Imani yako juu ya Mungu

Imani yako juu ya Mungu

Prince Naahjum_

Senior Member
Joined
Jun 13, 2016
Posts
139
Reaction score
125
1470764890450.jpg

Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake, wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao, maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana ambako hakukuwa na watu wala wanyama isipokuwa wadudu tu!

Alifika ufukweni amechoka sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko kwa kula matunda. Aliweza kujenga ka-kibanda kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala panga, hatimaye akaanza maisha mapya.

Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki. Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi. Alilala hapo hapo hadi usiku wa manane aliposhtushwa na joto kali lisilo la kawaida. Kumbe moto ulishika nyasi za kibanda chake na kibanda chote kikaungua moto.

Alilia sana na kumlaani sana Mungu kwa mateso hayo akisema "Hivi Mungu nimekukosea nini mpaka unitese hivi? Pamoja na shida zote hizi bado unaniongezea shida nyingine, umeteketeza makazi yangu ilhali nimejenga kwa shida, Hukuridhika kunitenga mbali na familia yangu nilipoishi kwa raha? Hukuridhika kuwaua rafiki zangu wote baharini? Kwanini Mungu umekuwa mkatili hivi? Bora nife tuu maana nimeshachoshwa na hizi shida!"

Akaendelea kulalamika na kumlaani Mungu hadi kukapambazuka.

Ilipofika asubuhi aliiona meli ikija kwa mbali kuelekea alipo, alishangaa maana hakuna meli yoyote inayoweza kwenda kisiwa kile labda kama imepotea njia. Meli ilipofika ufukweni yule kijana akaifuata, alienda moja kwa moja hadi kwa kapteni.

Kapteni akamwambia "tuliona moto mkali sana usiku tukahisi ni meli inawaka moto tukasema tuje ili tutoe msaada..kwa kweli tumetembea masaa mengi sana hadi kufika hapa, mshukuru Mungu maana ametumia moto kutuleta hapa" yule kijana kusikia hivyo alilia sana, akajilaumu kwa jinsi alivyo mnung'unikia Mungu.

Akaelewa kuwa Mungu ana njia nyingi za kuleta msaada kwa mtu. Akapiga magoti akatubu huku akimshukuru Mungu. Safari ya kurudi nyumbani ikaanza.

FUNDISHO:

Wakati mwingine Kuna mambo mabaya huwa yanatokea katika maisha yetu yanayotufanya tuone kama Mungu ametusahau. Tunamnung'unikia na kumlaumu Mungu bila kujua kuwa Mungu ana njia nyingi sana kutuletea msaada. Njia za Mungu huwa zinaonekana kama ujinga fulani, lakini kiukweli ujinga wa Mungu ndiyo akili kubwa ya mwisho ya mwanadamu. Tunasahau kuwa mabaya tunayokutana nayo yanafanya kazi kwa Manufaa ya hatma zetu.

Unaweza fukuzwa kazi usijue kumbe ndio unaelekea katika kazi bora zaidi, unaweza kuachwa na mtu uliyempenda sana ukadhani ndiyo mwisho wa maisha kumbe Mungu amekuandalia mtu mwingine mwenye mapenzi ya dhati mtakayefikia malengo ya kujenga familia, unaweza kukataliwa na kutengwa na ndugu kumbe Mungu amekuandalia watu-baki watakaofanikisha ufikie malengo yako pasipo masimango ya ndugu, hata rafiki wanaweza kukusaliti kumbe Mungu amewaondoa makusudi ili kukuepusha na mabaya waliyoyapanga juu yako.

Sasa usimlaumu Mungu ukadhani anakuzidishia matatizo, hapo anatafuta njia ya kuyaondoa hayo matatizo.

Mshukuru Mungu kwa Kila Jambo, kwakuwa hajawahi kukuwazia mabaya. Anakuwazia mema sikuzote.

PRINCE NAAHJUM ALSINA
 
Attachments

  • 1470764874223.jpg
    1470764874223.jpg
    16.3 KB · Views: 58
Mshukuru Mungu kwa Kila Jambo, kwakuwa hajawahi kukuwazia mabaya. Anakuwazia mema sikuzote.

Huyo mungu alikuwa wapi wakati Anathe Msuya anachinjwa kama mbuzi huku mwanae akiwa ndani ya nyumba na kumshuhudia mama yake asubuhi akiwa anaogelea kwenye dimbwi la damu?

Huyo mungu alikuwa wapi wakati tumbo la Mwangosi linafumuliwa na bunduki la kufyatulia mabomu ya machozi?

