Imedhihirika, Lowassa Mguu Mmoja CCM, Mwingine Chadema

Kama issue ni mfumo ndio chanzo cha Ufisadi wadhani EL akiingia yeye au akimuweka mfuasi wake basi wataufuta huo mfumo uliopo au ndo watataka nao kwa wakati wao kwa kutumia mwamvuli wa mfumo mbovu basi wajimalizie vilivyobaki ikiwa ni pamoja na kurudisha gharama zao walizotumia kujieka kitini?
 
Maelezo yako hayana mafao kwa sababu unajaribu kuwagawa viongozi wa ngazi za juu wa ccm katika makundi mawili yaani waliosafi na mafisadi. Lakini ki ukweli ni kwamba hakuna aliye safi wote wako kundi moja, hapa unajaribu tu kumtetea mmoja wao dhidi ya mwingine, kwa kutoa mfano, jiulize lowasa fisadi na jk je? kuna ufisadi wa aina nyingi kama wa raslimali, utumiaji mbaya wa madaraka, kuigawa jamii kiitikadi nk nk. Ukiunganisha aina zote za ufisadi jk ni mfisadi hatari kuliko el

Big Up mkuu. JK watu wengi hawamsemi kama fisadi, lakini ukweli yeye ndo fisadi hodari na hatari. Hakuna mikataba ya kifisadi iliyosainiwa bila JK kubariki. Kuanzia IPTL JK alikuwa waziri wa Nishati na Madini. Hii mikataba ya juzi juzi yeye aidha alikuwa waziri wa mambo ya nje au Rais kabisa. Hata kuingia Ikulu aliingia kiufisadi. Angalia anavyowakingia kifua mafisadi wasichukuliwe hatua. JK ni mbaya kuliko hata Lowassa. Yeye anawapeleka mahakamani watu wanaotofautiana naye kisiasa (wasiokuwa wana mtandao). JK ana maovu mengi kuliko hata Lowassa. Nikirudi kwenye mada, Lowassa ni kiongozi mwenye msimamo na maamuzi. Ni jasiri kweli. Sio kama JK. Lakini dhambi ya ufisadi kwake haisafishiki kabisa. Akiingia CDM ndo kifo cha CDM kitaanzia hapo. Akitaka kujiunga na Chama cha upinzani aanzishe chake.
 
from january mpaka leo huu ni mkoa wa sita nafanya research kuhusu 2015 election na juu ya katiba mpya blv me or not lowasa watu wanamuitaji sana,hasa wanakumbuka uchapa kazi wake na mamuzi yasiosubiri files mezani..i thnk ana great chance kwa 2015.
 
source ya habari yangu ni mtu aliyekaribu sana na lowassa.

Lowassa amejiwekea option tatu, moja kubaki ccm kama hawatamwekea vikwazo vya kugombea urais, pili amuunge mkono mtu wake ndani ya ccm na ikitokea mtu wake amekosa ataenda chadema. Mazungumzo ya awali yalishafanyika na chadema kwamba itakuwa rahisi sana kumsafisha. Hoja kubwa ni kwamba tatizo la ufisadi si la mtu binafsi bali la mfumo uliojengwa na ccm, kwamba unaweza ukawa na wana ccm wabovu wakaja chadema wakawa wasafi kwani mfumo utakaojengwa na chadema hauruhusu ufisadi. Na nadhani hiyo ndio hoja si kwamba wana chadema ni malaika, hata kidogo. Watakachofanya ni kujenga mfumo mpya na taasisis huru zenye nguvu kupambana na rushwa. Akiwa ndani ya chadema lowassa hatakuwa kiongozi bali mtu wa kawaida ila anahitaji zaidi ulinzi azibughudhiwe maana anahofia wakiingia kina sitta watamsumbua sana.

Sasa mkakati mkubwa wa lowassa kwa sasa ni kuisaidia chadema indirectly ili izidi kuimarika na kuwa tisho la kweli kwa cm. Lengo ni nini? Inasemekana lengo ni kuwa ccm ikiwa imewekwa kitanzini hawatamudu kuruhusu mgawanyiko ndani ya chama hasa kuwaondoa wale wanaoonekana kama mafisadi. Itabidi waruhusu tu yule atakayeshinda kura za maoni ipite bila mizengwe ili chama kibaki kimoja. Lakini swali ni je, kama lowassa akipata tiketi ya ccm atawarudisha vipi wale ambao tayari wameshahamia chadema na kuijenga vilivyo? Wengine watasema kirahisi kuwa ni uzushi ila kama upo karibu na viongozi wakuu wa chadema au marafiki wa lowassa watakuambia kwa sasa lowassa yupo karibu sana na chadema na kuna agenda nzito ndani yake. Siku njema

ungebadili id yako ukajiita i-bangi badala ya ibange ningekuelewa
 
Lowasa akija CDM basi huo ndio utakuwa mwanzo mpya wa wananchi kuondoa imani na chama chochote cha siasa kwani lowasa ni fisadi sugu sasa how comes na yy aje tuungane? Ktk hili viongozi wa juu wa CDM wanatakiwa kujihadhari sana kwani CDM hatuna tena haja ya ushawishi wowote kutoka nje kwani tunajitosheleza kila idara so haitakuwa vyema tena hao mafisadi kuja ku-teplace tena nafasi huku CDM.

