Imani za kishirikina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imani za kishirikina

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Power to the People, Nov 3, 2009.

 1. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  People nahitaji msaada wenu. Kwa bahati mbaya sana tulifiwa na mama yetu muda mrefu sasa. Kabla ya hapo familia yetu ilikuwa ni ya watu wa kufanya kazi kwa bidii na kujituma. tulikuwa na miradi mingi sana and money was not an issue.

  lakini sasa tangu kufariki kwa mama baba yetu hajataka kujishughulisha kwa kitu chochote kile miradi imeporomoka, na amebaki akilaumu watu wanamloga ndio maana hafanikiwi. kila kukicha safari kwa waganga haziishi sisi kama watoto tumejaribu sana kumuomba na kumsihi aachane na mambo hayo lakini ni kama tumechochea moto. yuko tayari hata kuleta hao waganga na wachawi wake nyumbani na anataka hata kutujumuisha na sisi kwenye hizo rituals. lakini tumekataa kabisa.

  how can i make this stop for good, tunasali na tunaendelea kusali lakini mabadilko hayaonekani hali ndio inazidi kuwa mbaya. how cn we deal wit this Help Please
   
 2. T

  Tsidekenu Senior Member

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mungu huwa anajibu wala msikate tamaa, cha msingi msijiiingize kwenye hayo mambo nyie ambao hamjawahi maana mikataba yake ni vigumu sana kuivunja. inhitaji viongozi wa kanisa wenye upeo mkubwa sana wa kiroho. ninachoweza kukushauri nene kwa mchungaji mmoja anatwa Apostle MARY LUTUMBA - KANISA LAKE LINAITWA RIVERS OF LIFE MINISTRIES(MLIMA WA MABADILIKO). Nimeshuhudia kwa macho yangu watu wengi/familia nyingi zilizokuwa na matatizo kama yako zikifunguliwa kupitia uweza wa MUNGU. Kanisa lake liko Tabata au piga simu namba 0755 209727 au 0718 680122. Huwa pia anahubiri kila jtatu praise power radio saa tatu na nusu usiku. au kama wewe unafanya kazi city centre kuna lunch hour fellowship kila jumanne na alhamisi kuanzia saa saba hadi saa nane mchana pale ywca posta mpya. mtafute huyu mama ataweza kuwasaidia wote familia nzima kwa kuwa mungu amekuwa anamtumia sana.
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pelekeni Nguo yake moja kwa Mchungaji akaombewe! Akiivaa tu atazinduka kutoka fikra za kishetani
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ooooh...too bad for a person of his age...Ni ngumu sana kumshauri kitu kwa nafasi yenu kama watoto! Ila kama mnasali na mnamaanisha, basi Mungu wa Mbinguni atatenda miujiza katika muda ambao ninyi na yeye hamjui. Kwa muda huu msilazimishe kitu!
   
 5. October

  October JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Poleni sana kwa yaliyowasibu. Tafuteni mchungaji wakiroho awaombee kwa ajili ya kufunguliwa katika hizo nguvu za giza. Ila jihadharini sana msikubali kuingizwa kwenye mikataba ya kishetani kwa kushiriki katika uganga au kunywa dawa kutoka kwa waganga. Suluhisho kwa tatizo lenu ni kwa Mungu wa mbinguni peke yake, Mganga siku zote kazi yake ni kukuongezea mashetani zaidi na si kuyatoa.
   
 6. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Poleni sana, nadhani baba amekuwa physiologically affected kwa kufiwa na kipenzi mke wake. Endeleeni kuomba, Mungu atamfunua baba aondoke huko kwenye nguvu za giza.

  Hao waganga ni wezi tu ndiyo wanazidi kumaliza hicho kilichopo.

  Poleni sana.
   
 7. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Poleni kwa kumpoteza Mama.
  Hapa hakuna cha kulogwa wala nini. Kama Baba haendi kujishughulisha kwa kitu chochote kwanini miradi isiporomoke?. Mimi naona Baba amechanganyikiwa kumpoteza Mama na hakuna lingine. Tafuteni njia kumfanya akubaliane na hali iliyotokea ili akili yake irudi sawa na aanze kujishughulisha na miradi kama zamani muone kama pesa hazitaingia.
   
Loading...