Bi. Anathe na Bw. David nao wamshukuru mungu kwa yaliyowapata eh?
 
hapana.mtoto wa aneth akikua amshukuru Mungu kwa kila jambo...na mke wa mwangosi na wanae pia wamshukuru mungu kwa kila jambo.
kwani imeandikwa "furahini katika majaribu na dhiki pia kwani kazi ya dhiki ni kuleta saburi,na saburi huleta uthabiti wa moyo na kamwe tumaini halitahayarishi.
so kwa hayo yote yalowapata wamshukuru Mungu na kufurahi wakiendelea kumuamini na kumtumaini kwani hawajui kawaandalia nini mbeleni baada ya kuruhusu hayo..kamwe hawatahayarika!!!
 
Amshukuru mungu? Kwa lipi? Kwa kushindwa kuwashinda na kuwalegeza hao wachinjaji wa mama yake?

Umajinuni huo!
 
Amshukuru mungu? Kwa lipi? Kwa kushindwa kuwashinda na kuwalegeza hao wachinjaji wa mama yake?

Umajinuni huo!
Everything happen for a reason..kwaio kila anayepatwa na shida anapaswa kumlaumu Mungu?
Katika maisha kuna shida na raha unapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo haijalishi.
 
Everything happen for a reason..kwaio kila anayepatwa na shida anapaswa kumlaumu Mungu?
Katika maisha kuna shida na raha unapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo haijalishi.

Lakini kwa nini mungu muweza wa yote na mwenye upendo na huruma aruhusu shida, hususan kwa wasiojiweza na wasio na hatia au kosa lolote?

Hivi huyo mungu hakumuonea huruma mtoto wa Anathe? Mbona mimi nimemuonea huruma sana na ningekuwa na uwezo ningezuia yaliyomtokea mama yake kutokea.

Kwa nini mungu hakuzuia yasitokee?

Yaani mtu kachinjwa kama mbuzi halafu mungu muweza wa yote kajikalia tu na hakufanya chochote? Really? Seriously?
 
Mjue duniani kuna Shetani na ndiye mungu wa dunia hii. Yeye anatawala system ya dunia hii ndiyo maana watu wanachinjana kila siku na huku tuendako ndio kuchinjana kutaongezeka. Kazi ya shetani ni kuharibu kile Mungu alichokiumba ambaye ni mwanadamu. Sasa basi kwa sababu ya sisi kumwacha Mungu, shetani anapata nafasi kutuangamiza maana tunakuwa hatuna ulinzi wa Kimungu maana kwa ajili ya maovu yetu au dhambi zetu Mungu anatugeuzia kisogo na shetani anapata mda wa kutungamiza. Mungu na dhambi ni mbalimbali. Mungu hapendi dhambi, yeye ni mwenye haki.
 
Lakini kwa nini mungu muweza wa yote na mwenye upendo na huruma aruhusu shida, hususan kwa wasiojiweza na wasio na hatia au kosa lolote?

Hivi huyo mungu hakumuonea huruma mtoto wa Anathe? Mbona mimi nimemuonea huruma sana na ningekuwa na uwezo ningezuia yaliyomtokea mama yake kutokea.

Kwa nini mungu hakuzuia yasitokee?

Yaani mtu kachinjwa kama mbuzi halafu mungu muweza wa yote kajikalia tu na hakufanya chochote? Really? Seriously?
Haikutokea labda kwa sababu Mungu hana uruma au hampendi mtoto wa aneth ila anamakusudi yke sisi binadamu ni ngumu kufahamu kusudi ya Mungu, Shida zipo kutujaribu wanadamu..
Unaweza kuta kuna vitu vya ndani sana kuhusu kifo cha aneth ndio maana hii issue bado inasiri kubwa ambayo sisi hatujui"(mambo yakifamilia)

Mtoto kwa umri wake ni mapema sana kuachwa na mzazi wake na inasikitisha lkn ndio hvo pia duniani kunatokea mambo mengi hata mabaya zaid ya hili na Mungu yupo.

Mm kama mkristo tumefundishwa yatupasa kushukuru kwa kila jambo.
Ndio maana wakristo husema "Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la bwana LIBARIKIWE" haijalishi mtu alikufa kifo cha aina gani
 
A whole lot of tripe!
 
Lakini kwa nini mungu muweza wa yote na mwenye upendo na huruma aruhusu shida, hususan kwa wasiojiweza na wasio na hatia au kosa lolote?

Hivi huyo mungu hakumuonea huruma mtoto wa Anathe? Mbona mimi nimemuonea huruma sana na ningekuwa na uwezo ningezuia yaliyomtokea mama yake kutokea.

Kwa nini mungu hakuzuia yasitokee?

Yaani mtu kachinjwa kama mbuzi halafu mungu muweza wa yote kajikalia tu na hakufanya chochote? Really? Seriously?
Imeandikwa wapi kua mungu ni muweza wa yote, mwenye upendo na huruma etc.?!
 
Back
Top Bottom