaza hata kamanda wa kikosi cha Polisi kinachopambana na biashara ya madawa ya kulevya afande Nzowa. Hata hivyo, jambo hili sio geni kwani miaka michache iliyopita ilikamatwa mitungi ya gesi pale kivukoni ikiwa na bangi ndani. Mitungi ile ilikuwa ikisafirishwa kwenda visiwani Comoro.
Tukiliangalia suala hili kwa mtazamo wa kifalsafa kwa kujenga mantiki (logic) tunawezaona kwa nini miaka ya hivi karibuni biashara ya mafuta na gesi ya kupikia imepamba moto. Kila kona ya miji yetu mikubwa utakutana na utitiri wa wauza na mawakala wa usambazaji gesi ya kupikia; hapa ukiona Oryx , pale utaona Lake gas , kule utakutana na Mihan gas , nyuma hapo pana puma gas na kule mbele utakuta pana Camel gas na nyinginezo.
Ukiingia ndani ya biashara hiyo utakutana na majina ya watoto na marafiki wa viongozi wa juu kabisa kitaifa. Wafanyabiashara hiyo wanajulikana sana. Watu hawa kama sio watoto wa viongozi wa juu kitaifa na ndani ya chama chetu (hapan' shaka, chama chetu mnakijua), basi ni wafadhiri wakuu wa sherehe na chaguzi za chama.
Aidha, tujikumbushe sakata la uhaba wa sukari hapa nchini mwaka juzi na mwaka jana. Serikali iliposema kuna uhaba mkubwa wa sukari nchini, wenye viwanda vya sukari nchini walisema wana akiba kubwa ya sukari kwenye maghala yao. Kutokana na uhaba huo wa kutengenezwa wa sukari na saruji ili bidi serikali itoe vibali vya kuagiza sukari na saruji nje ya nchi. Hapa ndipo, sukari ilibidi iingizwe nchini kwa wingi toka Brazil na Saruji ikatoka Pakstan. Kwa hoja za kifasafa, Brazil na Pakistan zinajulikana kwa biashara ya mihadarati. Tuliagiza sukari na saruji toka nchi hizo huku tukijua lengo letu ni nini na tunafa nini.
Kwa hiyo na kwa vyo vyote vile, watu hawa wenye kujishughurisha na biashara hii wanajulikana. Na ieleweke hapa kwamba sio kila mfanyabiashara ya mafuta na gesi ni zungu la unga la hasha. Wapo wengi wenye hofu ya Mungu ndani mwa mioyo yao. Hawa wanaona huruma sana na kuumia wanapoona mateja yanaongezeka kila uchao ndani ya jamii.