Imani ya Watanzania kwa Rais Samia yaendelea kuongezeka

Imani ya Watanzania kwa Rais Samia yaendelea kuongezeka

Kwa Sasa mkulima anafurahia jasho lake chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais wetu mpendwa mama Samia kwa kupata Bei nzuri ya mazao yake tangia wakati wa mavuno
Nani kakudanganya? Wakulima washauza mazao yao tangu mwaka jana sasa hivi wanakula msoto kama sisi tu.. sasa hivi mazao yote yapo kwa walanguzi
 
Ndugu zangu watanzania,

Huo ndio ukweli ambao unaendelea kujidhihirisha mitaani kupitia maongezi ya watu, watanzania wanaendelea kumwamini Sana Rais Samia na serikali Yake, matumaini ya watanzania Ni makubwa Sana chini ya uongozi shupavu wa Rais Samia.

Rais Samia Ameendelea kujizolea umaarufu, na uungwaji mkono, watetezi wa Rais Samia mitaani wanaongezeka siku Hadi siku bila kujari vyama vyao,Rais Samia anasemewa kwa mema na watanzania wote,Kila litakapotajwa jina la Rais Samia mitaani unaona Tabasamu Katika nyuso za watanzania na furaha mioyoni mwao.

Rais Samia Ni Nyota imulikayo gizani na kuleta matumaini kwa watu wote waitazamayo juu ya kusonga mbele na Kuendelea na safari Yao, ameleta matumaini katika maisha ya watanzania,ameponya wenye majeraha ,amewapa faraja wenye maumivu na Amejenga kuaminiana na kusikilizana miongoni mwa watanzania,ndio sababu unaona kila mtu atakaye hojiwa na chombo chochote Cha habari au yeyote yule unaona anamsemea mazuri Rais samia.

Rais Samia anapendwa na kukubalika na watanzania Ni hakuna mfano , utendaji kazi na uchapa kazi wake umezikonga nyoyo za watanzania,uzalendo wake umeziteka nyoyo za watanzania,hekima busara na upendo uliojaa katika kifua Cha Rais Samia umewafanya watanzania watamani uchaguzi ufike haraka ili wampigie kura Rais Samia .Hakika Rais Samia Amebarikiwa Sana na kuifanya Tanzania kuwa yenye baraka na Neema kwa kila jambo.

Kazi Iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

0742-676627
WEWE ANZISHA BLOG YAKO UWE UNAPOST UCHAWA WAKO HUKO! Humu unatufanya tushindwe kufanya uchambuzi wenye uhalisia!
 
Kusema pesa zimepigwa zimepelekwa China na hachukui hatua Ni udhaifu mkubwa
 
WEWE ANZISHA BLOG YAKO UWE UNAPOST UCHAWA WAKO HUKO! Humu unatufanya tushindwe kufanya uchambuzi wenye uhalisia!
Hili Ni jukwaa huru au ukitaka wewe ndiye anzisha jukwaa lako ili ukafanyie uchaambuzi wako
 
Kusema pesa zimepigwa zimepelekwa China na hachukui hatua Ni udhaifu mkubwa
Ukiona Rais katamka na kusema hayo hadharani ujuwe kuwa Tayari hatua zinaendelea kuchukuliwa na wahusika wanakuwa kwenye macho ya vyombo vyetu vya Ulinzi kwa upelelezi na uchunguzi wa kina
 
Huyu jamaa hakuna kitu anakijua
Mimi Ni mkulima ninayeishi kwa kilimo kwa hiyo nachokuwa nakizungumza nakuwa nakifahamu vizuri tofauti na wewe uliyejibanza mjini na kulia Lia Bei za Mchele na unga kupanda wakati hujuwi hata gharama anazotumia mkulima mpaka avune mazao yake
 
Nyie wakulima ndio mnauza mchele kilo 3000?
Kwanza nikuulize wewe Ni mkulima? Maana nisije kuwa nakubebesha hoja na majibu yaliyokuzidi kimo kwa kuwa tu hujuwi Wala kuwahi kuwa na Shamba mahali popote pale
 
Kwanza nikuulize wewe Ni mkulima? Maana nisije kuwa nakubebesha hoja na majibu yaliyokuzidi kimo kwa kuwa tu hujuwi Wala kuwahi kuwa na Shamba mahali popote pale
Nalima mkuu, nipo sumbawanga huku vijijini nalima mahindi, nashangaa watu niliwauzia debe sh8000 Leo wanayauza 22000
 
Nalima mkuu, nipo sumbawanga huku vijijini nalima mahindi, nashangaa watu niliwauzia debe sh8000 Leo wanayauza 22000
Sumbawanga sehemu gani huko? Tunko,miangalia,laela,ndelema, Lusaka,kalambanzite,mpui ,kaengesa? Upo wapi huko,maana hiyo Bei umedanagaya hapa.
 
Mimi Ni mkulima ninayeishi kwa kilimo kwa hiyo nachokuwa nakizungumza nakuwa nakifahamu vizuri tofauti na wewe uliyejibanza mjini na kulia Lia Bei za Mchele na unga kupanda wakati hujuwi hata gharama anazotumia mkulima mpaka avune mazao yake

Ww ni mkulima wa ajabu, wakulima wenzako wamekuja bungeni kudai atleast serikali iwaangalie Kwa jicho la huruma then na ww unakuja na porojo zako

Watu kama nyie ndio mnafanya tuzidi kuibiwa na viongozi wazidi kuwa mafisisadi

Mkulima wa korosho ameuza kilo 1200, ww unakuja na porojo za ajabu kabisa

Nenda kwenye pamba, nenda kwenye mahindi, Debe wameuza elf kumi,

Unajua sh ngapi mjini? No elf 25, je hiyo elf 15 ya ziada imeenda Kwa nani?
 
Hao wakulima walikuja na Alama kwenye nyuso zao? Maana sisi wakulima tunaendelea kumshukuru mh Rais kwa kutufuta machozi na kutufanya tufaidike na jasho letu lililokuwa linaliwa na waliokimvulini kwa miaka mingi Sana na kutuacha tukiendelea kuwa maskini wa vipato kwa miaka mingi Sana,kilimo Ni biashara Hakuna anayependa biashara ya kumletea hasara kila siku
 
Ww endelea kusifia ujinga

Chawa wenzako uwa wanajibu hoja ambazo zinakuwa zimetoka na sio kuja na iyena iyena
 
Back
Top Bottom