Moshi unafuka, sioni dalili ya kuuzima moto huu. Naona kwa mbaaali sana, mwewe anavikwa sura ya kuku na mama kuku. Ole vifaranga walioanguliwa na kuku mwenye urafiki na mwewe....
Labda naye ni mwewe aliyevishwa sura ya mama kuku!
Poleni sana mnaomini siasa, siasa kama mpira wa miguu, lolote laweza kutokea ndani ya dk 90.
Mungu wetu anaita sasa! Siku ipo mtakayomsikia, endeleeni kushikilia pembe zenu kwa nta, bado asubuhi!
Mungu wetu anaita!
 
hivi hatuna watu wengine wa kuwakweza mpaka kila siku tuongee habari za waarifu kuwapa madaraka? binafsi mpaka sasa sioni nani anatufaa natamani kama inawezekana watu waombe hii kazi mapema na tufanye evaluation hapahapa lakini sio kutupotezea muda na hawa wezi. naelewa jamii forum ni kioo cha viongozi na wengi wanaangalia tumesemaje wakiwatuma mawakala wao. CHADEMA mkileta ujinga hatutakubali na ndo utakuwa mwisho wa chama na sidhani kama cc wadanganyika safari hii tutakubali lazima tutawapiga mawe! hamuwezi kutujengea matumaini ya kupambana na ufisadi halafu ununuliwe na fenesi jaribuni muone alaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Haitakuwa ajabu mbona Fisadi Raisi Jakaya Kikwete alitaka kwenda huko mnamo mwaka 2005,
 
lowassa ni ccm for life yule....he bleeds CCM...haendi popote...atakufa nayo!!

Lowasa hatoki CCM katu,ndio nguzo yake.Sio bendera kufuata upepo,wala hakosi kujiimarisha zaidi akiwa ndani ya CCM.Uzoevu wake ndani ya chama unampa sifa ya kukielewa chama,nini afanye na nini asifanye kwa wakati gani.
 
Kazi ya CDM sasa na baada ya kuchukua nchi ni kusimamia rasilimali za nchi ili ziinufaishe nchi yetu. Suala la Lowasa kuja CDM sio hoja, ana uhuru wa kujiunga na chama chochote ili mradi ana sifa za kuwa mwanachama. Kama atakosa sifa hizo kwa CDM (nina hakika hana kwa sasa), kwa hakika hawezi kupata huo uanachama. CDM imeshafukuza wengi wa aina yake na tabia yake, hivyo sidhani kama wembe huo anaweza kuukwepa usimnyoe, labda atubu kwa toba ya kueleweka!
 
jamaa anataka uraisi kwa nguvu sijui ana nia ya kutatua matatizo yetu au nia ya kupata mali zaidi??
 
source ya habari yangu ni mtu aliyekaribu sana na lowassa.

Lowassa amejiwekea option tatu, moja kubaki ccm kama hawatamwekea vikwazo vya kugombea urais, pili amuunge mkono mtu wake ndani ya ccm na ikitokea mtu wake amekosa ataenda chadema. Mazungumzo ya awali yalishafanyika na chadema kwamba itakuwa rahisi sana kumsafisha. Hoja kubwa ni kwamba tatizo la ufisadi si la mtu binafsi bali la mfumo uliojengwa na ccm, kwamba unaweza ukawa na wana ccm wabovu wakaja chadema wakawa wasafi kwani mfumo utakaojengwa na chadema hauruhusu ufisadi. Na nadhani hiyo ndio hoja si kwamba wana chadema ni malaika, hata kidogo. Watakachofanya ni kujenga mfumo mpya na taasisis huru zenye nguvu kupambana na rushwa. Akiwa ndani ya chadema lowassa hatakuwa kiongozi bali mtu wa kawaida ila anahitaji zaidi ulinzi azibughudhiwe maana anahofia wakiingia kina sitta watamsumbua sana.

Sasa mkakati mkubwa wa lowassa kwa sasa ni kuisaidia chadema indirectly ili izidi kuimarika na kuwa tisho la kweli kwa cm. Lengo ni nini? Inasemekana lengo ni kuwa ccm ikiwa imewekwa kitanzini hawatamudu kuruhusu mgawanyiko ndani ya chama hasa kuwaondoa wale wanaoonekana kama mafisadi. Itabidi waruhusu tu yule atakayeshinda kura za maoni ipite bila mizengwe ili chama kibaki kimoja. Lakini swali ni je, kama lowassa akipata tiketi ya ccm atawarudisha vipi wale ambao tayari wameshahamia chadema na kuijenga vilivyo? Wengine watasema kirahisi kuwa ni uzushi ila kama upo karibu na viongozi wakuu wa chadema au marafiki wa lowassa watakuambia kwa sasa lowassa yupo karibu sana na chadema na kuna agenda nzito ndani yake. Siku njema

basi wengi tutakuwa madodoki kweli kama tutaamini kwama mla rushwa anaweza kukubali kujenga mfumo ambao utamzuia kula rushwa! Mla nyama ya mtu haachi ataendelea tu kula... Mla rushwa hawezi kuacha ataendelea tuu kula na hata siku moja hatakubali hoja ya kujenga mfumo wa kumzuia yeye kula au kufanya anachokipenda! Tunataka kiongozi atakayesimama na kutuambia kwamba anaichukia rushwa na wote tumwamini siyo kuangalia pembeni na kumcheka kwa kejeli.....
 
Akiamini katika nguvu ya Chadema na kubatizwa kwa maji ya bendera ya CDM, akatubu na kurejesha raslimali alizofisadi apokelewae.
 
Imekaa kiudaku zaidi!
Source?
Bila kujali hii habari ni ya kweli au la, hebu wana JF tuonyeshe tunatumia akili zetu kufikiri na sio mbumbumbu wala bendera fuata upepo na tuondokane hii tabia ya kikasuku ya kukimbilia ku-type neno ''source?'' kila habari inapoletwa hapa. Au kwa vile ni neno la kiingereza hatujui lina maana gani? Nadhani wengi wetu tunapodai source ya habari hata hatujui tunadai nini.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom