Kaka sina elimu kama Khadithi ulioitoa ni sahihi,Nzuri(hassan),dhaifu au ya uwongo....ila kwa Mujibu wa Qur-ani..Kiama ni moja kati ya Mambo amabayo Allah hakumpa elimu yake mtu yoyote..
Q79:42
Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
Q79:43
Una nini wewe hata uitaje?
Ufafanuzi; Una elimu gani wewe Muhammad hata uitaje khabari ya Kiama.
Q79:44
Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
Ufafanuzi: Kwa mola wako mlezi ndio kwenye habari zote za habari ya Kiama.
...Mtume ametoa dalili za kutokea kwake...kama vile kukithiri kwa wanawake wengi wanaokwenda uchi,watu kumiliki mali nyingi na kushindana kujenga majumba marefu..nk.....Pia kabla kiama kuja kuna mambo mengi yatatokea..kama Masih Dajjal, Kuja kwa Issah bin Mariam, Kutokea ukame mkubwa utakaosababisha na kina Juuj wa Maajuuj.
Ukiangaliza miaka 67 unayoisema ni kipindi kifupi kwa mambo yote hayo kuweza kutokea....Mwenyezi ndio mwenye elimu ya jambo hili kwa hio ni vyema tuka kaza kamba ya kufanya ibada na kulea vijana wetu vizuri...